Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - Swahili vertaling - Abdoellah Mohammed en Nasser Khamees

Pagina nummer:close

external-link copy
73 : 21

وَجَعَلۡنَٰهُمۡ أَئِمَّةٗ يَهۡدُونَ بِأَمۡرِنَا وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡهِمۡ فِعۡلَ ٱلۡخَيۡرَٰتِ وَإِقَامَ ٱلصَّلَوٰةِ وَإِيتَآءَ ٱلزَّكَوٰةِۖ وَكَانُواْ لَنَا عَٰبِدِينَ

Na tukamfanya Ibrāhīm, Isḥāq na Ya'qūb kuwa viongozi wa watu, wanawalingania wamuabudu Yeye na kumtii kwa idhini Yake Aliyetukuka, na tuliwaletea wahyi kufanya mema ya kuzifuata kivitendo sheria za Manabii, kusimamisha Swala kwa njia zake na kutoa Zaka. Na wao walizifuata amri hizo na walikuwa watiifu kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake bila Mwingine. info
التفاسير:

external-link copy
74 : 21

وَلُوطًا ءَاتَيۡنَٰهُ حُكۡمٗا وَعِلۡمٗا وَنَجَّيۡنَٰهُ مِنَ ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلَّتِي كَانَت تَّعۡمَلُ ٱلۡخَبَٰٓئِثَۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمَ سَوۡءٖ فَٰسِقِينَ

Na tulimpa Lūṭ unabii, kufanya uamuzi baina ya watesi na ujuzi wa amri za Mwenyezi Mungu na Dini Yake. Na tulimuokoa na kijiji chake Sadūm ambacho watu wake walikuwa wakifanya mambo machafu. Wao, kwa sababu ya machafu na maovu ambayo watu wa uovu na uchafu wakiyatenda, walikuwa nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
75 : 21

وَأَدۡخَلۡنَٰهُ فِي رَحۡمَتِنَآۖ إِنَّهُۥ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Na Mwenyezi Mungu Akamkamilishia nema, Akamtia ndani ya rehema Yake kwa kumuokoa na kile kilichowafikia watu wake kwa kuwa yeye alikuwa ni miongoni mwa wale wanaofanya matendo ya utiifu Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
76 : 21

وَنُوحًا إِذۡ نَادَىٰ مِن قَبۡلُ فَٱسۡتَجَبۡنَا لَهُۥ فَنَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥ مِنَ ٱلۡكَرۡبِ ٱلۡعَظِيمِ

Na mkumbuke Nūḥ, ewe Mtume, alipomuita Mola Wake kabla yako na kabla ya Ibrāhīm na Lūṭ, tukaitika mwito wake na tukamuokoa, yeye na watu wake waliomuamini, na makero makubwa. info
التفاسير:

external-link copy
77 : 21

وَنَصَرۡنَٰهُ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمَ سَوۡءٖ فَأَغۡرَقۡنَٰهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Na tukamnusuru na vitimbi vya watu waliozikanusha alama zetu zenye kuonesha ukweli wake. Kwa haki, wao walikuwa ni watu wa ubaya, na hivyo basi tuliwazamisha wote kwa mafuriko. info
التفاسير:

external-link copy
78 : 21

وَدَاوُۥدَ وَسُلَيۡمَٰنَ إِذۡ يَحۡكُمَانِ فِي ٱلۡحَرۡثِ إِذۡ نَفَشَتۡ فِيهِ غَنَمُ ٱلۡقَوۡمِ وَكُنَّا لِحُكۡمِهِمۡ شَٰهِدِينَ

Na kumbuka Nabii wa Mwenyezi Mungu Dāwūd na mwane Sulaiman, ewe Mtume, walipotoa uamuzi juu ya kesi iliyoletwa na wagonvi wawili, kondoo wa mmoja wao waliharibu mimea ya mwingine, walienea kwenye mimea hiyo kipindi cha usiku wakaiharibu. Dāwūd alitoa uamuzi kwamba wale kondoo wawe ni milki ya mwenye mimea wakiwa ni badala ya mimea yake iliyoharibiwa, kwa kuwa thamani ya viwili hivyo ni sawa. Na sisi tuliushuhudia uamuzi wao, haukufichamana kwetu. info
التفاسير:

external-link copy
79 : 21

فَفَهَّمۡنَٰهَا سُلَيۡمَٰنَۚ وَكُلًّا ءَاتَيۡنَا حُكۡمٗا وَعِلۡمٗاۚ وَسَخَّرۡنَا مَعَ دَاوُۥدَ ٱلۡجِبَالَ يُسَبِّحۡنَ وَٱلطَّيۡرَۚ وَكُنَّا فَٰعِلِينَ

Tukamfahamisha Sulaymān kuzingatia maslahi ya pande mbili na kufanya uadilifu, akatoa uamuzi kwamba yule mwenye kondoo ashughulike kutengeneza mimea iliyoharibika na kumalizika kwa muda maalumu ambapo katika muda huo yule mwenye mimea ajifaidishe kwa manufaa ya kondoo, kama vile maziwa, sufi na mfano wake, na baadaye kondoo warudi kwa mwenyewe na mimea irudi kwa mwenyewe, kwa kuwa thamani ya mimea iliyoharibiwa inalingana na manufaa ya wale kondoo. Na kila mmoja kati ya Dāwūd na Sulaymān tulimpa busara na ujuzi. Na tulimfanyia Dāwūd wema wa kumdhalilishia majabali yakawa yanaleta tasbihi anapoleta tasbihi, na vilevile ndege wakawa wanaleta tasbihi, na sisi tulikuwa ni wenye kulifanya hilo. info
التفاسير:

external-link copy
80 : 21

وَعَلَّمۡنَٰهُ صَنۡعَةَ لَبُوسٖ لَّكُمۡ لِتُحۡصِنَكُم مِّنۢ بَأۡسِكُمۡۖ فَهَلۡ أَنتُمۡ شَٰكِرُونَ

Na Mwenyezi Mngu Alimhusu Dāwūd, amani imshukiye, kwa kumfundisha kutengeneza nguo za kivita, akizifanya kwa kutunga vikuku vilivyoshikamana, kurahisisha harka ya mwili, ili kuwakinga wapiganaji wasiathiriwe na silaha wanazopigwa. Je, nyinyi ni wenye kushukuru neema ya Mwenyezi Mungu kwenu kupitia kwa mkono wa mja Wake Dāwūd? info
التفاسير:

external-link copy
81 : 21

وَلِسُلَيۡمَٰنَ ٱلرِّيحَ عَاصِفَةٗ تَجۡرِي بِأَمۡرِهِۦٓ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ ٱلَّتِي بَٰرَكۡنَا فِيهَاۚ وَكُنَّا بِكُلِّ شَيۡءٍ عَٰلِمِينَ

Na tulimdhalilishia Sulaymān upepo wenye kuvuma kwa kasi ukimchukua yeye na walio pamoja naye, ukawa unapita kwa amri yake kuelekea ardhi ya Bayt al-Maqdis iliyoko Shām amabayo tuliibariki kwa kheri nyingi. Na ujuzi wetu umeenea vitu vyote. info
التفاسير: