Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Al-Fil

external-link copy
1 : 105

أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصۡحَٰبِ ٱلۡفِيلِ

Je hujui, ewe Mtume, namna Alivyowafanya Mola wako watu wa ndovu: Abraha Mhebeshi na jeshi lake ambalo alikuja nalo ili kuivunja Alkaba tukufu? info
التفاسير:

external-link copy
2 : 105

أَلَمۡ يَجۡعَلۡ كَيۡدَهُمۡ فِي تَضۡلِيلٖ

Kwani Hakuijaalia mipango yao mibaya waliyoifanya ni yenye kuvunjika na kupita patupu? info
التفاسير:

external-link copy
3 : 105

وَأَرۡسَلَ عَلَيۡهِمۡ طَيۡرًا أَبَابِيلَ

Na Aliwapelekea makundi yaliyofuatana, info
التفاسير:

external-link copy
4 : 105

تَرۡمِيهِم بِحِجَارَةٖ مِّن سِجِّيلٖ

ya ndege waliokuwa wakiwatupia wao vijiwe vya udongo mkavu mgumu. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 105

فَجَعَلَهُمۡ كَعَصۡفٖ مَّأۡكُولِۭ

Akawapondaponda, wakawa ni kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama na halafu kutupwa. info
التفاسير: