Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - Swahili vertaling - Abdoellah Mohammed en Nasser Khamees

external-link copy
8 : 6

وَقَالُواْ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ مَلَكٞۖ وَلَوۡ أَنزَلۡنَا مَلَكٗا لَّقُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ ثُمَّ لَا يُنظَرُونَ

Na walisema washirikina hawa, «Si Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amteremshie Muhammad Malaika kutoka mbinguni ili amsadiki kwa yale aliyokuja nayo Ya utume.» Na lau tulimteremsha Malaika kutoka mbinguni kwa kujibu ombi lao, uamuzi wa kuwaangamiza ungalipitishwa, na wasingepewa muhula wa kutubia, kwani imetangulia kwenye ujuzi wa Mwenyezi Mungu kuwa wao hawataamini. info
التفاسير: