Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Abdallah Mohamed na Nassor Khamis

Yusuf

external-link copy
1 : 12

الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ

Alif, Lām, Rā’. Maneno yametangulia juu ya herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqrah. Hizi ni aya za Kitabu kilichobainika kilicho wazi katika maana yake, mahalalisho yake, maharamisho yake na uongofu wake. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 12

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ قُرۡءَٰنًا عَرَبِيّٗا لَّعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Sisi tumekuteremshia Qur’ani kwa lugha ya Waarabu, huenda nyinyi, enyi Waarabu mkayatia akilini maana yake, mkayafahamu na mkatenda kulingana na uongofu wake. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 12

نَحۡنُ نَقُصُّ عَلَيۡكَ أَحۡسَنَ ٱلۡقَصَصِ بِمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ وَإِن كُنتَ مِن قَبۡلِهِۦ لَمِنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ

Sisi tunakusimulia wewe, ewe Mtume, visa vizuri zaidi kwa wahyi tuliyokuletea wa hii Qur’ani, na ingawa, kabla ya kukuteremshia, ulikuwa ni miongoni mwa walioghafilika nazo, hujui chochote kuhusu habari hizi. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 12

إِذۡ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَٰٓأَبَتِ إِنِّي رَأَيۡتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوۡكَبٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ رَأَيۡتُهُمۡ لِي سَٰجِدِينَ

Kumbuka, ewe Mtume, kuwaambia watu wako neno la Yūsuf kumwambia babake, «Mimi nimeota usingizini kuona nyota kumi na moja, jua na mwezi, zote zikinisujudia.» Ndoto hii ilikuwa ni bishara ya cheo kikubwa, cha ulimwenguni na Akhera, alichofikia Yūsuf, amani imshukiye. info
التفاسير: