Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Yunus

external-link copy
1 : 10

الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡحَكِيمِ

(Alif, Lām, Rā’.) Yametangulia maelezo juu ya herufi zilizotajwa kimkato mwanzo wa sura ya Al- Baqarah. Hizi ni aya za Kitabu kilichopangwa vizuri ambacho Mwenyezi Mungu Amekipanga na kukifafanua kwa waja Wake. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 10

أَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنۡ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ رَجُلٖ مِّنۡهُمۡ أَنۡ أَنذِرِ ٱلنَّاسَ وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَنَّ لَهُمۡ قَدَمَ صِدۡقٍ عِندَ رَبِّهِمۡۗ قَالَ ٱلۡكَٰفِرُونَ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٞ مُّبِينٌ

Je, lilikuwa jambo la ajabu kwa watu lile la kuteremsha kwetu wahyi wa Qur’ani kwa mtu miongoni mwao anayewaonya mateso ya Mwenyezi Mungu na kuwapa habari njema wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake kwamba wao watapata malipo mazuri kwa matendo mema waliyoyatanguliza? Alipowajia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa wahyi wa Mwenyezi Mungu na akawasomea, wakanushaji walisema, «Muhammad ni mchawi, na aliyokuja nayo ni uchawi wenye ubatilifu waziwazi.» info
التفاسير:

external-link copy
3 : 10

إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ إِذۡنِهِۦۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡ فَٱعۡبُدُوهُۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Hakika Mola wenu ni Mwenyezi Mungu Ambaye Alizipatisha mbingu na ardhi katika kipindi cha Siku Sita, kisha Akalingana, yaani Akawa juu ya 'Arsh, mlingano unaonasibiana na utisho Wake na utukufu Wake. Anaendesha mambo ya viumbe Vyake. Hakuna yoyote Anayempinga katika uamuzi Wake na hakuna muombezi yoyote anayeombea mbele Yake Siku ya Kiyama isipokuwa baada ya Yeye kumpa idhini kuombea. Basi muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wenu, Anayesifika kwa sifa hizi na mtakasiyeni ibada. Je, hamwaidhiki na mkazizingatia aya hizi na hoja? info
التفاسير:

external-link copy
4 : 10

إِلَيۡهِ مَرۡجِعُكُمۡ جَمِيعٗاۖ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقًّاۚ إِنَّهُۥ يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ لِيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ بِٱلۡقِسۡطِۚ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَهُمۡ شَرَابٞ مِّنۡ حَمِيمٖ وَعَذَابٌ أَلِيمُۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡفُرُونَ

Kwa Mola wenu ndio marejeo yenu nyote Siku ya Kiyama. Na hili ndilo agizo la Mwenyezi Mungu lililo kweli. Yeye Ndiye Ambaye Anaanza kuumba viumbe kisha Atawarudisha baada ya kufa, Awafanye wawe hai kama walivyokuwa mwanzo, ili Awalipe waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na akafanya matendo mazuri malipo mazuri zaidi kwa uadilifu. Na wale waliokanusha upweke wa Mwenyezi Mungu na ujumbe wa Mtume Wake watakuwa na vinywaji vya maji moto sana yanayochoma nyuso na kukata tumbo; na watakuwa na adhabu inayoumiza kwa sababu ya ukafiri wao na upotevu wao. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 10

هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ ٱلشَّمۡسَ ضِيَآءٗ وَٱلۡقَمَرَ نُورٗا وَقَدَّرَهُۥ مَنَازِلَ لِتَعۡلَمُواْ عَدَدَ ٱلسِّنِينَ وَٱلۡحِسَابَۚ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۚ يُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Mwenyezi Mungu Ndiye ambaye Alilifanya jua kuwa d,iyā’ (mwangaza), Akaufanya mwezi kuwa ni nūr (mng’aro) na Akaupangia mwezi njia zake za kupita. Ikawa kwa jua zinajulikana siku, na kwa mwezi inajulikana miezi na miaka. Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Hakuumba jua na mwezi isipokuwa ni hekima kubwa, na kuonesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu na ujuzi Wake; Anafafanua hoja na dalili kwa watu wanaojua hekima ya utengenezaji wa uumbaji. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 10

إِنَّ فِي ٱخۡتِلَٰفِ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ ٱللَّهُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَتَّقُونَ

Hakika katika kupishana usiku na mchana na Alichokiumba Mwenyezi Mungu, katika mbingu na ardhi na zilizomo ndani yake zilizopangika na kutengenezeka miongoni mwa maajabu ya uumbaji, ni dalili na hoja zilizo wazi kwa watu wanaoogopa mateso ya Mwenyezi Mungu, ghadhabu Zake na adhabu Yake. info
التفاسير: