Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

external-link copy
19 : 59

وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ نَسُواْ ٱللَّهَ فَأَنسَىٰهُمۡ أَنفُسَهُمۡۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ

Na msiwe, enyi Waumini, kama wale walioacha kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu Aliyoipasisha juu yao, na kwa sababu hiyo Akawasahaulisha wao kujifanyia wema nafsi zao kwa kufanya matendo mema yenye kuwaokoa wao na adhabu ya Siku ya Kiyama. Hao ndio wenye kusifika kwa uasi, wenye kutoka nje ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu na utiifu kwa Mtume Wake. info
التفاسير: