Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução Suaíli - Abdullah Muhammad e Nasser Khamis

Al-Ma'arij

external-link copy
1 : 70

سَأَلَ سَآئِلُۢ بِعَذَابٖ وَاقِعٖ

Ameapiza mwenye kuapiza miongoni mwa washirikina, kujiapiza mwenyewe na kuwaapiza watu wake kuteremkiwa na adhabu, info
التفاسير:

external-link copy
2 : 70

لِّلۡكَٰفِرِينَ لَيۡسَ لَهُۥ دَافِعٞ

nayo ni yenye kuwashukia bila shaka Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 70

مِّنَ ٱللَّهِ ذِي ٱلۡمَعَارِجِ

Hakuna mzuiaji yoyote wa kuizuia isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mwenye utukufu na haiba. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 70

تَعۡرُجُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيۡهِ فِي يَوۡمٖ كَانَ مِقۡدَارُهُۥ خَمۡسِينَ أَلۡفَ سَنَةٖ

Malaika na Jibrili wanapanda kuenda Kwake, Aliyetukuka, kwa siku moja ambayo kadiri yake ni myaka elfu hamsini katika myaka ya duniani, nayo kwa aliyeamini ni kama muda wa Swala moja ya faradhi. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 70

فَٱصۡبِرۡ صَبۡرٗا جَمِيلًا

Basi vumilia, ewe Mtume, kule kufanya kwao shere na kutaka kwao wafikiwe na adhabu kwa haraka, uvumilivu usiokuwa na babaiko wala kumshtakia asiyekuwa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 70

إِنَّهُمۡ يَرَوۡنَهُۥ بَعِيدٗا

Kwa kweli makafiri wanaiona adhabu kuwa iko mbali na wanaona kuwa si yenye kutukia. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 70

وَنَرَىٰهُ قَرِيبٗا

Na sisi tunaiona ni yenye kutukia kwa kipindi cha karibu bila shaka. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 70

يَوۡمَ تَكُونُ ٱلسَّمَآءُ كَٱلۡمُهۡلِ

Siku ambayo mbingu itayayuka iwe ni kama rojo la mafuta, info
التفاسير:

external-link copy
9 : 70

وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ

na majabali yawe ni kama sufi iliyochanganywa na iliyoshanuliwa na kupeperushwa na upepo. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 70

وَلَا يَسۡـَٔلُ حَمِيمٌ حَمِيمٗا

Wala mtu hatamuuliza jamaa yake wa karibu kuhusu jambo lake, kwani kila mmoja ameshughulishwa na nafsi yake. info
التفاسير: