Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Abdallah Mohamed na Nassor Khamis

numero y'urupapuro:close

external-link copy
31 : 12

فَلَمَّا سَمِعَتۡ بِمَكۡرِهِنَّ أَرۡسَلَتۡ إِلَيۡهِنَّ وَأَعۡتَدَتۡ لَهُنَّ مُتَّكَـٔٗا وَءَاتَتۡ كُلَّ وَٰحِدَةٖ مِّنۡهُنَّ سِكِّينٗا وَقَالَتِ ٱخۡرُجۡ عَلَيۡهِنَّۖ فَلَمَّا رَأَيۡنَهُۥٓ أَكۡبَرۡنَهُۥ وَقَطَّعۡنَ أَيۡدِيَهُنَّ وَقُلۡنَ حَٰشَ لِلَّهِ مَا هَٰذَا بَشَرًا إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا مَلَكٞ كَرِيمٞ

Aliposikia mke wa Kiongozi kusengenya kwao na hila zao za kumtukana yeye, aliwatumia ujumbe na kuwaita kuja kumtembelea, na akatayarisha mito ya kutegemea na chakula cha kula, na akampa kila mmoja miongoni mwao kisu cha kukatia chakula kisha akasema kumwambia Yūsuf, «Jitokeze kwao.» Walipomshuhudia, walimuona ni kitu kikubwa chenye haiba, na wakashikwa na babaiko la uzuri wake na kuvutia kwake, wakajikata mikono yao katika hali ya kukata chakula kwa babaiko kuu na mshangao, na wakasema kwa kustaajabu, «Twajilinda na Mwenyezi Mungu! Huyu si binadamu!» kwa kuwa uzuri wake sio ule ujulikanao kwa wanadamu, «Huyu si mwingine isipokuwa ni mtukufu miongoni mwa Malaika.» info
التفاسير:

external-link copy
32 : 12

قَالَتۡ فَذَٰلِكُنَّ ٱلَّذِي لُمۡتُنَّنِي فِيهِۖ وَلَقَدۡ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفۡسِهِۦ فَٱسۡتَعۡصَمَۖ وَلَئِن لَّمۡ يَفۡعَلۡ مَآ ءَامُرُهُۥ لَيُسۡجَنَنَّ وَلَيَكُونٗا مِّنَ ٱلصَّٰغِرِينَ

Mke wa kiongozi alisema kuwaambia wanawake waliojikata mikono yao, «Haya ndiyo yaliyowapata kwa kumuona yeye. Aliyefanya mpatikane na haya ni huyu kijana ambaye nyinyi mumenilaumu kusalitika naye. Kwa kweli nilimtaka na nikajaribu kumvutia ili anikubalie, akajizuia na akakataa. Na asipofanya ninachomuamuru mbeleni, atateswa kwa kutiwa jela na hapo atakuwa ni miongoni mwa wanyonge. info
التفاسير:

external-link copy
33 : 12

قَالَ رَبِّ ٱلسِّجۡنُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا يَدۡعُونَنِيٓ إِلَيۡهِۖ وَإِلَّا تَصۡرِفۡ عَنِّي كَيۡدَهُنَّ أَصۡبُ إِلَيۡهِنَّ وَأَكُن مِّنَ ٱلۡجَٰهِلِينَ

Yūsuf akasema, akijilinda na shari lao na vitimbi vyao, «Ewe Mola wangu! Jela ni bora kwangu kuliko yale wanayoniitia ya kufanya machafu. Na usiponiepulia vitimbi vyao, nitalemea kwao na nitakuwa ni miongoni mwa wachache wa akili wenye kujifanyia madhambi kwa ujinga wao. info
التفاسير:

external-link copy
34 : 12

فَٱسۡتَجَابَ لَهُۥ رَبُّهُۥ فَصَرَفَ عَنۡهُ كَيۡدَهُنَّۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Mwenyezi Mungu Akamkubalia Yūsuf maombi yake, akamwepushia kile alichotaka mke wa Kiongozi na marafiki zake kutoka kwake cha kumuasi Mwenyezi Mungu. Mwenyezi mungu Ndiye Mwenye kuyasikia maombi ya Yūsuf na maombi ya kila mwenye kuomba kati ya waja Wake, Ndiye Mwenye kuyajua matakwa yake, haja zake na kile kinachomfaa, na pia haja za viumbe Vyake vyote na yale yanayowafaa. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 12

ثُمَّ بَدَا لَهُم مِّنۢ بَعۡدِ مَا رَأَوُاْ ٱلۡأٓيَٰتِ لَيَسۡجُنُنَّهُۥ حَتَّىٰ حِينٖ

Kisha ikamdhihirikia waziri na marafiki zake, baada ya kuziona dalili za kuwa Yūsuf hana hatia na amejiepusha na machafu, wamfunge mpaka muda fulani, mrefu au mfupi, ili kuzuia fedheha. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 12

وَدَخَلَ مَعَهُ ٱلسِّجۡنَ فَتَيَانِۖ قَالَ أَحَدُهُمَآ إِنِّيٓ أَرَىٰنِيٓ أَعۡصِرُ خَمۡرٗاۖ وَقَالَ ٱلۡأٓخَرُ إِنِّيٓ أَرَىٰنِيٓ أَحۡمِلُ فَوۡقَ رَأۡسِي خُبۡزٗا تَأۡكُلُ ٱلطَّيۡرُ مِنۡهُۖ نَبِّئۡنَا بِتَأۡوِيلِهِۦٓۖ إِنَّا نَرَىٰكَ مِنَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Wakaingia jela pamoja na yeye vijana wawili. Mmoja wao akasema, «Mimi nimeota usingizini kwamba mimi nakamua zabibu ili ziwe pombe.» Na mwingine alisema, «Mimi nimeota kwamba nabeba mkate juu ya kichwa changu na ndege wanaula. Wakasema, «Tupe habari, ewe Yūsuf, uaguzi wa ndoto tulizoziota. Sisi tunakuona wewe ni miongoni mwa wale wanaofanya wema katika kuabudu kwao Mwenyezi Mungu na kuingiliana kwao na viumbe Wake.» info
التفاسير:

external-link copy
37 : 12

قَالَ لَا يَأۡتِيكُمَا طَعَامٞ تُرۡزَقَانِهِۦٓ إِلَّا نَبَّأۡتُكُمَا بِتَأۡوِيلِهِۦ قَبۡلَ أَن يَأۡتِيَكُمَاۚ ذَٰلِكُمَا مِمَّا عَلَّمَنِي رَبِّيٓۚ إِنِّي تَرَكۡتُ مِلَّةَ قَوۡمٖ لَّا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ كَٰفِرُونَ

Yūsuf aliwaambia, «Hamtajiwa na riziki ya chakula kwa namna yoyote ile, isipokuwa mimi nitawapa tafsiri yake kabla ya kuwajia. Tafsiri hiyo nitakayowapa nyinyi wawili ni miongoni mwa yale niliyofundishwa na Mola wangu. Mimi nimemuamini na nimemtakasia ibada na nimejiepusha na dini ya wasiomuamini Mwenyezi Mungu wala kuamini kufufuliwa na kuhesabiwa. info
التفاسير: