Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução Suaíli - Abdullah Muhammad e Nasser Khamis

Número de página:close

external-link copy
14 : 13

لَهُۥ دَعۡوَةُ ٱلۡحَقِّۚ وَٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَسۡتَجِيبُونَ لَهُم بِشَيۡءٍ إِلَّا كَبَٰسِطِ كَفَّيۡهِ إِلَى ٱلۡمَآءِ لِيَبۡلُغَ فَاهُ وَمَا هُوَ بِبَٰلِغِهِۦۚ وَمَا دُعَآءُ ٱلۡكَٰفِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَٰلٖ

Ni wa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Peke Yake, ulinganizi wa tawhīd «Hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu.» Haabudiwi wala haombwi isipokuwa Yeye. Na waungu ambao wao wanawaabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawaitiki maombi ya mwenye kuwaomba. Na hali yao pamoja na hao waungu ni kama hali ya mwenye kiu anayenyosha vitanga vyake viwili vya mkono kwenye maji kutoka mbali ili yafike kwenye kinywa chake, yakawa hayafiki. Na maombi ya makafiri kwa hao waungu hayakuwa isipokuwa yako mbali na usawa, kwa kuwa wao wanamshirikisha wengine pamoja na Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 13

وَلِلَّهِۤ يَسۡجُدُۤ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ طَوۡعٗا وَكَرۡهٗا وَظِلَٰلُهُم بِٱلۡغُدُوِّ وَٱلۡأٓصَالِ۩

Na Mwenyezi Mungu Peke Yake wanamsujudia, wakinyenyekea na kufuata, walioko mbinguni na ardhini wote, Waumini wanamsujudia na kumnyenyekea kwa ridhaa na hiari, na makafiri wanamnyenyekea kwa nguvu, kwa kuwa wao wanafanya kiburi kumuabudu na hali yao na maumbile yao yanawakanusha juu ya hilo. Na vivuli vya viumbe vinafuata utukufu wa Mwenyezi Mungu, vinatembea kulingana na matakwa Yake mwanzo wa mchana na mwisho wake. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 13

قُلۡ مَن رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ قُلِ ٱللَّهُۚ قُلۡ أَفَٱتَّخَذۡتُم مِّن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَ لَا يَمۡلِكُونَ لِأَنفُسِهِمۡ نَفۡعٗا وَلَا ضَرّٗاۚ قُلۡ هَلۡ يَسۡتَوِي ٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡبَصِيرُ أَمۡ هَلۡ تَسۡتَوِي ٱلظُّلُمَٰتُ وَٱلنُّورُۗ أَمۡ جَعَلُواْ لِلَّهِ شُرَكَآءَ خَلَقُواْ كَخَلۡقِهِۦ فَتَشَٰبَهَ ٱلۡخَلۡقُ عَلَيۡهِمۡۚ قُلِ ٱللَّهُ خَٰلِقُ كُلِّ شَيۡءٖ وَهُوَ ٱلۡوَٰحِدُ ٱلۡقَهَّٰرُ

Waambie washirikina, ewe Mtume, «Ni nani muumba mbingu na ardhi na mwenye kuziendesha?» Sema, «Mwenyezi Mungu Ndiye Muuumba Mwenye kuziendesha. Na nyinyi mnalikubali hilo.» Kisha waambie ukiwalazimisha hoja, «Je, mnawafanya wasiokuwa Yeye ni waabudiwa wenu, na hali ya kuwa wao hawawezi kuzinufaisha nafsi zao au kuzidhuru, wacha kule kuwanufaisha nyinyi au kuwadhuru, na mkaacha kumuabudu mwenye kuwamiliki wao?» Waambie, «Kwani analingana kwenu nyinyi kafiri, ambaye ni kama kipofu, na Muumini, ambaye ni kama anayeona? Au kwani unalingana kwenu nyinyi ukafiri, ambao ni kama giza, na Imani, ambayo ni kama mwangaza? Au ni kwamba wale wasimamizi wao wanaowafanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu wanaumba kama Anavyoumba, vikawatatiza viumbe vya washirika na viumbe vya Mwenyezi Mungu, ndipo wakaitakidi kwamba wao wanastahiki kuabudiwa?» Waambie, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu Aliyetukuka ni Muumba kila kilichoko ambacho hakikuwako; Yeye Ndiye Anayestahiki kuabudiwa Peke Yake na Yeye Ndiye Aliye mmoja Mwenye kutendesha nguvu Anayestahiki uungu na ibada, na sio masanamu na mizimu isiyodhuru wala kunufaisha.» info
التفاسير:

external-link copy
17 : 13

أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَسَالَتۡ أَوۡدِيَةُۢ بِقَدَرِهَا فَٱحۡتَمَلَ ٱلسَّيۡلُ زَبَدٗا رَّابِيٗاۖ وَمِمَّا يُوقِدُونَ عَلَيۡهِ فِي ٱلنَّارِ ٱبۡتِغَآءَ حِلۡيَةٍ أَوۡ مَتَٰعٖ زَبَدٞ مِّثۡلُهُۥۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡحَقَّ وَٱلۡبَٰطِلَۚ فَأَمَّا ٱلزَّبَدُ فَيَذۡهَبُ جُفَآءٗۖ وَأَمَّا مَا يَنفَعُ ٱلنَّاسَ فَيَمۡكُثُ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡأَمۡثَالَ

Kisha Mwenyezi Mungu Akapiga mfano wa ukweli na urongo kuwa ni kama maji Aliyoyateremsha kutoka juu, yakapita kwenye mabonde ya ardhi kwa kadiri ya udogo wake na ukubwa wake, mikondo ya maji ikabeba povu likiwa juu yake lisilo na faida. Na akapiga mfano mwingine wa madini ambayo watu huyachoma moto ili kuyayeyusha kutaka kutengeneza pambo, kama vile dhahabu na fedha, au kutaka manufaa ya kujinufaisha, kama vile shaba, ukatoka uchafu wake usio na faida kama ule uliokuwa pamoja na maji. Kwa mfano huu, Mwenyezi Mungu Apigia mfano ukweli na urongo. Urongo ni kama povu la maji, linapotea au linatupwa kwa kuwa halina faida, na ukweli ni kama maji safi na madini yaliyotakasika, yanasalia kwenye ardhi kwa kunufaika nayo. Kama Alivyowafafanulia nyinyi mifano hii, hivyo ndivyo Anavyoipiga kwa watu upate kufunuka wazi ukweli ujitenge na urongo, na uongofu ujitenge na upotevu. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 13

لِلَّذِينَ ٱسۡتَجَابُواْ لِرَبِّهِمُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَٱلَّذِينَ لَمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَهُۥ لَوۡ أَنَّ لَهُم مَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا وَمِثۡلَهُۥ مَعَهُۥ لَٱفۡتَدَوۡاْ بِهِۦٓۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ سُوٓءُ ٱلۡحِسَابِ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ

Pepo ni ya wenye kuamini ambao wanamtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na Moto ni wa wale ambao hawakumtii na wakamkanusha. Na lau walikuwa wanamiliki kila kilichoko ardhini na zaidi ya kama hiko pamoja nacho, wangalikitoa kwa kujikomboa nafsi zao na adhabu ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, na hakingalikubaliwa kutoka kwao. Wao watafanyiwa hesabu kwa kila tendo baya walilolitenda. Na makazi yao ya kukaa ni Jahanamu, itakuwa ni tandiko kwao. Na tandiko baya mno ni hilo walilojitayarishia nafsi zao. info
التفاسير: