Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

external-link copy
11 : 59

۞ أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ نَافَقُواْ يَقُولُونَ لِإِخۡوَٰنِهِمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَئِنۡ أُخۡرِجۡتُمۡ لَنَخۡرُجَنَّ مَعَكُمۡ وَلَا نُطِيعُ فِيكُمۡ أَحَدًا أَبَدٗا وَإِن قُوتِلۡتُمۡ لَنَنصُرَنَّكُمۡ وَٱللَّهُ يَشۡهَدُ إِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ

Je huwatazami hao wanafiki wanawaambia ndugu zao katika ukafiri miongoni mwa Mayahudi wa Banū al Naḍī, «Tunaapa kwamba Muhammad na walio pamoja na yeye wakiwatoa kutoka majumbani mwenu tutatoka na nyinyi! Na hatutamfuata yoyote kuhusu nyinyi anayetutaka tusiwasaidie au tuache kutoka pamoja na nyinyi, na wakipigana na nyinyi tutawasaidia juu yao?» na Mwenyezi Mungu Anashuhudia kwamba wanafiki ni warongo katika yale waliyowaahidi Banū al Naḍī. info
التفاسير: