Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - Swahili vertaling - Abdoellah Mohammed en Nasser Khamees

Pagina nummer:close

external-link copy
53 : 29

وَيَسۡتَعۡجِلُونَكَ بِٱلۡعَذَابِ وَلَوۡلَآ أَجَلٞ مُّسَمّٗى لَّجَآءَهُمُ ٱلۡعَذَابُۚ وَلَيَأۡتِيَنَّهُم بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ

Na wanakuharakisha, ewe Mtume, hawa washirikina wa watu wako uwaletee adhabu kwa kukufanyia shere. Na lau si Mwenyezi Mungu kuwa Amewawekea wakati wa kuadhibiwa wao duniani usiotangulia wala kuchelewa, ingaliwajia wao adhabu pale walipoitaka. Na kwa hakika itawajia ghafula na hali wao hawaitambui wala kuihisi. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 29

يَسۡتَعۡجِلُونَكَ بِٱلۡعَذَابِ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةُۢ بِٱلۡكَٰفِرِينَ

Wanakuharakisha uwaletee adhabu ulimwenguni, na hali hiyo ni yenye kuwajia hapana budi, ima hapa ulimwenguni au huko Akhera. Na kwa hakika adhabu ya Jahanamu huko Akhera ni yenye kuwazunguka, hawana makimbilio nayo. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 29

يَوۡمَ يَغۡشَىٰهُمُ ٱلۡعَذَابُ مِن فَوۡقِهِمۡ وَمِن تَحۡتِ أَرۡجُلِهِمۡ وَيَقُولُ ذُوقُواْ مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Hiyo Siku ya Kiyama, adhabu ya Jahanamu itawafinika makafiri upande wa juu ya vichwa vyao na upande wa chini ya nyayo zao. Hivyo basi Moto utawazunguka pande zao zote, na Mwenyezi Mungu Atasema kuwaambia wakati huo, «Onjeni malipo ya yale mliokuwa mkiyafanya ulimwenguni, ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kufanya uhalifu na madhambi. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 29

يَٰعِبَادِيَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ أَرۡضِي وَٰسِعَةٞ فَإِيَّٰيَ فَٱعۡبُدُونِ

«Enyi waja wangu mlioamini! Iwapo muna shida ya kudhihirisha Imani na ibada ya Mwenyezi Mungu Peke Yake, basi hamieni kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu iliyo kunjufu na munitakasie ibada mimi peke yangu.» info
التفاسير:

external-link copy
57 : 29

كُلُّ نَفۡسٖ ذَآئِقَةُ ٱلۡمَوۡتِۖ ثُمَّ إِلَيۡنَا تُرۡجَعُونَ

Kila nafsi iliyo hai ni yenye kuonja kifo, kisha kwetu sisi mtarejea muhesabiwe na mulipwe. info
التفاسير:

external-link copy
58 : 29

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَنُبَوِّئَنَّهُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ غُرَفٗا تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ نِعۡمَ أَجۡرُ ٱلۡعَٰمِلِينَ

Na wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya matendo mema waliyoamrishwa kwayo, tutawatayarishia katika Pepo vyumba vilivyo juu, ambavyo chini yake inapita mito, hali ya kukaa humo milele.Neema ya malipo ya wenye kufanya utiifu kwa Mwenyezi Mungu ni Vyumba hivi vilivyoko ndani ya Mabustani ya starehe. info
التفاسير:

external-link copy
59 : 29

ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

Mabustani hayo yaliyotajwa ni ya Waumini waliovumilia katika kumuabudu Mwenyezi Mungu, wakashikamana na dini yao na wakawa wanamtegemea Mwenyezi Mungu katika riziki zao na kupigana jihadi na maadui wao. info
التفاسير:

external-link copy
60 : 29

وَكَأَيِّن مِّن دَآبَّةٖ لَّا تَحۡمِلُ رِزۡقَهَا ٱللَّهُ يَرۡزُقُهَا وَإِيَّاكُمۡۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Ni viumbe vingapi vitambaavyo visivyojiwekea akiba ya chakula chao cha kesho, kama vile mwanadamu anavyofanya. Basi Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kuwa juu, Anaviruzuku kama Anavyowaruzuku nyinyi. Na Yeye ni Msikizi wa maneno yenu, ni Mjuzi wa vitendo vyenu na mawazo ya nyoyo zenu. info
التفاسير:

external-link copy
61 : 29

وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّنۡ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُۖ فَأَنَّىٰ يُؤۡفَكُونَ

Na ukiwauliza, ewe Mtume, hao washirikina,»Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi kwa mpango huu mzuri na akalidhalilisha jua na mwezi?» Watasema, «Aliyeviumba hivyo ni Mwenyezi Mungu Peke Yake.» Basi vipi wao watapotoshwa waache kumuamini Mwenyezi Mungu, Muumba na Muendeshaji wa kila kitu, na wakawa wanamuabudu asiyekuwa Yeye? Basi uonee ajabu uzushi wao na urongo wao! info
التفاسير:

external-link copy
62 : 29

ٱللَّهُ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦ وَيَقۡدِرُ لَهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ

Mwenyezi Mungu, aliyetakasika na kuwa juu, Anampanulia riziki Anayemtaka na Anawabania wengine katika wao, kwa kuwa Anayajua yanayowafaa waja Wake. Hakika Mwenyezi Mungu kwa kila jambo, katika hali zenu na mambo yenu, ni Mjuzi, hakuna chochote kinachofichamana Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
63 : 29

وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّن نَّزَّلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِ مَوۡتِهَا لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُۚ قُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ

Na ukiwauliza, ewe Mtume, hao washirikina, «Ni nani anayeteremsha maji kutoka mawinguni, yakaotesha mimea juu ya ardhi baada ya kuwa imekauka?» watakwambia huku wakikubali, «Mwenyezi Mungu Peke Yake Ndiye Anayeyateremsha hayo.» Sema, «Shukrani ni za Mwenyezi Mungu Aliyedhihirisha hoja yako kwao. Lakini wengi wao hawafahamu yanayowafaa wala yanayowadhuru, na lau waelewa hawangalimshirikisha Mwenyezi Mungu na Mwengine. info
التفاسير: