വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - റുവ്വാദ് തർജമ സെൻ്റർ

പേജ് നമ്പർ:close

external-link copy
146 : 2

ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَعۡرِفُونَهُۥ كَمَا يَعۡرِفُونَ أَبۡنَآءَهُمۡۖ وَإِنَّ فَرِيقٗا مِّنۡهُمۡ لَيَكۡتُمُونَ ٱلۡحَقَّ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ

Wale tuliowapa Kitabu, wanayajua haya kama wanavyowajua watoto wao. Na kuna kikundi katika wao huificha haki na hali wanajua.[1] info

[1] Wao kwa hakika walikuwa wanajua katika sifa zake kabla ya kumuona, ambazo ziliingiliana na yeye mwenyewe walipomuona. (Tafsir Ibn Al-Qayyim)

التفاسير:

external-link copy
147 : 2

ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ

Haki inatoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe kabisa miongoni mwa wenye shaka. info
التفاسير:

external-link copy
148 : 2

وَلِكُلّٖ وِجۡهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَاۖ فَٱسۡتَبِقُواْ ٱلۡخَيۡرَٰتِۚ أَيۡنَ مَا تَكُونُواْ يَأۡتِ بِكُمُ ٱللَّهُ جَمِيعًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Na kila mmoja anao mwelekeo anaoelekea. Basi shindanieni mema. Popote mlipo, Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamoja. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. info
التفاسير:

external-link copy
149 : 2

وَمِنۡ حَيۡثُ خَرَجۡتَ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۖ وَإِنَّهُۥ لَلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Na kokote uendako, uelekeze uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na hiyo kwa hakika ndiyo haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayoyatenda. info
التفاسير:

external-link copy
150 : 2

وَمِنۡ حَيۡثُ خَرَجۡتَ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَحَيۡثُ مَا كُنتُمۡ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ شَطۡرَهُۥ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيۡكُمۡ حُجَّةٌ إِلَّا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِي وَلِأُتِمَّ نِعۡمَتِي عَلَيۡكُمۡ وَلَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ

Na kokote uendako, uelekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo, zielekezeni nyuso zenu upande wake, ili watu wasiwe na hoja juu yenu; isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Basi, msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi. Na ili niwatimizie neema yangu, na ili mpate kuongoka info
التفاسير:

external-link copy
151 : 2

كَمَآ أَرۡسَلۡنَا فِيكُمۡ رَسُولٗا مِّنكُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِنَا وَيُزَكِّيكُمۡ وَيُعَلِّمُكُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمۡ تَكُونُواْ تَعۡلَمُونَ

Kama tulivyomtuma Mtume kwenu anayetokana na nyinyi, anawasomea Aya zetu na kuwatakasa na kuwafundisha Kitabu na hekima, na anawafundisha ambayo hamkuwa mnayajua. info
التفاسير:

external-link copy
152 : 2

فَٱذۡكُرُونِيٓ أَذۡكُرۡكُمۡ وَٱشۡكُرُواْ لِي وَلَا تَكۡفُرُونِ

Basi nikumbukeni, nitawakumbuka. Na nishukuruni, wala msinikufuru. info
التفاسير:

external-link copy
153 : 2

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱلصَّبۡرِ وَٱلصَّلَوٰةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na Swala. Hakika, Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri. info
التفاسير: