വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി പരിഭാഷ - അലി മുഹ്സിൻ അൽബർവാനി

പേജ് നമ്പർ:close

external-link copy
43 : 23

مَا تَسۡبِقُ مِنۡ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ

Hapana umma uwezao kutanguliza ajali yake wala kuikawiza. info

Kila umma una zama zake maalumu, hazitangulii wala hazikawii.

التفاسير:

external-link copy
44 : 23

ثُمَّ أَرۡسَلۡنَا رُسُلَنَا تَتۡرَاۖ كُلَّ مَا جَآءَ أُمَّةٗ رَّسُولُهَا كَذَّبُوهُۖ فَأَتۡبَعۡنَا بَعۡضَهُم بَعۡضٗا وَجَعَلۡنَٰهُمۡ أَحَادِيثَۚ فَبُعۡدٗا لِّقَوۡمٖ لَّا يُؤۡمِنُونَ

Kisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipo wafikia Mtume wao walimkanusha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya ni hadithi za kusimuliwa. Wakapotelea mbali watu wasio amini. info

Kisha tukawatuma Mitume wetu wakifuatana, kila mmoja kwa kaumu yake. Kila akija Mtume kwa kaumu yake waliukadhibisha wito wake. Nasi tukawateketeza mfululizo, na tukazifanya khabari zao ni hadithi za watu kusimuliana na kuzistaajabia. Basi hao kaumu wasio isadiki Haki wala hawaifuati wametengeka mbali na rehema, na wamehiliki.

التفاسير:

external-link copy
45 : 23

ثُمَّ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ وَأَخَاهُ هَٰرُونَ بِـَٔايَٰتِنَا وَسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٍ

Kisha tukamtuma Musa na nduguye, Haaruni, pamoja na ishara zetu na hoja zilizo wazi. info

Kisha tukamtuma Musa na nduguye, Haaruni, tukawapa dalili za kukata kuthibitisha ukweli wa ujumbe wao, na hoja wazi yenye kudhihirisha kuwa wao ni kweli wametumwa kutoka kwangu.

التفاسير:

external-link copy
46 : 23

إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمًا عَالِينَ

Kumwendea Firauni na wakuu wake. Lakini walijivuna, nao walikuwa watu majeuri. info

Tuliwatuma wawili hao kwa Firauni na kaumu yake. Wakakataa kuamini kwa ajili ya takaburi, na wao ni watu walio kuwa wakisifika kwa kiburi, na majivuno, na ujeuri.

التفاسير:

external-link copy
47 : 23

فَقَالُوٓاْ أَنُؤۡمِنُ لِبَشَرَيۡنِ مِثۡلِنَا وَقَوۡمُهُمَا لَنَا عَٰبِدُونَ

Wakasema: Je, tuwaamini wanaadamu wawili hawa kama sisi, na ambao watu wao ni watumwa wetu? info

Wakasema kwa mastaajabu na kukanya: Je, tuuamini wito wa watu wawili walio ni wanaadamu kama sisi, na tena watu wao hawa Wana wa Israili ni wenye kutunyenyekea sisi na kutut'ii kama ni watumwa?

التفاسير:

external-link copy
48 : 23

فَكَذَّبُوهُمَا فَكَانُواْ مِنَ ٱلۡمُهۡلَكِينَ

Basi wakawakanusha, na wakawa miongoni mwa walio angamizwa. info

Basi waliwafanya waongo katika huo wito wao, na wakawa wenye kuhiliki kwa kuzamishwa.

التفاسير:

external-link copy
49 : 23

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ لَعَلَّهُمۡ يَهۡتَدُونَ

Na hakika tulimpa Musa Kitabu ili wapate kuongoka. info

Na hakika tulimfunulia Musa Taurati apate kuwaongoa watu wake kwa yaliyomo ndani yake ya uwongozi kwendea hukumu na njia za mafanikio.

التفاسير:

external-link copy
50 : 23

وَجَعَلۡنَا ٱبۡنَ مَرۡيَمَ وَأُمَّهُۥٓ ءَايَةٗ وَءَاوَيۡنَٰهُمَآ إِلَىٰ رَبۡوَةٖ ذَاتِ قَرَارٖ وَمَعِينٖ

Na tukamfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ni Ishara, na tukawapa makimbilio kwenda mahali palipo inuka penye utulivu na chemchem za maji. info

Na tumemjaalia Isa bin Maryamu na mama yake, kwa vile kuchukua mimba bila ya kuingiliwa na mtu, na kuzaliwa yeye Isa bila ya baba, kuwa dalili ya kukata ya uwezo wetu wenye kushinda. Na tukamweka Maryamu pahala pa kukaa penye ardhi iliyo nyanyuka na kukunjuka panapo faa kukaa, na pana maji mengi. Na hayo ndiyo yanayo wezesha maisha ya starehe.

التفاسير:

external-link copy
51 : 23

يَٰٓأَيُّهَا ٱلرُّسُلُ كُلُواْ مِنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَٱعۡمَلُواْ صَٰلِحًاۖ إِنِّي بِمَا تَعۡمَلُونَ عَلِيمٞ

Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayo yatenda. info

Tumewaambia Mitume wawafikishie watu wao: Kuleni vyakula vya kila namna vya halali na vizuri, na stareheni na ishukuruni neema yangu kwa vitendo vyema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa myatendayo na nitakulipeni kwayo.

التفاسير:

external-link copy
52 : 23

وَإِنَّ هَٰذِهِۦٓ أُمَّتُكُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَأَنَا۠ رَبُّكُمۡ فَٱتَّقُونِ

Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi. info

Na tukawaambia wawafikishie watu wao: Hakika hii Dini niliyo kutumeni muifikishe ni Dini moja kwa mintarafu ya Imani na misingi ya sharia. Na hakika nyinyi ni umma mmoja katika vizazi vyote. Miongoni mwao wapo walio ongoka, na wapo walio potoka. Na Mimi ndiye Mola wenu Mlezi niliye kuamrisheni muifuate, basi iogopeni adhabu yangu pindi mkiasi.

التفاسير:

external-link copy
53 : 23

فَتَقَطَّعُوٓاْ أَمۡرَهُم بَيۡنَهُمۡ زُبُرٗاۖ كُلُّ حِزۡبِۭ بِمَا لَدَيۡهِمۡ فَرِحُونَ

Lakini walikatiana jambo lao mapande mbali mbali. Kila kundi likifurahia kwa waliyo nayo. info

Lakini watu walilikata kata hili jambo la Dini yao. Wapo kati yao walio ongoka, na wapo walio potoka ambao wakafuata matamanio yao, wakafarikiana kwa sababu hiyo wakawa makundi mbali mbali yenye kufanyiana uadui. Kila kikundi kinafurahi kwa walio nayo, kwa kudhania kuwa wao tu ndio walio sibu.

التفاسير:

external-link copy
54 : 23

فَذَرۡهُمۡ فِي غَمۡرَتِهِمۡ حَتَّىٰ حِينٍ

Basi waache katika ghafla yao kwa muda. info

Basi, ewe Muhammad, waachilie mbali makafiri na ujinga wao na kughafilika kwao, maadamu wewe umekwisha wanasihi, mpaka Mwenyezi Mungu awahukumie adhabu baadae.

التفاسير:

external-link copy
55 : 23

أَيَحۡسَبُونَ أَنَّمَا نُمِدُّهُم بِهِۦ مِن مَّالٖ وَبَنِينَ

Je! Wanadhani ya kuwa kwa vile tunavyo wapa mali na watoto info

Hivyo hawa maasi wanadhani ya kwamba pale Sisi tunapo wawacha wakistarehe na mali na watoto tulio wapa

التفاسير:

external-link copy
56 : 23

نُسَارِعُ لَهُمۡ فِي ٱلۡخَيۡرَٰتِۚ بَل لَّا يَشۡعُرُونَ

Ndio tunawahimizia kheri? Lakini wenyewe hawatambui. info

Ndio basi Sisi tumekuwa radhi nao, na kheri zikawamiminikia mbio mbio na kwa wingi? Hao ni kama wanyama, hawatambui, kwa kuwa hawazitumii akili zao. Mimi si radhi nao. Na hizi neema ni kuwapururia tu, kuwapa muda.

التفاسير:

external-link copy
57 : 23

إِنَّ ٱلَّذِينَ هُم مِّنۡ خَشۡيَةِ رَبِّهِم مُّشۡفِقُونَ

Kwa hakika hao ambao kwa kumwogopa Mola wao Mlezi wananyenyekea, info

Hakika wale ambao humkhofu Mwenyezi Mungu na humwogopa, na zimejaa ndani yao khofu ya Mwenyewe Subhanahu,

التفاسير:

external-link copy
58 : 23

وَٱلَّذِينَ هُم بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ يُؤۡمِنُونَ

Na wale ambao Ishara za Mola wao Mlezi wanaziamini, info

Na wale ambao wanaziamini Ishara za Mola wao Mlezi ziliomo ulimwenguni na zinazo somwa katika Kitabu kilicho teremshwa,

التفاسير:

external-link copy
59 : 23

وَٱلَّذِينَ هُم بِرَبِّهِمۡ لَا يُشۡرِكُونَ

Na wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi, info

Na wale ambao hawamshirikishi Mwenyezi Mungu na yeyote,

التفاسير: