Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Ali Muhsin el-Beruani

external-link copy
45 : 7

ٱلَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبۡغُونَهَا عِوَجٗا وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ كَٰفِرُونَ

Wale ambao walikuwa wakizuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, na wakataka kuipotosha, nao wanaikanusha Akhera. info

Hawa madhaalimu ndio wanao wazuia watu wasende kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu wa Haki, nayo ndiyo Imani na kutenda mema; na wanaweka vikwazo, na shakashaka, ili hiyo Njia yende upogo iwapoteze watu wasiweze kuifuata. Na hao wanaikanusha Akhera hawaiogopi adhabu ya Mwenyezi Mungu.

التفاسير: