Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução Suaíli - Abdullah Muhammad e Nasser Khamis

Número de página:close

external-link copy
11 : 70

يُبَصَّرُونَهُمۡۚ يَوَدُّ ٱلۡمُجۡرِمُ لَوۡ يَفۡتَدِي مِنۡ عَذَابِ يَوۡمِئِذِۭ بِبَنِيهِ

Watawaona na watawajua, na hakuna yoyote atakayeweza kumnufaisha yoyote. Kafiri atatamani lau ajikomboa nafsi yake na adhabu ya Siku ya Kiyama kwa watoto wake, info
التفاسير:

external-link copy
12 : 70

وَصَٰحِبَتِهِۦ وَأَخِيهِ

mkewe, nduguye, info
التفاسير:

external-link copy
13 : 70

وَفَصِيلَتِهِ ٱلَّتِي تُـٔۡوِيهِ

jamaa zake wanaomuhami na ambao anajinasibisha nao kwa ujamaa info
التفاسير:

external-link copy
14 : 70

وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا ثُمَّ يُنجِيهِ

na kwa wote walio kwenye ardhi miongoni mwa binadamu na wengineo ili aokoke na adhabu ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 70

كَلَّآۖ إِنَّهَا لَظَىٰ

Mambo siyo kama vile unavyotamani yawe, ewe kafiri, ya kujikomboa. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 70

نَزَّاعَةٗ لِّلشَّوَىٰ

Huo ni moto wa Jahanamu, moto wake unawaka na kuroroma, joto lake linatoa kwa nguvu ngozi ya kichwa na sehemu nyingine za mwili, info
التفاسير:

external-link copy
17 : 70

تَدۡعُواْ مَنۡ أَدۡبَرَ وَتَوَلَّىٰ

unamwita aliyeipa mgongo haki duniani na akaacha kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, info
التفاسير:

external-link copy
18 : 70

وَجَمَعَ فَأَوۡعَىٰٓ

na akakusanya mali na kuyaweka kwenye mahazina yake na asitekeleze amri ya Mwenyezi Mungu kwenye mali hayo. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 70

۞ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ خُلِقَ هَلُوعًا

Hakika binadamu ameumbwa akiwa na tabia ya babaiko na pupa. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 70

إِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ جَزُوعٗا

Yakimpata makero na shida, anababaika sana na kufa moyo. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 70

وَإِذَا مَسَّهُ ٱلۡخَيۡرُ مَنُوعًا

Na yakimpata mambo mazuri na ukunjufu wa maisha, huwa ni mwingi wa kuzuia na. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 70

إِلَّا ٱلۡمُصَلِّينَ

Isipokuwa wenye kusimamisha Swala, info
التفاسير:

external-link copy
23 : 70

ٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ دَآئِمُونَ

wanaochunga kuitekeleza katika nyakati zake zote, hakuna shughuli yoyote inayowashughulisha nayo. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 70

وَٱلَّذِينَ فِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ مَّعۡلُومٞ

Na wale ambao katika mali yao kuna fungu maalumu alililowafaradhia Mwenyezi Mungu, nalo ni Zaka info
التفاسير:

external-link copy
25 : 70

لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ

wanaozitoa kwa anayeomba msaada na kwa na kwa asiyeomba. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 70

وَٱلَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ

Na wale ambao wanaiamini Siku ya kuhesabiwa na kulipwa wakajiandaa nayo kwa matendo mema. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 70

وَٱلَّذِينَ هُم مِّنۡ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشۡفِقُونَ

Na wale ambao wao wanaiogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu, info
التفاسير:

external-link copy
28 : 70

إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمۡ غَيۡرُ مَأۡمُونٖ

kwani adhabu ya Mola wao haipaswi kwa yoyote kujiaminisha nayo. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 70

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِفُرُوجِهِمۡ حَٰفِظُونَ

Na wale ambao wao ni wenye kutunza tupu zao na kila alichokiharamishia Mwenyezi Mungu, info
التفاسير:

external-link copy
30 : 70

إِلَّا عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِهِمۡ أَوۡ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَإِنَّهُمۡ غَيۡرُ مَلُومِينَ

isipokuwa wake zao na vijakazi vyao, hakika wao kwa hao hawapatilizwi. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 70

فَمَنِ ٱبۡتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡعَادُونَ

Basi mwenye kutaka kumaliza matamanio yake ya kimwili kwa wasiokuwa wake zake au vijakazi vyake, basi hao ndio wenye kukiuka mipaka ya halali kuingia kwenye haramu. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 70

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِأَمَٰنَٰتِهِمۡ وَعَهۡدِهِمۡ رَٰعُونَ

Na wale ambao wanazitunza amana za Mwenyezi Mungu na amana za waja, na wanatunza ahadi zao pamoja na Mwenyezi Munmgu, Aliyetukuka, na pamoja na waja. info
التفاسير:

external-link copy
33 : 70

وَٱلَّذِينَ هُم بِشَهَٰدَٰتِهِمۡ قَآئِمُونَ

Na wale ambao wanatekeleza ushahidi wao kwa ukweli bila kubadilisha au kuficha. info
التفاسير:

external-link copy
34 : 70

وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ

Na wale ambao wanatunza utekelezaji Swala wala hawaharibu chochote cha wajibu katika hiyo Swala. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 70

أُوْلَٰٓئِكَ فِي جَنَّٰتٖ مُّكۡرَمُونَ

Hao waliosifika kwa sifa hizo njema, ni wenye kutulia kwenye mabustani ya Pepo ya starehe, ni wenye kukirimiwa humo kwa kila aina ya takrima. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 70

فَمَالِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ قِبَلَكَ مُهۡطِعِينَ

Ni msukumo gani unaowasukuma makafiri watembee kwa haraka kuelekea upande wako, ewe Mtume, na huku wamenyosha shingo zao kwako, wamekukabili kwa macho yao, info
التفاسير:

external-link copy
37 : 70

عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ عِزِينَ

wanajikusanya kuliani kwako na kushotoni kwako, wakiwa wamekaa kwa kupiga maduara na wamejigawa vikundi mbalimbali, wanazungumza na kuona ajabu? info
التفاسير:

external-link copy
38 : 70

أَيَطۡمَعُ كُلُّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ أَن يُدۡخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٖ

Je ana tamaa kila mmoja miongoni mwa makafiri kuwa Mwenyezi Mungui Atamuingiza kwenye Pepo ya starehe ya daima? Mambo siyo kama vile wanavyotazamia. Wao hawataiingia hiyo Pepo kabisa. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 70

كَلَّآۖ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّمَّا يَعۡلَمُونَ

Hakika sisi tumewaumba kwa kile wanachokijua cha maji matwevu kama wengineo, na vilevile hawakuamini. Basi vipi watapata heshima ya kuingia Pepo ya sterehe? info
التفاسير:

external-link copy
40 : 70

فَلَآ أُقۡسِمُ بِرَبِّ ٱلۡمَشَٰرِقِ وَٱلۡمَغَٰرِبِ إِنَّا لَقَٰدِرُونَ

Sivyo hivyo. Najiapia Mimi Mwenyewe niliye Mola wa pande za kuchomoza na kutua jua, mwezi na sayari nyinginezo, kwa yanayopatikana humo miongoni mwa dalili waziwazi za kujulisha kufufuliwa, info
التفاسير: