पवित्र कुरअानको अर्थको अनुवाद - स्वाहिली अनुवाद : अली मुहसिन बरवानी ।

Al-Waqi'ah

external-link copy
1 : 56

إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ

Litakapo tukia hilo Tukio . info

Kitakapo tukia Kiyama

التفاسير:

external-link copy
2 : 56

لَيۡسَ لِوَقۡعَتِهَا كَاذِبَةٌ

Hapana cha kukanusha kutukia kwake. info

Haitotokea nafsi yoyote ya kukadhibisha.

التفاسير:

external-link copy
3 : 56

خَافِضَةٞ رَّافِعَةٌ

Literemshalo linyanyualo! info

Kiyama hicho kitawateremsha chini walio waovu, na kitawanyanyua juu walio wema.

التفاسير:

external-link copy
4 : 56

إِذَا رُجَّتِ ٱلۡأَرۡضُ رَجّٗا

Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso! info

Ardhi itakapo tikiswa, na ikatetemeshwa kwa nguvu.

التفاسير:

external-link copy
5 : 56

وَبُسَّتِ ٱلۡجِبَالُ بَسّٗا

Na milima itapo sagwasagwa! info

Na milima ikavurugwa teketeke,

التفاسير:

external-link copy
6 : 56

فَكَانَتۡ هَبَآءٗ مُّنۢبَثّٗا

Iwe mavumbi yanayo peperushwa! info

Ikawa vumbi la kupeperushwa, Aya hizi tukufu zinaeleza hadi gani vitakuwa vitisho vitavyo uteremkia ulimwengu kitapo fika Kiyama. Na katika vitisho hivyo ni hayo masaibu ya dunia yatakayo athiri ardhi na mat'abaka yake. Kwani hii ardhi tunayo ishi juu ya mgongo wake si yenye kutulia na kukaa sawa kwa utimilivu. Kwani hiyo imeundwa kwa mat'abaka ya majabali yaliyo ingiliana ovyo. Huenda baadhi yao yakateremka yakaachana na mengineyo yaliyo jirani nayo. Na huwa hiyo inayo itwa kupasuka kwa mat'abaka ya ardhi, Geological cleavage kama inavyo tokea katika maeneo kadhaa wa kadhaa. Mpasuko huu ulikuwa na ungali kuwa ndio asili ya chini kabisa ya zilzala, mitetemeko, mikubwa kwa kuathirika na nguvu za kudidimiza na kuvuta zinazo fuatana na mat'abaka ya ardhi yanapo vunjika. Basi mizani ya utulivu ya nguvu hizi inapo geuka kwa kuathirika na mambo mengineyo ya nje huenda zikafunguka nguvu za mtikiso mkubwa ndio ikatokea mitetemeko na mitikisiko ya ardhi, ambayo hubomoa kila kitu kiliopo juu ya ardhi karibu na ilipo anzia hiyo zilzala. Na hapo tena hutokea uharibifu mkubwa mno. Na hayo maelezo ya kisayansi hayageuzi kitu, wala hayako mbali na nadhari ya kidini. Kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu huenda akajaalia sababu za maumbile za kawaida zikajumuika kwa njia tusiyo izoea sisi ili zikiingiliana kwa njia ya kutisha ndio sababu ya kuharibika dunia. Hapo maelezo ya kisayansi yanafuatana na Aya zenye kuonya kwa vitisho hivyo vikuu. Na yote hayo yanatokana kwa Mwenyezi Mungu. Na hutokea kwa idhini yake Mwenyezi Mungu kutimiza hukumu yake katika dunia yetu.

التفاسير:

external-link copy
7 : 56

وَكُنتُمۡ أَزۡوَٰجٗا ثَلَٰثَةٗ

Na nyinyi mtakuwa namna tatu: . info

Na mkawa nyote siku hiyo namna tatu kwa mujibu wa vitendo vyenu;

التفاسير:

external-link copy
8 : 56

فَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ

Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani? info

Basi watu wa mkono wa kulia, watu wa cheo kilio bora, utukufu ulioje huo wa hali yao!

التفاسير:

external-link copy
9 : 56

وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ

Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni? info

Na watu wa kushotoni, hao ni watu wa cheo duni, uovu ulioje wa hali yao!

التفاسير:

external-link copy
10 : 56

وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلسَّٰبِقُونَ

Na wa mbele watakuwa mbele. info

Na walio tangulia mbele katika mambo ya kheri duniani ndio watakuwa mbele katika vyeo vya Akhera.

التفاسير:

external-link copy
11 : 56

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡمُقَرَّبُونَ

Hao ndio watakao karibishwa info

Hao ndio walio karibishwa mbele kwa Mwenyezi Mungu. Mola wao Mlezi atawatia katika Bustani zenye neema.

التفاسير:

external-link copy
12 : 56

فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ

Katika Bustani zenye neema. info

Mola wao Mlezi atawatia katika Bustani zenye neema.

التفاسير:

external-link copy
13 : 56

ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ

Fungu kubwa katika wa mwanzo, info

Hawa walio karibishwa mbele ni kundi la wengi katika mataifa yaliyo tangulia na Manabii wao,

التفاسير:

external-link copy
14 : 56

وَقَلِيلٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ

Na wachache katika wa mwisho. info

Na wachache katika umma wa Muhammad ukiwalinganisha na hao.

التفاسير:

external-link copy
15 : 56

عَلَىٰ سُرُرٖ مَّوۡضُونَةٖ

Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa. info

Juu ya viti au vitanda vilivyo nakishiwa kwa nakshi za vito vya thamani,

التفاسير:

external-link copy
16 : 56

مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيۡهَا مُتَقَٰبِلِينَ

Wakiviegemea wakielekeana. info

wakivitegemea kwa raha na utulivu huku wakielekezana nyuso kwa ziada ya mahaba.

التفاسير:

external-link copy
17 : 56

يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ

Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele, info

Wakiwazungukia kwa kuwakhudumia vijana watakao baki milele hivyo hivyo,

التفاسير:

external-link copy
18 : 56

بِأَكۡوَابٖ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسٖ مِّن مَّعِينٖ

Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi. info

Nao wamechukua vikombe na mabirika yaliyo jaa vinywaji vya Peponi, na bilauri zenye mvinyo kutoka chemchem zinazo miminika,

التفاسير:

external-link copy
19 : 56

لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ

Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa. info

Vinywaji hivyo haviwaletei kuumwa kichwa wala kutokwa akili kwa ulevi.

التفاسير:

external-link copy
20 : 56

وَفَٰكِهَةٖ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ

Na matunda wayapendayo, info

Na matunda ya kila namna wanayo yapenda na wanayo yaona;

التفاسير:

external-link copy
21 : 56

وَلَحۡمِ طَيۡرٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ

Na nyama za ndege kama wanavyo tamani. info

Na nyama za ndege kama zinavyo tamani nafsi zao.

التفاسير:

external-link copy
22 : 56

وَحُورٌ عِينٞ

Na Mahurulaini, info

Na wanawake wenye macho ya vikombe,

التفاسير:

external-link copy
23 : 56

كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ

Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa. info

Kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa katika chaza, kwa usafi wao na urembo wao.

التفاسير:

external-link copy
24 : 56

جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda. info

Watapewa haya kuwa ni malipo kwa mambo mema waliyo kuwa wakiyatenda duniani.

التفاسير:

external-link copy
25 : 56

لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا تَأۡثِيمًا

Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi, info

Huko Peponi hawatasikia maneno yasiyo kuwa na maana, wala masimulizi ya kumtia dhambini mwenye kuyasikia.

التفاسير:

external-link copy
26 : 56

إِلَّا قِيلٗا سَلَٰمٗا سَلَٰمٗا

Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama. info

Ila watalo sikia ni kauli ya wao kwa wao: Tunakusalimuni kwa Salama.

التفاسير:

external-link copy
27 : 56

وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ

Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani? info

Na watu wa mkono wa kulia, hapana ajuaye nini malipo ya watu wa kuliani.

التفاسير:

external-link copy
28 : 56

فِي سِدۡرٖ مَّخۡضُودٖ

Katika mikunazi isiyo na miba, info

Katika miti ya mikunazi iliyo katwa miba yake,

التفاسير:

external-link copy
29 : 56

وَطَلۡحٖ مَّنضُودٖ

Na migomba iliyo pangiliwa, info

Na migomba iliyo pangika na ndizi zake zimepandana juu ya mikungu,

التفاسير:

external-link copy
30 : 56

وَظِلّٖ مَّمۡدُودٖ

Na kivuli kilicho tanda, info

Na kivuli kilicho enea wala hakiondoki,

التفاسير:

external-link copy
31 : 56

وَمَآءٖ مَّسۡكُوبٖ

Na maji yanayo miminika, info

Na maji yanayo miminika karibu yao popote wayatakapo,

التفاسير:

external-link copy
32 : 56

وَفَٰكِهَةٖ كَثِيرَةٖ

Na matunda mengi, info

Na matunda ya namna nyingi na kabila nyingi yasiyo tindikia wakati wowote,

التفاسير:

external-link copy
33 : 56

لَّا مَقۡطُوعَةٖ وَلَا مَمۡنُوعَةٖ

Hayatindikii wala hayakatazwi, info

Wala hazuiwiliwi ayatakayo,

التفاسير:

external-link copy
34 : 56

وَفُرُشٖ مَّرۡفُوعَةٍ

Na matandiko yaliyo nyanyuliwa. info

Na matandiko yaliyo nyanyuliwa ya starehe.

التفاسير:

external-link copy
35 : 56

إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءٗ

Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya, info

Hakika Sisi tulianza kuwaumba Mahurulaini mwanzo,

التفاسير:

external-link copy
36 : 56

فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا

Na tutawafanya vijana, info

Na tukawafanya kuwa ni vijana,

التفاسير:

external-link copy
37 : 56

عُرُبًا أَتۡرَابٗا

Wanapendana na waume zao, hirimu moja. info

Wenye kupendwa na waume zao, wenye umri ulio karibiana,

التفاسير:

external-link copy
38 : 56

لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ

Kwa ajili ya watu wa kuliani. info

Wa tayari kwa neema ya watu wa kuliani.

التفاسير:

external-link copy
39 : 56

ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ

Fungu kubwa katika wa mwanzo, info

Watu wa kulia ni wengi katika mataifu yaliyo kwisha tangulia,

التفاسير:

external-link copy
40 : 56

وَثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ

Na fungu kubwa katika wa mwisho. info

Na kikundi kikubwa katika umma wa Muhammad.

التفاسير:

external-link copy
41 : 56

وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ

Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni? info

Na watu wa kushoto, hapana anaye jua nini adhabu ya watu wa kushoto.

التفاسير:

external-link copy
42 : 56

فِي سَمُومٖ وَحَمِيمٖ

Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka, info

Watakuwa kwenye upepo umoto utakao wazunguka, unao penya katika tundu za mwili, na maji yaliyo chemshwa motoni wayanywe na wamiminiwe vichwani,

التفاسير:

external-link copy
43 : 56

وَظِلّٖ مِّن يَحۡمُومٖ

Na kivuli cha moshi mweusi, info

Na katika kivuli cha kiza cheusi cha moshi umoto,

التفاسير:

external-link copy
44 : 56

لَّا بَارِدٖ وَلَا كَرِيمٍ

Si cha kuburudisha wala kustarehesha. info

Hapana ubaridi wa kupunguza joto la hewa, wala huruma ya kuwaletea nafuu wanapo vuta pumzi.

التفاسير:

external-link copy
45 : 56

إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ

Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa. info

Hakika hao kabla ya haya walikuwa wamepita kiasi katika kustarehea neema za duniani, wamepumbaa hawataki kumt'ii Mwenyezi Mungu Mtukufu.

التفاسير:

external-link copy
46 : 56

وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ

Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa, info

Na walikuwa wameshikilia daima kufanya dhambi kubwa kabisa, kwani waliapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba kabisa Mwenyezi Mungu hatamfufua aliye kufa.

التفاسير:

external-link copy
47 : 56

وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ

Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa? info

Na walikuwa wakisema kwa kukanusha kurejea tena: Ati tutafufuliwa baada ya kwisha kufa, na baadhi ya miili yetu ikisha kuwa udongo na mengine mifupa iliyo chakaa? Ati sisi tutarudishwa tuwe hai mara ya pili?

التفاسير:

external-link copy
48 : 56

أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ

Au baba zetu wa zamani? info

Ati tutafufuliwa sisi na baba zetu wa zamani walio kwisha kuwa udongo ulio tapanyika na umepotea katika ardhi?

التفاسير:

external-link copy
49 : 56

قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ

Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho info

Waambie kwa kuwajibu kukanusha kwao: Hakika wa zamani na wa mwisho, ambao nyinyi ni katika jumla ya hao,

التفاسير:

external-link copy
50 : 56

لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ

Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu. info

Nyote mtakusanywa katika wakati wa siku malumu, na wala hamtoipita.

التفاسير:

external-link copy
51 : 56

ثُمَّ إِنَّكُمۡ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلۡمُكَذِّبُونَ

Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha, info

Kisha nyinyi, enyi mnao ipinga Njia ya Uwongofu, mnao kanusha kufufuliwa,

التفاسير:

external-link copy
52 : 56

لَأٓكِلُونَ مِن شَجَرٖ مِّن زَقُّومٖ

Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu. info

Bila ya shaka mtakula mti wa Zaqqumu katika Jahannamu, na mtayajaza matumbo yenu kwa shida ya njaa.

التفاسير:

external-link copy
53 : 56

فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ

Na kwa mti huo mtajaza matumbo. info

Na mtayajaza matumbo yenu kwa shida ya njaa.

التفاسير:

external-link copy
54 : 56

فَشَٰرِبُونَ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡحَمِيمِ

Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka. info

Mtakunywa juu ya mlicho kila maji yenye kutokota, yasiyo ondoa kiu,

التفاسير:

external-link copy
55 : 56

فَشَٰرِبُونَ شُرۡبَ ٱلۡهِيمِ

Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu. info

Na mtakunywa kwa wingi na pupa kama anavyo kunywa ngamia mwenye kiu kisicho katika kiu chake kwa maji.

التفاسير:

external-link copy
56 : 56

هَٰذَا نُزُلُهُمۡ يَوۡمَ ٱلدِّينِ

Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo. info

Hayo yaliyo tajwa ya mateso mbali mbali ndio karamu yao waliyo andaliwa kwa siku ya malipo.

التفاسير:

external-link copy
57 : 56

نَحۡنُ خَلَقۡنَٰكُمۡ فَلَوۡلَا تُصَدِّقُونَ

Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki? info

Sisi tulianza kukuumbeni mlipo kuwa si chochote, basi hebu hamkiri uweza wetu wa kukurejesheni tena baada ya kukufufueni?

التفاسير:

external-link copy
58 : 56

أَفَرَءَيۡتُم مَّا تُمۡنُونَ

Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza? info

Hamuangalii manii mnayo itia katika tumbo la uzazi?

التفاسير:

external-link copy
59 : 56

ءَأَنتُمۡ تَخۡلُقُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡخَٰلِقُونَ

Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji? info

Ni nyinyi ndio mwenye uweza juu yake na kuilea mpaka ikawa mtu, au ni Sisi ndio twenye makadara hayo?

التفاسير:

external-link copy
60 : 56

نَحۡنُ قَدَّرۡنَا بَيۡنَكُمُ ٱلۡمَوۡتَ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ

Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi info

Sisi tumekuhukumieni mauti, na tumeweka wakati makhsuri wa kufa kwenu. Na wala Sisi si wenye kushindwa kukubadilisheni sura zenu,

التفاسير:

external-link copy
61 : 56

عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمۡثَٰلَكُمۡ وَنُنشِئَكُمۡ فِي مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua. info

Na wala Sisi si wenye kushindwa kukubadilisheni sura zenu, na kuzileta nyengine, na tukakuumbeni katika umbo jengine na sura nyengine msiyo ijua.

التفاسير:

external-link copy
62 : 56

وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُولَىٰ فَلَوۡلَا تَذَكَّرُونَ

Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki? info

Bila ya shaka mmekwisha yakinika kuwa Mwenyezi Mungu alikuumbeni mara ya kwanza, basi je, hamkumbuki kwamba Mwenye kuweza hayo ni Mweza zaidi wa kufanya tena.

التفاسير:

external-link copy
63 : 56

أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَحۡرُثُونَ

Je! Mnaona makulima mnayo yapanda? info

Je! Hamuangalii mbegu mnayo ipanda katika ardhi?

التفاسير:

external-link copy
64 : 56

ءَأَنتُمۡ تَزۡرَعُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلزَّٰرِعُونَ

Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha? info

Ni nyinyi mnao ifanya imee au ni Sisi peke yetu ndio tunaifanya imee?

التفاسير:

external-link copy
65 : 56

لَوۡ نَشَآءُ لَجَعَلۡنَٰهُ حُطَٰمٗا فَظَلۡتُمۡ تَفَكَّهُونَ

Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu, info

Tungeli taka tungeli ifanya mimea hiyo iwe mabua na mapepe yaliyo katika katika kabla haijapevuka, mkawa mkistaajabu tu kwa uovu ulio isibu,

التفاسير:

external-link copy
66 : 56

إِنَّا لَمُغۡرَمُونَ

Mkisema: Hakika sisi tumegharimika; info

Huku mkisema: Hakika sisi tumepata khasara baada ya juhudi yetu.

التفاسير:

external-link copy
67 : 56

بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ

Bali sisi tumenyimwa. info

Bali sisi hatuna bahati, tumenyimwa riziki.

التفاسير:

external-link copy
68 : 56

أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلۡمَآءَ ٱلَّذِي تَشۡرَبُونَ

Je! Mnayaona maji mnayo yanywa? info

Je! Hamyaoni maji matamu mnayo yanywa?

التفاسير:

external-link copy
69 : 56

ءَأَنتُمۡ أَنزَلۡتُمُوهُ مِنَ ٱلۡمُزۡنِ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنزِلُونَ

Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha? info

Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni, au ni Sisi ndio Wenye kuyateremsha kuwa ni rehema juu yenu? Katika Kiarabu limetajwa neno Almuzni. Maana yake ni mawingu yanayo leta mvua. Na kitendo cha kunyesha mvua kinahitajia mambo yaliyo khusiana na hali ya hewa maalumu ambayo mwanaadamu hana mamlaka nayo, au kuyaleta kwa juhudi zake. Kwa mfano zinahitajiwa pepo zinazo kwenda kwa mkondo zilizo baridi juu ya nyengine zilizo za joto, au hali za kuondoka utulivu katika anga. Na watu wamejaribu kuinyesha mvua kwa mawingu yanayo pita kwa njia ya ufundi, lakini juhudi hizo mpaka sasa ni majaribio, na lilio thibiti katika sayansi ni kufuzu kwa majaribio hayo ni kudogo mno, na hata hivyo kunalazimu ziwepo hali maalumu za maumbile zinazo saidia.

التفاسير:

external-link copy
70 : 56

لَوۡ نَشَآءُ جَعَلۡنَٰهُ أُجَاجٗا فَلَوۡلَا تَشۡكُرُونَ

Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru? info

Lau tungeli taka tungeli yafanya hayo maji yakawa ya chumvi yasiyo nyweka. Basi mbona hamumshukuru Mwenyezi Mungu aliye yajaalia matamu yenye kunyweka?

التفاسير:

external-link copy
71 : 56

أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي تُورُونَ

Je! Mnauona moto mnao uwasha? info

Je! Hamuuoni moto huo mnao uasha?

التفاسير:

external-link copy
72 : 56

ءَأَنتُمۡ أَنشَأۡتُمۡ شَجَرَتَهَآ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنشِـُٔونَ

Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji? info

Ni nyinyi ndio mlio uotesha mti wake, na mkautia ndani ya huo mti moto, au ni Sisi ndio tulio uumbia hivyo, kadhaalika?

التفاسير:

external-link copy
73 : 56

نَحۡنُ جَعَلۡنَٰهَا تَذۡكِرَةٗ وَمَتَٰعٗا لِّلۡمُقۡوِينَ

Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani. info

Sisi tumeufanya huu moto uwe ni ukumbusho wa Moto wa Jahannamu mtapo uona, na uwe ni manufaa kwa wasafiri wa msitu na nyika, wakinafiika kwa kupikia chakula chao na kuotea moto wakati wa baridi.

التفاسير:

external-link copy
74 : 56

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ

Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu. info

Basi dumisha kusabihi, kutakasa, kwa kulidhukuru jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa, kwa kumtakasa na kumshukuru kwa neema hizi nzuri.

التفاسير:

external-link copy
75 : 56

۞ فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ

Basi naapa kwa maanguko ya nyota, info

Basi ninaapa kweli kwa maangukio ya nyota pale zinapo tua mwisho wa usiku wakati wa Tahajudi, ibada za usiku, na kustaghafiru.

التفاسير:

external-link copy
76 : 56

وَإِنَّهُۥ لَقَسَمٞ لَّوۡ تَعۡلَمُونَ عَظِيمٌ

Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua! info

Na hakika bila ya shaka hicho ni kiapo kikubwa chenye maana ya kufikia mbali, lau kuwa mnafikiri makusudio yake. Aya mbili hizi zinabainisha hadi ya umuhimu wa kiapo hichi kikubwa. Kwani nyota ni vitu vyenye kutoa mwangaza wenyewe, na nyota ya karibu mno kwetu sisi, nayo ni jua, ni kiasi ya masafa ya miaka 500 ya mwangaza. Na nyota ifuatayo kwa ukaribu iko mbali nasi kwa kiasi cha miaka 4 ya mwangaza takriban. Basi nguvu tunazo zitumia kutokana na jua ndizo zinazo tuwezesha kuishi. Lau kuwa umbali wa jua kutokana na ardhi ni duni ya hivyo au zaidi ya hivyo basi hapana shaka kuwa maisha yangeli kuwa taabu, bali ni muhali. Kadhaalika ukubwa wa nyota unakhitalifiana. Zipo nyota kubwa mno hata ukubwa wake unaweza kukusanya hii ardhi na jua juu ya umbali wao. Vipo vikundi vya nyota vinavyo itwa A'naqiid vinaogelea angani zikivuka Njia ya Maziwa The Milky Way mara kwa mara. Wakati wa kupita kwake zikasadifiana kukutana na kikundi cha jua na zikagongana basi hakika hapo itakuwa ndio maangamizo na kumalizika kwa kweli. Hata ikikaribia nyota moja katika nyota zitokazo kwenye jua basi hayo pia yataleta kuharibika mizani na kupelekea maangamizo na kumalizika ulimwengu. Kwa hivyo basi hakika Ishara za mazingatio na uweza wa Mwenyezi Mungu zinaonekana katika ulimwengu huu alio uumba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala na akaupanga.

التفاسير:

external-link copy
77 : 56

إِنَّهُۥ لَقُرۡءَانٞ كَرِيمٞ

Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu, info

Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani yenye manufaa mengi,

التفاسير:

external-link copy
78 : 56

فِي كِتَٰبٖ مَّكۡنُونٖ

Katika Kitabu kilicho hifadhiwa. info

Imo katika ubao ulio hifadhiwa Al-lauhu-lmahfudh, usio karibiwa na yeyote ila Malaika walio karibishwa kwa Mwenyezi Mungu. (Kwa watumiaji Computer wanaweza kukisia kuwa hiyo Al-lauhu-lmahfudh ni kama Disk iliyomo ndani ya Computer na haigusi mtu, na Misahafu tunayo iona, na kuisoma, ni kama yapigwayo chapa kutoka hiyo Disk.)

التفاسير:

external-link copy
79 : 56

لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُطَهَّرُونَ

Hapana akigusaye ila walio takaswa. info

Hawaigusi Qur'ani Tukufu ila walio t'ahirika na najisi na hadathi, vitengua udhu;

التفاسير:

external-link copy
80 : 56

تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. info

imeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe vyote.

التفاسير:

external-link copy
81 : 56

أَفَبِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ أَنتُم مُّدۡهِنُونَ

Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza? info

Je! Mnapuuza? Ni Qur'ani hii tukufu ndio nyinyi mnaidharau?

التفاسير:

external-link copy
82 : 56

وَتَجۡعَلُونَ رِزۡقَكُمۡ أَنَّكُمۡ تُكَذِّبُونَ

Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha? info

Na badala ya kuishukuru riziki yenu ndio mna ikadhibisha?

التفاسير:

external-link copy
83 : 56

فَلَوۡلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلۡحُلۡقُومَ

Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo, info

Basi je! Ikifika roho ya mmoja wenu kwenye mapitio ya pumzi,

التفاسير:

external-link copy
84 : 56

وَأَنتُمۡ حِينَئِذٖ تَنظُرُونَ

Na nyinyi wakati huo mnatazama! info

Na nyinyi inapo fika roho kwenye koo nanyi mnamwangalia huyo anaye kufa,

التفاسير:

external-link copy
85 : 56

وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُبۡصِرُونَ

Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi. info

Na Sisi tuko karibu zaidi kwa huyo aliye kabiliwa na mauti na tunaijua zaidi hali yake kuliko nyinyi, lakini nyinyi hamjui hayo wala hamhisi.

التفاسير:

external-link copy
86 : 56

فَلَوۡلَآ إِن كُنتُمۡ غَيۡرَ مَدِينِينَ

Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu, info

Basi je! Ikiwa nyinyi si wenye kunyenyekea kwa Ungu wetu,

التفاسير:

external-link copy
87 : 56

تَرۡجِعُونَهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli? info

Mrudishieni roho yake huyo aliye kabiliwa na mauti ikiwa nyinyi mwasema kweli kwamba nyinyi mnazo nguvu na hamshindwi.

التفاسير:

external-link copy
88 : 56

فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ

Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa, info

Ama akiwa huyo aliye kabiliwa na mauti ni katika walio tangulia walio karibishwa ,

التفاسير:

external-link copy
89 : 56

فَرَوۡحٞ وَرَيۡحَانٞ وَجَنَّتُ نَعِيمٖ

Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema. info

Basi mwisho wake ni raha, na rehema, na riziki njema, na Pepo yenye neema.

التفاسير:

external-link copy
90 : 56

وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ

Na akiwa katika watu wa upande wa kulia, info

Ama akiwa katika watu wa mkono wa kulia,

التفاسير:

external-link copy
91 : 56

فَسَلَٰمٞ لَّكَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ

Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia. info

Basi ataambiwa kwa maamkio na takrima: Unapewa salamu kutokana na watu wa kuliani.

التفاسير:

external-link copy
92 : 56

وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ

Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu, info

Na ama akiwa ni katika wa kushoto, wanao kanusha, walio wapotovu,

التفاسير:

external-link copy
93 : 56

فَنُزُلٞ مِّنۡ حَمِيمٖ

Basi karamu yake ni maji yanayo chemka, info

Basi atakirimiwa maji ya moto hadi ya kuchemka,

التفاسير:

external-link copy
94 : 56

وَتَصۡلِيَةُ جَحِيمٍ

Na kutiwa Motoni. info

Na kubabuliwa na moto wa mwisho wa ukali.

التفاسير:

external-link copy
95 : 56

إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلۡيَقِينِ

Hakika hii ndiyo haki yenye yakini. info

Hakika haya yaliyo tajwa katika Sura hii tukufu bila ya shaka ni kiini cha yakini iliyo thibiti, isiyo ingiliwa na shaka.

التفاسير:

external-link copy
96 : 56

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ

Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa. info

Tanguliza tasbihi kwa kumdhukuru Mola wako Mlezi aliye Mkubwa, kwa kumtakasa na kumshukuru kwa neema zake.

التفاسير: