Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

external-link copy
182 : 2

فَمَنۡ خَافَ مِن مُّوصٖ جَنَفًا أَوۡ إِثۡمٗا فَأَصۡلَحَ بَيۡنَهُمۡ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Basi yoyote atakayejua kuwa mwenye kuusia amepinduka, kwa kuiacha haki katika wasia wake kwa njia ya kukosea au kukusudia, akamnasihi mtoaji wasia, wakati wa kutoa wasia, afanye uadilifu, na iwapo hilo halikuwa akaleta upatanishi kati ya pande zinazohusika kwa kugeuza wasia ili ulingane na Sheria, basi atakuwa hana dhambi katika kupatanisha huku. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kuwasamehe waja wake, ni Mwenye huruma kwao. info
التفاسير: