Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução em Swahili - Áli Muhsin

Ash-Shura

external-link copy
1 : 42

حمٓ

H'a Mim . info

H'a Mim, A'yn Sin Qaf: Sura imeanzia kwa harufi hizi za kutamkwa kama ilivyo ada katika Sura nyingi katika Qur'ani.

التفاسير:

external-link copy
2 : 42

عٓسٓقٓ

A'yn Sin Qaf . info

H'a Mim, A'yn Sin Qaf: Sura imeanzia kwa harufi hizi za kutamkwa kama ilivyo ada katika Sura nyingi katika Qur'ani.

التفاسير:

external-link copy
3 : 42

كَذَٰلِكَ يُوحِيٓ إِلَيۡكَ وَإِلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكَ ٱللَّهُ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mwenye hikima anavyo kuletea Wahyi wewe na walio kabla yako. info

Mfano wa yaliyomo katika Sura hii anakufunulia wewe na Mitume walio kuwa kabla yako, Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda kwa nguvu zake, ambaye amepanga kila kitu kwa pahala pake, kwa mujibu wa hikima katika vitendo vyake na mipango yake.

التفاسير:

external-link copy
4 : 42

لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَلِيُّ ٱلۡعَظِيمُ

Ni vyake viliomo mbinguni, na viliomo katika ardhi. Na Yeye ndiye Mtukufu, Mkuu. info

Ni vya Mwenyezi Mungu, peke yake, vyote viliomo katika mbingu na ardhi, kwa kuviumba, kuvimilika, na kuviendesha. Naye ni peke yake aliye tukuka kwa nafsi, na ukawa mkuu ufalme wake.

التفاسير:

external-link copy
5 : 42

تَكَادُ ٱلسَّمَٰوَٰتُ يَتَفَطَّرۡنَ مِن فَوۡقِهِنَّۚ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمۡدِ رَبِّهِمۡ وَيَسۡتَغۡفِرُونَ لِمَن فِي ٱلۡأَرۡضِۗ أَلَآ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Zinakaribia mbingu kupasuka juu huko, na Malaika wakimtakasa Mola wao Mlezi na kumhimidi, na wakiwaombea maghfira waliomo kwenye ardhi. Ama hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. info

Mbingu, juu ya ukubwa wake na kushikamana kwake, zimekaribia kupasuka kutoka huko juu kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu, na kuathirika kwa taadhima yake na utukufu wake. Na Malaika wanamtakasa Mwenyezi Mungu na kila lisilo elekea naye, na humsifu kwa analo stahiki. Na humwomba Mwenyezi Mungu awasamehe watu wa duniani. Na Yeye Subhanahu ananabihisha kwamba hakika ni Mwenyezi Mungu tu, peke yake, ndiye Mwenye maghfira ya wote, na rehema iliyo kunjufu.

التفاسير:

external-link copy
6 : 42

وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَ ٱللَّهُ حَفِيظٌ عَلَيۡهِمۡ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡهِم بِوَكِيلٖ

Na wale walio wafanya walinzi wengine badala yake Yeye, Mwenyezi Mungu ni Mwangalizi juu yao. Wala wewe si wakili juu yao. info

Na hao walio wafanya wengineo badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ndio wa kuwanusuru, Mwenyezi Mungu anaangalia hayo wayatendayo. Wala wewe hukupewa kazi hiyo ya kuwaangalia wao.

التفاسير:

external-link copy
7 : 42

وَكَذَٰلِكَ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ قُرۡءَانًا عَرَبِيّٗا لِّتُنذِرَ أُمَّ ٱلۡقُرَىٰ وَمَنۡ حَوۡلَهَا وَتُنذِرَ يَوۡمَ ٱلۡجَمۡعِ لَا رَيۡبَ فِيهِۚ فَرِيقٞ فِي ٱلۡجَنَّةِ وَفَرِيقٞ فِي ٱلسَّعِيرِ

Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na uhadharishe na Siku ya Mkutano, haina shaka hiyo. Kundi moja litakuwa Peponi, na kundi jengine Motoni. info

Na mfano wa ufunuo huo ulio wazi, tumekufunulia wewe hii Qur'ani kwa lugha ya Kiarabu isiyo na ubabaishi, ili upate kuwaonya watu wa Makka na walio pembezoni mwake katika Waarabu, na uwaonye watu adhabu ya siku watakao kusanywa khalaiki wote kwa ajili ya hisabu. Hapana shaka yoyote kuja siku hiyo. Watu siku hiyo watakuwa mafungu mawili - fungu moja litakuwa Peponi. ma kundi jengine litakuwa Motoni.

التفاسير:

external-link copy
8 : 42

وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَهُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن يُدۡخِلُ مَن يَشَآءُ فِي رَحۡمَتِهِۦۚ وَٱلظَّٰلِمُونَ مَا لَهُم مِّن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ

Na Mwenyezi Mungu angeli penda ange wafanya wote umma mmoja, lakini anamwingiza katika rehema yake amtakaye. Na wenye kudhulumu hawana mlinzi wala msaidizi. info

Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli penda kuwakusanya watu wote katika dunia wakafuata njia moja angeli wakusanya hivyo. Lakini Yeye humtia katika rehema yake amtakaye, kwa kuwa anajua kuwa hao wamekhiari uwongofu kuliko upotofu. Na wenye kujidhulumu nafsi zao kwa ukafiri hawana mlinzi badala ya Mwenyezi Mungu wa kudhamini kuwalinda, wala msaidizi wa kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
9 : 42

أَمِ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَۖ فَٱللَّهُ هُوَ ٱلۡوَلِيُّ وَهُوَ يُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Au wamechukua walinzi wengine badala yake! Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi khasa. Na Yeye ndiye anaye huisha wafu. Na Yeye ndiye Mweza wa kila kitu. info

Hawa wenye kudhulumu hawakumfanya Mwenyezi Mungu kuwa ni mlinzi wao, bali wamewafanya wengineo kuwa ndio walinzi wao. Na wala haiwafalii wao hayo. Kwani Mwenyezi Mungu, peke yake, ndiye Mwenye kustahiki kuwa Mlinzi kama wao wanataka mlinzi. Yeye ndiye anaye fufua walio kufa kwa ajili ya hisabu. Na Yeye ndiye Mwenye madaraka juu ya kila kitu kwa uweza wake.

التفاسير:

external-link copy
10 : 42

وَمَا ٱخۡتَلَفۡتُمۡ فِيهِ مِن شَيۡءٖ فَحُكۡمُهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبِّي عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ أُنِيبُ

Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi, ninaye mtegemea na kwake Yeye narejea. info

Na mliyo khitalifiana kwayo katika mambo yaliyo khusu Imani na ukafiri, hukumu yake ya kukata iko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye amekwisha ibainisha. Yeye huyo ndiye Hakimu wa kuhukumu mliyo khitalifiana, Mwenyezi Mungu, Mwenye kumiliki mambo yangu yote. Mimi namtegemea Yeye kwa mambo yangu. Na kwake Yeye peke yake ndio narejea ili kutafuta uwongozi.

التفاسير: