Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
8 : 17

عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يَرۡحَمَكُمۡۚ وَإِنۡ عُدتُّمۡ عُدۡنَاۚ وَجَعَلۡنَا جَهَنَّمَ لِلۡكَٰفِرِينَ حَصِيرًا

Inatarajiwa kuwa Mola wenu, enyi Wana wa Isrāīl, Atawarehemu baada ya kuwatesa, mkitubia na mkatengenea, na mkirudi kufanya uharibifu na maonevu, tutarudi kuwatesa na kuwadhili. Na tumeufanya moto wa Jahanamu, kwenu na kwa makafiri kwa jumla, ni gereza ambalo hakuna kutoka humo kabisa. Katika aya hii na ile kabla yake pana onyo kwa ummah huu dhidi ya kufanya maasia ili lisiwapate lile lililowapata Wana wa Isrāīl, basi mipango ya Mwenyezi Mungu ni mimoja, haina kubadilika wala kugeuka. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 17

إِنَّ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ يَهۡدِي لِلَّتِي هِيَ أَقۡوَمُ وَيُبَشِّرُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٱلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ أَنَّ لَهُمۡ أَجۡرٗا كَبِيرٗا

Hii Qur’ani tuliyoiteremsha kwa mja wetu Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, inawaongoza watu kwenye njia nzuri kabisa nayo ni mila ya Kiislamu, na inawapa bishara njema Waumini, wanaofanya yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewaamrisha kwayo na wanaokomeka na yale ambayo Amewakataza nayo, kwamba watakuwa na malipo makubwa, info
التفاسير:

external-link copy
10 : 17

وَأَنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ أَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا

na kwamba wale ambao hawaamini Nyumba ya Akhera na malipo yaliyoko huko, tumewatayarishia adhabu yenye kuumiza ndani ya Moto. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 17

وَيَدۡعُ ٱلۡإِنسَٰنُ بِٱلشَّرِّ دُعَآءَهُۥ بِٱلۡخَيۡرِۖ وَكَانَ ٱلۡإِنسَٰنُ عَجُولٗا

Na binadamu wakati mwingine hujiapiza mabaya nafsi yake au mtoto wake au mali yake awapo na hasira kama vile anavyoomba mema. Hii ni kwa sababu ya ujinga wa mwanadamu na pupa lake. Na miongoni mwa rehema ya Mwenyezi Mungu kwake ni kwamba Yeye Anayakubali maombi yake mema na sio mabaya na kwamba Yeye anajua kuwa yeye hakukusudia kutaka hilo. Hakika binadamu ana tabia ya kuwa na pupa sana. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 17

وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ ءَايَتَيۡنِۖ فَمَحَوۡنَآ ءَايَةَ ٱلَّيۡلِ وَجَعَلۡنَآ ءَايَةَ ٱلنَّهَارِ مُبۡصِرَةٗ لِّتَبۡتَغُواْ فَضۡلٗا مِّن رَّبِّكُمۡ وَلِتَعۡلَمُواْ عَدَدَ ٱلسِّنِينَ وَٱلۡحِسَابَۚ وَكُلَّ شَيۡءٖ فَصَّلۡنَٰهُ تَفۡصِيلٗا

Na tumefanya usiku na mchana kuwa ni alama mbili zenye kuonyesha upweke wetu na uweza wetu, tukaifuta alama ya usiku, nayo ni mwezi, na tukaifanya alama ya mchana, nayo ni jua, ni yenye mwangaza, ili binadamu apate kuona kwenye mwangaza wa mchana namna ya kupekesha mambo ya maisha yake na ili aingie kwenye utulivu na mapumziko wakati wa usiku, na ili watu wajue, kwa kupishana mchana na usiku, idadi ya miaka na hesabu ya miezi na siku, wakaweka juu ya hiyo mipango wanayoitaka ya maslahi yao. Na kila kitu tumekifafanua ufafanuzi wa kutosha. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 17

وَكُلَّ إِنسَٰنٍ أَلۡزَمۡنَٰهُ طَٰٓئِرَهُۥ فِي عُنُقِهِۦۖ وَنُخۡرِجُ لَهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ كِتَٰبٗا يَلۡقَىٰهُ مَنشُورًا

Na kila binadamu Mwenyezi Mungu Anayajaalia yale anayoyatenda, yawe mema au maovu, ni yenye kuwa na yeye wakati wote, hatahisabiwa kwa matendo ya mtu mwingine, wala mwingine hatahesabiwa kwa matendo yake yeye. Na Mwenyezi Mungu Atamtolea , Siku ya Kiyama, kitabu kilichoandikwa ndani yake yale aliyoyatenda; atakiona kimefunguliwa mbele yake. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 17

ٱقۡرَأۡ كِتَٰبَكَ كَفَىٰ بِنَفۡسِكَ ٱلۡيَوۡمَ عَلَيۡكَ حَسِيبٗا

Ataambiwa, «Soma kitabu cha matendo yako.» Hapo atasoma, hata kama hakuwa akijua kusoma ulimwenguni, «Leo nafsi yako itakutosheleza kuwa ni yenye kukuhesabia matendo yako, upate kujua malipo yake.» Huu ni miongoni mwa uadilifu na uchungaji haki mkubwa kabisa kwamba mja aambiwe, ‘jihesabu nafsi yako, kwani inatosha kuwa ni yenye kukuhesabu. ’ info
التفاسير:

external-link copy
15 : 17

مَّنِ ٱهۡتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهۡتَدِي لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيۡهَاۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰۗ وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبۡعَثَ رَسُولٗا

Mwenye kuongoka akafuata njia ya haki, basi malipo mema yake yatamrudia yeye peke yake; na mwenye kupotoka akafuata njia ya ubatilifu, basi mateso ya kufanya hivyo yatamrudia yeye peke yake; na hakuna nafsi yoyote iliyofanya dhambi itabeba makosa ya nafsi nyingine iliyofanya dhambi. Na Mwenyezi Mungu Hatamuadhibu yoyote isipokuwa baada ya kumsimamishia hoja kwa kutuma Mitume na kuteremsha Vitabu. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 17

وَإِذَآ أَرَدۡنَآ أَن نُّهۡلِكَ قَرۡيَةً أَمَرۡنَا مُتۡرَفِيهَا فَفَسَقُواْ فِيهَا فَحَقَّ عَلَيۡهَا ٱلۡقَوۡلُ فَدَمَّرۡنَٰهَا تَدۡمِيرٗا

Na tukitaka kuwaangamiza watu wa mji kwa udhalimu wao, tunawaamrisha wenye gogi wao wamtii Mwenyezi Mungu, wampwekeshe na wawaamini Mitume Wake, na wasokuwa wao wako nyuma yao kwa kuwafuata, wakaasi amri ya Mola wao na wakawakanusha Mitume Wake, hapo likapasa juu yao neno la adhabu ambalo hakuna namna ya kurudishwa, na tukawamaliza kwa maangamivu yaliyotimia. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 17

وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا مِنَ ٱلۡقُرُونِ مِنۢ بَعۡدِ نُوحٖۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ بِذُنُوبِ عِبَادِهِۦ خَبِيرَۢا بَصِيرٗا

Na ni wengi tuliowaangamiza miongoni mwa watu waliokanusha Mitume wao baada ya Nabii wa Mwenyezi Mungu, Nūḥ. Na inatosha kwamba Mola wako, ewe Mtume, ni Mjuzi wa matendo yote ya waja Wake, hakifichamani Kwake chochote chenye kufichamana. info
التفاسير: