Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
152 : 6

وَلَا تَقۡرَبُواْ مَالَ ٱلۡيَتِيمِ إِلَّا بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ أَشُدَّهُۥۚ وَأَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ وَٱلۡمِيزَانَ بِٱلۡقِسۡطِۖ لَا نُكَلِّفُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَاۖ وَإِذَا قُلۡتُمۡ فَٱعۡدِلُواْ وَلَوۡ كَانَ ذَا قُرۡبَىٰۖ وَبِعَهۡدِ ٱللَّهِ أَوۡفُواْۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ

«Wala msiyasogelee, enyi wasimamizi, mali ya yatima isipokuwa kwa namana ya kuyatengeneza na kuyafanya yenye faida, mpaka atakapofikia myaka ya kubaleghe na awe mwangalifu. Na pindi afikiapo umri huo, mpeni mali yake. Na tekelezeni vipimo na mizani kwa usawa kwa namna ambayo utekelezaji utakuwa umefanyika kwa ukamilifu. Na mtakapojibidiisha uwezo wenu, hapana ubaya kwenu katika yale ambayo huenda yakawa na upungufu upande wenu. Kwani hatumlazimishi mtu isipokuwa uwezo wake. Na msemapo, basi jitahidini katika maneno yenu kuchunga usawa pasi na kupotoka kwenye haki kwenye utoaji habari au ushahidi au hukumu au kwenye uombezi, hata kama yule ambaye neno hilo linamuhusu yeye ana ujamaa na nyinyi, msilemee upande wake bila ya haki. Na tekelezeni yale aliyowaagiza mufanye ya kujilazimisha na sheria Yake. Hukumu hizo mlizosomewa, Mola wenu Amewausia mzifuate kwa matarajio kwmba mkumbuke mwisho wa mambo yenu. info
التفاسير:

external-link copy
153 : 6

وَأَنَّ هَٰذَا صِرَٰطِي مُسۡتَقِيمٗا فَٱتَّبِعُوهُۖ وَلَا تَتَّبِعُواْ ٱلسُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمۡ عَن سَبِيلِهِۦۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ

«Na miongoni mwa mambo aliyowausia Mwenyezi Mungu ni kwamba huu Uislamu ndio njia ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, iliyolingana sawa. Basi ifuateni wala msifuate njia za upotevu zikawatawanya na kuwaepusha na njia ya Mwenyezi Mungu iliyolingana sawa. Muelekeo huo upande wa njia nyofu, ndio Aliowausia nao Mwenyzi Mungu ili mjikinge na adhabu Yake kwa kuyatekeleza maamrisho Yake na kijitenga na makatazo Yake.» info
التفاسير:

external-link copy
154 : 6

ثُمَّ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ تَمَامًا عَلَى ٱلَّذِيٓ أَحۡسَنَ وَتَفۡصِيلٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لَّعَلَّهُم بِلِقَآءِ رَبِّهِمۡ يُؤۡمِنُونَ

Kisha sema, ewe Mtume, uwaambie hawa washirikina, «Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ndiye Aliyempa Mūsā Taurati, kwa kuzitimiza neema Zake kwa watu wa mila yake wanaofanya wema, na kwa kufafanua kila kitu katika mambo ya dini yao, na kuwapa uongofu na muelekeo wa njia iliyolingana sawa, na kuwarehemu, kwa matumaini kuwa watakubali kwamba kuna kufufuliwa baada ya kufa na kuna hesabu na malipo, na hilo liwafanya watende mema. info
التفاسير:

external-link copy
155 : 6

وَهَٰذَا كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ مُبَارَكٞ فَٱتَّبِعُوهُ وَٱتَّقُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Na hii Qur’ani ni kitabu tulichokiteremsha kwa Nabii wetu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Kheri yeke ni nyingi. Basi kifuateni kwa yale anayowaamrisha na kuwakataza. Na muogopeni Mwenyezi Mungu msije mkaenda kinyume na amri Yake yoyote, kwa matumaini kuwa mtarehemewa na mtaokolewa na adhabu Yake na mpate malipo Yake mema. info
التفاسير:

external-link copy
156 : 6

أَن تَقُولُوٓاْ إِنَّمَآ أُنزِلَ ٱلۡكِتَٰبُ عَلَىٰ طَآئِفَتَيۡنِ مِن قَبۡلِنَا وَإِن كُنَّا عَن دِرَاسَتِهِمۡ لَغَٰفِلِينَ

Na tumeiteremsha hii Qur’ani, ili msije mkasema, enyi makafiri wa Kiaarabu, «Hakika Kitabu kutoka mbinguni waliteremshiwa Mayahudi na Wanaswara; na sisi tuna mambo ya kutushughulisha kutowahi kuvisoma vitabu vyao; na sisi hatuna ujuzi navyo wala maarifa.» info
التفاسير:

external-link copy
157 : 6

أَوۡ تَقُولُواْ لَوۡ أَنَّآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا ٱلۡكِتَٰبُ لَكُنَّآ أَهۡدَىٰ مِنۡهُمۡۚ فَقَدۡ جَآءَكُم بَيِّنَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞۚ فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَصَدَفَ عَنۡهَاۗ سَنَجۡزِي ٱلَّذِينَ يَصۡدِفُونَ عَنۡ ءَايَٰتِنَا سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ بِمَا كَانُواْ يَصۡدِفُونَ

Na ili msije mkasema, enyi washirikina, «Lau kama sisi tuliteremshiwa kitabu kutoka mbinguni, kama walivyoteremshiwa Mayahudi na Wanaswara, tungalikuwa na muelekeo madhubuti sana kwenye njia ya haki kuliko wao.» Hakika kimewajia Kitabu kwa lugha ya Kiarabu chenye ufafanuzi. Na hiyo ni hoja iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu, ni muongozo wa njia ya haki na ni rehema kwa umma huu. Na hapana yoyote mbaya wa dhuluma na uadui kuliko yule aliyezikanusha hoja za Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na akazipa mgongo. Basi hawa wenye kupa mgongo tutawatesa mateso makubwa kwenye Moto wa Jahanamu, kwa sababu ya kuzipa mgongo kwao aya zetu na kuzuia kwao njia zetu. info
التفاسير: