Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - Swahili vertaling - Abdoellah Mohammed en Nasser Khamees

Al-Mumtahanah

external-link copy
1 : 60

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمۡ أَوۡلِيَآءَ تُلۡقُونَ إِلَيۡهِم بِٱلۡمَوَدَّةِ وَقَدۡ كَفَرُواْ بِمَا جَآءَكُم مِّنَ ٱلۡحَقِّ يُخۡرِجُونَ ٱلرَّسُولَ وَإِيَّاكُمۡ أَن تُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ رَبِّكُمۡ إِن كُنتُمۡ خَرَجۡتُمۡ جِهَٰدٗا فِي سَبِيلِي وَٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِيۚ تُسِرُّونَ إِلَيۡهِم بِٱلۡمَوَدَّةِ وَأَنَا۠ أَعۡلَمُ بِمَآ أَخۡفَيۡتُمۡ وَمَآ أَعۡلَنتُمۡۚ وَمَن يَفۡعَلۡهُ مِنكُمۡ فَقَدۡ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo! Msiwachukue maadui wangu na maadui wenu mkawafanya ni marafiki halisi na vipenzi, mkawa mnaamiliana na wao kwa upendo na mkawapasha habari za Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Waislamu wengine, na hali wao wameikanusha haki iliyowajia ya kumuamini Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Qur’ani iliyoteremshwa kwake. Wanamtoa Mtume na wanawatoa nyinyi, enyi Waumini, kutoka Makkah kwa kuwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu Mola wenu na mnampwekesha. Mkiwa nyinyi, enyi Waumini, mmehama kwa kupigana jihadi katika njia yangu kwa kutafuta radhi yangu kwenu, basi msifanye urafiki na maadui wangu na maadui wenu. Mnawaambia wao kwa siri kuwa mnawapenda, na mimi ninayajua mnayoyaficha na mnayoyadhihirisha. Na yoyote anayefanya hivyo miongoni mwenu, ashakosea njia ya haki na sawa na amepotea njia ya wastani. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 60

إِن يَثۡقَفُوكُمۡ يَكُونُواْ لَكُمۡ أَعۡدَآءٗ وَيَبۡسُطُوٓاْ إِلَيۡكُمۡ أَيۡدِيَهُمۡ وَأَلۡسِنَتَهُم بِٱلسُّوٓءِ وَوَدُّواْ لَوۡ تَكۡفُرُونَ

Wakiwapatia nafasi nyinyi hao mnaowapenda kwa siri watawapiga vita na watanyosha mikono yao kwenu, wawaue nyinyi na wawateke, na pia ndimi zao, wawatukane nyinyi na wawatusi, na wao walitamani, kwa hali yoyote, lau nyinyi mlikanusha kama wao. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 60

لَن تَنفَعَكُمۡ أَرۡحَامُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُمۡۚ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَفۡصِلُ بَيۡنَكُمۡۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Hawatawanufaisha nyinyi jamaa zenu wa karibu wala watoto wenu kitu chochote mnapofanya urafiki na wakanushaji kwa ajili yao. Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu Atawatenganisha nyinyi na wao, Awatie Peponi wanaomtii na Awatie Motoni wanaomuasi. Na Mwenyezi Mungu Anayaona mnayoyafanya, hakuna chochote kinachofichamana Kwake cha maneno yenu na matendo yenu. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 60

قَدۡ كَانَتۡ لَكُمۡ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ فِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥٓ إِذۡ قَالُواْ لِقَوۡمِهِمۡ إِنَّا بُرَءَٰٓؤُاْ مِنكُمۡ وَمِمَّا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ كَفَرۡنَا بِكُمۡ وَبَدَا بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكُمُ ٱلۡعَدَٰوَةُ وَٱلۡبَغۡضَآءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَحۡدَهُۥٓ إِلَّا قَوۡلَ إِبۡرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسۡتَغۡفِرَنَّ لَكَ وَمَآ أَمۡلِكُ لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۖ رَّبَّنَا عَلَيۡكَ تَوَكَّلۡنَا وَإِلَيۡكَ أَنَبۡنَا وَإِلَيۡكَ ٱلۡمَصِيرُ

Kwa hakika mlikuwa na kiigizo kizuri, enyi Waumini, kwa Ibrāhīm na wale waliokuwa pamoja na yeye waliposema kuwaambia wakanushaji Mwenyezi Mungu, «Sisi tumejiepusha na nyinyi na vile mnavyoviabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tumewakanusha nyinyi na tumeukataa ukafiri mlionao, na umejitokeza nje uadui na machukivu ya milele baina yetu sisi na nyinyi madamu bado mko kwenye ukanushaji wenu, mpaka mmuamini Mwenyezi Mungu Peke Yake.» Lakini haliingii kwenye kuigiza tendo la Ibrāhīm la kumuombea msamaha babake, kwa kuwa hilo lilitokea kabla ya Ibrāhīm kufunukiwa kuwa babake ni adui wa Mwenyezi Mungu, na alipofunukiwa kuwa yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu alijiepusha na yeye. Mola wetu! Kwako wewe tumetegemea, na kwako wewe tumerejea kwa kutubia, na kwako wewe ndiko marejeo Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 60

رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ وَٱغۡفِرۡ لَنَا رَبَّنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Mola wetu! Usitufanye ni mtihani wa wale waliokukanusha wewe, kwa kutuadhibu au kuwapa nguvu makafiri juu yetu wakatufitini kwa kutuepusha na Dini yetu au wakawa na nguvu juu yetu wakafitinika kwa hilo na hapo waseme, «Lau hawa wangalikuwa kwenye haki haingaliwapata adhabu hii,» na wazidi ukafiri. Na utufinikie dhambi zetu kwa kutusamehe, ewe Mola wetu! Hakika wewe ni Mshindi Asiyekuwa na mwenye kushindana Naye, Mwingi wa hekima katika maneno Yake na matendo Yake. info
التفاسير: