Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução Suaíli - Abdullah Muhammad e Nasser Khamis

Número de página:close

external-link copy
154 : 2

وَلَا تَقُولُواْ لِمَن يُقۡتَلُ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمۡوَٰتُۢۚ بَلۡ أَحۡيَآءٞ وَلَٰكِن لَّا تَشۡعُرُونَ

Na wala msiseme, enyi Waumini, kuhusu wale wanaouawa hali ya kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kuwa wao wamekufa. Bali wao wako hai, uhai maalumu unaowahusu wao, ndani ya Makaburi yao. Wala hakuna anayejua yako vipi maisha hayo isipokuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, lakini nyinyi hamuyahisi maisha hayo. Katika haya, pana ushahidi kwamba kuna neema za kaburini. info
التفاسير:

external-link copy
155 : 2

وَلَنَبۡلُوَنَّكُم بِشَيۡءٖ مِّنَ ٱلۡخَوۡفِ وَٱلۡجُوعِ وَنَقۡصٖ مِّنَ ٱلۡأَمۡوَٰلِ وَٱلۡأَنفُسِ وَٱلثَّمَرَٰتِۗ وَبَشِّرِ ٱلصَّٰبِرِينَ

Tutawapa, tena tutawapa, mtihani wa kitu hafifu cha hali ya kuogopa, njaa, upungufu wa mali, iwe ni uzito kuyapata au yaondoke, upungufu wa watu: kwa kufa au kufa-shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kwa upungufu wa matunda ya mitende na mizabibu na nafaka: kwa kupungua mazao yake au kuharibika kwake.Wape, ewe Nabii, habari njema, wale wenye subira juu ya haya na mfano wake, kwa yale yatakayowafurahisha na kuwapendeza ya mwisho mwema duniani na Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
156 : 2

ٱلَّذِينَ إِذَآ أَصَٰبَتۡهُم مُّصِيبَةٞ قَالُوٓاْ إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّآ إِلَيۡهِ رَٰجِعُونَ

Miongoni mwa sifa za hawa wenye kusubiri ni kwamba wao wanapofikwa na kitu wanachokichukia husema, «Sisi ni waja waliomilikiwa na Mwenyezi Mungu, tunaoendeshwa kwa amri Yake na mapitisho Yake. Anafanya kwetu Alitakalo. Na sisi Kwake, Peke Yake, ni wenye kurudi kwa kufa, kisha kwa kufufuliwa ili kuhesabiwa na kulipwa. info
التفاسير:

external-link copy
157 : 2

أُوْلَٰٓئِكَ عَلَيۡهِمۡ صَلَوَٰتٞ مِّن رَّبِّهِمۡ وَرَحۡمَةٞۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُهۡتَدُونَ

Hao wenye kusubiri wana utajo mwema kutoka kwa Mola wao na rehema kubwa kutoka Kwake, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, na hao ndio walioongoka njia ya uongofu. info
التفاسير:

external-link copy
158 : 2

۞ إِنَّ ٱلصَّفَا وَٱلۡمَرۡوَةَ مِن شَعَآئِرِ ٱللَّهِۖ فَمَنۡ حَجَّ ٱلۡبَيۡتَ أَوِ ٱعۡتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَاۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيۡرٗا فَإِنَّ ٱللَّهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ

Hakika Swafa na Marwa, nayo ni majabali mawili madogo karibu ya Alkaba upande wa Mashariki, ni miongoni mwa alama za dini ya Mwenyezi Mungu zilizo wazi ambazo Mwenyezi Mungu Amezifanya ni sehemu za ibada kwa waja Wake kusai baina yake. Hivyo basi, yoyote mwenye kuikusudia Alkaba kwa kuhiji au kufanya Umra, si dhambi kwake kusai baina ya hayo majabali mawili, bali ni wajibu kwake kufanya hivyo. Na yule mwenye kufanya mambo ya kutii amri, kwa hiyari yake, hali ya kumtakasia Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushukuru, Analipa juu ya kichache kwa kingi, ni Mwenye kuzijua amali za waja Wake: Hazipotezi wala Hampunji yoyote chochote hata kama ni uzito wa chungu mdogo. info
التفاسير:

external-link copy
159 : 2

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡتُمُونَ مَآ أَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلۡهُدَىٰ مِنۢ بَعۡدِ مَا بَيَّنَّٰهُ لِلنَّاسِ فِي ٱلۡكِتَٰبِ أُوْلَٰٓئِكَ يَلۡعَنُهُمُ ٱللَّهُ وَيَلۡعَنُهُمُ ٱللَّٰعِنُونَ

Hakika wale ambao wanazificha aya zilizo waziwazi, zijulishazo utume wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na yale aliyokuja nayo, nao ni wanavyuoni wa Kiyahudi na wajuzi wa Kinaswara na wengineo, miongoni mwa wafichao yalyoteremshwa na Mwenyezi Mungu, baada ya sisi kuyadhihirisha kwa watu katika Taurati na Injili, hao Mwenyezi Mungu Atawafukuza kutoka kwenye rehema Yake, na viumbe wote watawaapiza laana. info
التفاسير:

external-link copy
160 : 2

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ وَأَصۡلَحُواْ وَبَيَّنُواْ فَأُوْلَٰٓئِكَ أَتُوبُ عَلَيۡهِمۡ وَأَنَا ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Isipokuwa wale waliorudi hali ya kutubia makosa yao, wakarekebisha waliyoyaharibu na wakayabainisha waliyoyaficha. Hao nitazikubali toba zao na nitawalipa kwa kuwasamehe. Na mimi ni Mwenye kukubali mno toba ya mwenye kutubia kati ya waja Wangu na ni Mwenye huruma kwao kwa kuwapa taufiki ya kutubia na kukubali toba kutoka kwao. info
التفاسير:

external-link copy
161 : 2

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَمَاتُواْ وَهُمۡ كُفَّارٌ أُوْلَٰٓئِكَ عَلَيۡهِمۡ لَعۡنَةُ ٱللَّهِ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ وَٱلنَّاسِ أَجۡمَعِينَ

Hakika wale waliokanusha imani na wakaficha haki na wakaendelea hivyo mpaka kufa kwao, juu yao kuna laana ya Mwenyezi Mungu na Malaika na watu wote kwa kuwatoa kwenye rehema Yake. info
التفاسير:

external-link copy
162 : 2

خَٰلِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ

Watadumu kwenye laana na Moto. Hawatapunguziwa adhabu, wala hawatapumzishwa na kungojewa kwa udhuru wowote watakaoutoa. info
التفاسير:

external-link copy
163 : 2

وَإِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلرَّحۡمَٰنُ ٱلرَّحِيمُ

Na Mola wenu, enyi watu, ni Mola Mmoja Aliyepwekeka katika dhati Yake, majina Yake, sifa Zake na vitendo Vyake na uja wa viumbe Vyake Kwake. Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, Mwingi wa rehema, Mwenye kusifika kwa sifa ya rehema katika dhati Yake, vitendo Vyake kwa waja Wake wote, na Mwenye kuwarehemu waumini. info
التفاسير: