Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução Suaíli - Abdullah Muhammad e Nasser Khamis

Número de página:close

external-link copy
19 : 13

۞ أَفَمَن يَعۡلَمُ أَنَّمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ ٱلۡحَقُّ كَمَنۡ هُوَ أَعۡمَىٰٓۚ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ

Je, yule anayejua kwamba kile ulichokuja nacho, ewe Mtume, ndicho ukweli unaotoka kwa Mwenyezi Mungu na akauamini ni kama kipofu asiyeuona ukweli ambaye hakuamini? Hakika wanaowaidhika ni wenye akili timamu info
التفاسير:

external-link copy
20 : 13

ٱلَّذِينَ يُوفُونَ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ وَلَا يَنقُضُونَ ٱلۡمِيثَٰقَ

ambao wanatekeleza ahadi ya Mwenyezi Mungu Ambayo Aliwaamrisha kwayo na wasiitangue ahadi ya mkazo ambayo walimuahidi nayo Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 13

وَٱلَّذِينَ يَصِلُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيَخۡشَوۡنَ رَبَّهُمۡ وَيَخَافُونَ سُوٓءَ ٱلۡحِسَابِ

Nao ndio ambao wanawaunga wale ambao Mwenyezi Mungu Amewaamrisha wawaunge kama jamaa wa karibu na wahitaji, wanamtunza Mola wao na wanaogopa Asiwahesabu kwa madhambi yao yote na Asiwasamehe chochote katika hayo. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 13

وَٱلَّذِينَ صَبَرُواْ ٱبۡتِغَآءَ وَجۡهِ رَبِّهِمۡ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنفَقُواْ مِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ سِرّٗا وَعَلَانِيَةٗ وَيَدۡرَءُونَ بِٱلۡحَسَنَةِ ٱلسَّيِّئَةَ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عُقۡبَى ٱلدَّارِ

Nao ndio ambao walivumilia udhia na kusimama juu ya utiifu na kujiepusha na uasi kwa kutafuta radhi za Mola wao, walitekeleza Swala kwa namna iliyotimia zaidi, walitekeleza Zaka za lazima za mali yao na matumizi yanayopendekezwa kwa siri na kwa dhahiri na wakawa wanaondoa baya kwa zuri lenye kulifuta. Hao wanaosifika kwa sifa hizi watakuwa na mwisho wenye kusifiwa huko Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 13

جَنَّٰتُ عَدۡنٖ يَدۡخُلُونَهَا وَمَن صَلَحَ مِنۡ ءَابَآئِهِمۡ وَأَزۡوَٰجِهِمۡ وَذُرِّيَّٰتِهِمۡۖ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ يَدۡخُلُونَ عَلَيۡهِم مِّن كُلِّ بَابٖ

Mwisho wao ni mabustani ya Pepo ya 'Adn, watakaa humo, hawataondoka kutoka humo, na pamoja nao watakuwamo waliokuwa wema miongoni mwa mababa, wake na watoto waume kwa wake, na huku malaika waingia kwao kutoka kila mlango wakipongeza na kuingia Peponi. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 13

سَلَٰمٌ عَلَيۡكُم بِمَا صَبَرۡتُمۡۚ فَنِعۡمَ عُقۡبَى ٱلدَّارِ

Malaika watawaambia, «Amani iwashukie, yakiwa ni maamkizi yenu peke yenu, na msalimike na kila baya kwa uvumilivu wenu katika kumtii Mwenyezi Mungu. Neema ya nyumba ya mwisho ni Pepo.» info
التفاسير:

external-link copy
25 : 13

وَٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهۡدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مِيثَٰقِهِۦ وَيَقۡطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمُ ٱللَّعۡنَةُ وَلَهُمۡ سُوٓءُ ٱلدَّارِ

Ama waovu, wamesifiwa kwa sifa kinyume na zile za Waumini. Wao ni wale ambao hawatekelezi ahadi za Mwenyezi Mungu kwa kumpwekesha, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, kwa ibada baada ya kujitukulia ahadi ya mkazo. Na wao ni wale wanaokata kile ambacho Mwenyezi Mungu amewaamrisha kukiunga kama vile kukata zao na mengineyo na wanafanya uharibifu katika ardhi kwa kufanya maasia. Hao waliosifiwa kwa sifa hizi mbaya watakalolipata ni kufukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu na watakuwa na mambo ambayo ni mabaya kwao ya adhabu kali katika Nyumba ya Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 13

ٱللَّهُ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقۡدِرُۚ وَفَرِحُواْ بِٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا فِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِلَّا مَتَٰعٞ

Mwenyezi Mungu Peke Yake Anamkunjulia riziki Anayemtaka miongoni mwa waja Wake na Anambania Anayemtaka kati yao. Na makafiri waliufurahia ukunjufu duniani. Na dunia hii haikuwa ikilinganishwa na Akhera isipokuwa ni kitu kidogo cha kustarehe nacho, na kwa haraka sana kinaondoka. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 13

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦۚ قُلۡ إِنَّ ٱللَّهَ يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِيٓ إِلَيۡهِ مَنۡ أَنَابَ

Na makafiri wanasema kwa kushindana, «Si ateremshiwe Muhammad miujiza inayoonekena kama miujiza ya Mūsā na 'Īsā. Waambie kwamba Mwenyezi Mungu Anampoteza Anayemtaka miongoni mwa washindani wasiotaka uongofu na haimfai miujiza na Anawaongoza kwenye dini Yake ya haki anayerejea Kwake na kutaka radhi Zake. info
التفاسير:

external-link copy
28 : 13

ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَطۡمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكۡرِ ٱللَّهِۗ أَلَا بِذِكۡرِ ٱللَّهِ تَطۡمَئِنُّ ٱلۡقُلُوبُ

Na Anawaongoza wale ambao nyoyo zao zimetulia kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtaja zikapata utulivu. Jua utanabahi kwamba kumtii Mwenyezi Mungu, kumtaja na malipo mema kutoka Kwake yanafanya nyoyo zitulie na zipumbae. info
التفاسير: