Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - Swahili vertaling - Abdoellah Mohammed en Nasser Khamees

external-link copy
47 : 6

قُلۡ أَرَءَيۡتَكُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُ ٱللَّهِ بَغۡتَةً أَوۡ جَهۡرَةً هَلۡ يُهۡلَكُ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Nambieni iwapo mateso ya Mwenyezi Mungu yamewashukia ghafla na hali kwamba nyinyi hamuna hisia nayo, au yakawa waziwazi yanaonekana na nyinyi mnayaangalia: Je, kwani kuna wanaoteswa isipokuwa wale watu madhalimu ambao wamekiuka mpaka kwa kuipeleka ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi mungu, Aliyetukuka, na kwa kukanusha kwao Mitume Yake?» info
التفاسير: