Kila kiliomo katika mbingu na kiliomo katika ardhi kinamtakasa Mwenyezi Mungu na kila kisicho kuwa ni laiki yake. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye kuvishinda vitu vyote, Mwenye hikima iliyo fika ukomo.
Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigania kutaka kulinyanyua Neno lake nao wameshikamana kitu kimoja, kama kwamba wao ni jengo lilio simama imara.
Ewe Muhammad! Kumbuka pale Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Kwa nini mnaniudhi mimi, na hali nyinyi mnajua kwamba hakika mimi ni Mjumbe niliye tumwa na Mwenyezi Mungu nije kwenu? Walipo endelea na kuiacha Haki, Mwenyezi Mungu alizipotoa nyoyo zao zisipokee uwongofu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu walio toka kwenye ut'iifu wake.