Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Ali Muhsin el-Beruani

Al-Fil

external-link copy
1 : 105

أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصۡحَٰبِ ٱلۡفِيلِ

Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? [1] info

[1] Hakika, ewe Muhammad, unajua kwa ujuzi usio ingiliwa na shaka yoyote, alivyo fanya Mola wako Mlezi kuwafanyia wale watu wenye tembo (ndovu), wakataka kuishambulia Nyumba takatifu ya Al-Kaaba.

التفاسير:

external-link copy
2 : 105

أَلَمۡ يَجۡعَلۡ كَيۡدَهُمۡ فِي تَضۡلِيلٖ

Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? [2] info

[2] Unajua ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu amejaalia juhudi yao kutaka kuibomoa Al-Kaaba ivize na ipotelee mbali. Juhudi yao ikapeperuka, na wao wasipate makusudio yao.

التفاسير:

external-link copy
3 : 105

وَأَرۡسَلَ عَلَيۡهِمۡ طَيۡرًا أَبَابِيلَ

Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, [3] info

[3] Na Mwenyezi Mungu aliwasalitisha na majeshi ya ndege yaliyo watokea makundi kwa makundi yakifuatana, na yakawazunguka kila upande.

التفاسير:

external-link copy
4 : 105

تَرۡمِيهِم بِحِجَارَةٖ مِّن سِجِّيلٖ

Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, [4] info

[4] Wakiwatupia mawe kutoka Jahannamu.

التفاسير:

external-link copy
5 : 105

فَجَعَلَهُمۡ كَعَصۡفٖ مَّأۡكُولِۭ

Akawafanya kama majani yaliyo liwa! [5] info

[5] Akawafanya kama majani ya mimea yaliyo sibiwa yakatilifu.

التفاسير: