Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

At-Tin

external-link copy
1 : 95

وَٱلتِّينِ وَٱلزَّيۡتُونِ

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa tini na zaituni, nayo ni miongoni mwa matunda yanayojulikana. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 95

وَطُورِ سِينِينَ

Na Anaapa kwa jabali la Ṭūr Sīnā’ ambalo Mwenyezi Mungu Alisema na Mūsā juu yake. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 95

وَهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ ٱلۡأَمِينِ

Na Anaapa kwa Mji huu wa amani, usiokuwa na mambo ya kutisha. Nao ni mji wa Makkah, chimbuko la Uislamu. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 95

لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِيٓ أَحۡسَنِ تَقۡوِيمٖ

Hakika Tumemuumba binadamu katika sura nzuri. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 95

ثُمَّ رَدَدۡنَٰهُ أَسۡفَلَ سَٰفِلِينَ

Kisha Tutampeleka Motoni akiwa hakumtii Mweyezi Mungu na hakuwafuata Mitume. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 95

إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فَلَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونٖ

Isipokuwa wale walioamini na wakafanya amali njema; wao watakuwa na malipo makubwa yasiyokatika wala kupungua. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 95

فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعۡدُ بِٱلدِّينِ

Ni lipi linalokupelekea wewe, ewe binadamu, kukanusha kufufuliwa na kulipwa, hali ya kuwa kuna dalili wazi kwamba Mwenyezi Mungu Ana uweza wa kufanya hayo? info
التفاسير:

external-link copy
8 : 95

أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِأَحۡكَمِ ٱلۡحَٰكِمِينَ

Je, Hakuwa Mwenyezi Mungu , Ambaye Ameiweka Siku hii kutoa uamuzi baina ya watu, ni muadilifu zaidi ya wanaosifika kuwa ni waadilifu katika kila Alichokiumba? Kwani? Alikuwa. Basi wataachwa viumbe rebe: hawaamrishwi wala hawakatazwi wala hawalipwi kwa mema wala hawateswi kwa mabaya? Hilo si sahihi wala haliwi. info
التفاسير: