Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução Suaíli - Abdullah Muhammad e Nasser Khamis

Número de página:close

external-link copy
231 : 2

وَإِذَا طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَبَلَغۡنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمۡسِكُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٍ أَوۡ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٖۚ وَلَا تُمۡسِكُوهُنَّ ضِرَارٗا لِّتَعۡتَدُواْۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ فَقَدۡ ظَلَمَ نَفۡسَهُۥۚ وَلَا تَتَّخِذُوٓاْ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ هُزُوٗاۚ وَٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَمَآ أَنزَلَ عَلَيۡكُم مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَٱلۡحِكۡمَةِ يَعِظُكُم بِهِۦۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ

Pindi mtakapowataliki wanawake wakakaribia siku za kumaliza eda lao, basi warejeeni hali ya kuwa nia zenu ni kuwatekelezea haki zao kwa njia nzuri, kisheria na kidesturi, au waacheni mpaka eda lao limalizike. Na kueni na hadhari, isije ikawa kuwarejea ni kwa lengo la kuwadhuru kwa kuwafanyia uadui katika haki zao. Na yoyote atakayelifanya hilo, ameshaidhulumu nafsi yake kwa kustahiki mateso. Na wala msizifanye aya za Mwenyezi Mungu na hukumu Zake kuwa ni mchezo na upuzi. Nakumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu kwenu, kwa kuwafanya Waislamu na kuwafafanulia hukumu Zake. Na yakumbukeni yale Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, ya Qur’ani na mafundisho ya Mtume Wake. Na mshukuruni Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa neema hizi zilzo kubwa. Mwenyezi Mungu Anawakumbusha hayo na Anawatisha msende kinyume nayo. Basi, mcheni Mwenyezi Mungu na mumlindize. Na mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu, hapana kitu chenye kufichika Kwake, na Atamlipa kila mmoja kwa anayostahiki alipwe. info
التفاسير:

external-link copy
232 : 2

وَإِذَا طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَبَلَغۡنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعۡضُلُوهُنَّ أَن يَنكِحۡنَ أَزۡوَٰجَهُنَّ إِذَا تَرَٰضَوۡاْ بَيۡنَهُم بِٱلۡمَعۡرُوفِۗ ذَٰلِكَ يُوعَظُ بِهِۦ مَن كَانَ مِنكُمۡ يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۗ ذَٰلِكُمۡ أَزۡكَىٰ لَكُمۡ وَأَطۡهَرُۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ

Na mtakapowaacha wake zenu chini ya talaka tatu na eda lao likaisha bila nyinyi kuwarejea, basi msiwadhiki, enyi mawalii, hao walioachwa kwa kuwazuia kurudi kwa waume zao, kwa kufunga ndoa upya, wakiwa wenyewe wametaka hilo na yakapatikana maridhiano kisheria na kidesturi. Hilo aidhiwa kwalo aiyekuwa, miongoni mwenu, ni mkweli kwenye imani yake kwa Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hakika kuacha kuwazuia na kuwawezesha waume kuwaoa waliokuwa wake zao, ni jambo lenye kukuza zaidi na kutakasa zaidi heshima zenu, na ni lenye nafuu kubwa zaidi na thawabu nyingi zaidi kwenu. Na Mwenyezi Mungu Anayajua yenye maslahi kwenu; na nyinyi hamjui hilo. info
التفاسير:

external-link copy
233 : 2

۞ وَٱلۡوَٰلِدَٰتُ يُرۡضِعۡنَ أَوۡلَٰدَهُنَّ حَوۡلَيۡنِ كَامِلَيۡنِۖ لِمَنۡ أَرَادَ أَن يُتِمَّ ٱلرَّضَاعَةَۚ وَعَلَى ٱلۡمَوۡلُودِ لَهُۥ رِزۡقُهُنَّ وَكِسۡوَتُهُنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ لَا تُكَلَّفُ نَفۡسٌ إِلَّا وُسۡعَهَاۚ لَا تُضَآرَّ وَٰلِدَةُۢ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوۡلُودٞ لَّهُۥ بِوَلَدِهِۦۚ وَعَلَى ٱلۡوَارِثِ مِثۡلُ ذَٰلِكَۗ فَإِنۡ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٖ مِّنۡهُمَا وَتَشَاوُرٖ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِمَاۗ وَإِنۡ أَرَدتُّمۡ أَن تَسۡتَرۡضِعُوٓاْ أَوۡلَٰدَكُمۡ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ إِذَا سَلَّمۡتُم مَّآ ءَاتَيۡتُم بِٱلۡمَعۡرُوفِۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Na ni juu ya wanawake waliozaa kuwanyonyesha watoto wao muda wa miaka miwili kamili, kwa yule atakaye kukamilisha unyonyeshaji. Na ni wajibu kwa mababa kuwadhamini wanyonyeshaji, waliopewa talaka, kwa chakula chao na mavazi yao kwa njia ipendekezayo kisheria na kimila. Kwani Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu ela kiasi cha uwezo wake. Na haifai kwa wazazi wawili kumfanya mototo aliyezaliwa kuwa ni njia ya kudhuriana kati yao. Na inamlazimu mrithi, mzazi anapokufa, kile kinachomlazimu mzazi, kabla hajafa, cha matumizi na mavazi. Na wazazi wanapotaka kumuachisha mtoto kunyonya, kabla kukamilisha miaka miwili, basi si makosa kwao iwapo wameridhiana na kushawiriana kwa hilo na kufikia kwenye uamuzi wenye maslahi ya mtoto. Na iwapo wazazi wawili wamekubaliana kumpa mtoto mnyonyeshaji mwengine asiyekuwa mamake ili amnyonyeshe, pia si makosa kwao., iwapo baba atampa mama haki yake, na pia atampa mwenye kunyonyesha haki kwa mujibu wa desturi zinazoeleweka kwa watu. Na muogopeni Mwenyezi Mungu katika hali zenu zote. Na mjue kwamba Mwenyezi Mungu kwa mnayoyafanya ni muoni na Atawalipa kwayo. info
التفاسير: