Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Ali Muhsin el-Beruani

external-link copy
28 : 8

وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَآ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَأَوۡلَٰدُكُمۡ فِتۡنَةٞ وَأَنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥٓ أَجۡرٌ عَظِيمٞ

Na jueni ya kwamba mali zenu na wana wenu ni Fitna (mtihani), na kwamba kwa Mwenyezi Mungu upo ujira mkubwa. info

Enyi Waumini, wenye kusadiki! Jueni kuwa fitna ya nafsi zenu inatokana na kupita mpaka katika mapenzi yenu kwa watoto wenu na mali yenu. Basi isiwe kupenda kwenu kuyapenda mali na wenenu yakazidi kuliko mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hayo yatakuharibieni mambo yenu. Na jueni kuwa malipo ya Mwenyezi Mungu yanakutosheni kuliko mali na watoto.

التفاسير: