വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി പരിഭാഷ - അലി മുഹ്സിൻ അൽബർവാനി

പേജ് നമ്പർ:close

external-link copy
28 : 23

فَإِذَا ٱسۡتَوَيۡتَ أَنتَ وَمَن مَّعَكَ عَلَى ٱلۡفُلۡكِ فَقُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي نَجَّىٰنَا مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

Basi utakapo tulia wewe na walio pamoja nawe humo marikebuni, sema: Alhamdulillahi Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, aliye tuokoa na watu madhaalimu! info

Na ukisha panda na ukatua wewe na walio pamoja nawe katika jahazi hiyo basi sema kwa kumshukuru Mola wako Mlezi: Alhamdulillahi! Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliye tuokoa na shari ya watu makafiri walio asi.

التفاسير:

external-link copy
29 : 23

وَقُل رَّبِّ أَنزِلۡنِي مُنزَلٗا مُّبَارَكٗا وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلۡمُنزِلِينَ

Na sema: Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora wa wateremshaji. info

Na useme: Ewe Mola Mlezi! Nijaalie nishuke mashukio yenye baraka, pahala pazuri pa kukaa wakati wa kuteremka nchi kavu. Na unitunukie amani hapo. Kwani ni Wewe tu peke yako unaye weza kututeremsha pahala pa kheri na amani na salama.

التفاسير:

external-link copy
30 : 23

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ وَإِن كُنَّا لَمُبۡتَلِينَ

Hakika katika hayo yapo mazingatio. Na kwa yakini Sisi ni wenye kuwafanyia mtihani. info

Hakika katika kisa hichi yapo mazingatio na mawaidha mengi. Na hakika Sisi tunawajaribu (tunawapa mitihani) waja wetu kwa kheri na shari. Na ndani ya nafsi zao wana utayarisho wa yote hayo.

التفاسير:

external-link copy
31 : 23

ثُمَّ أَنشَأۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِمۡ قَرۡنًا ءَاخَرِينَ

Kisha baada yao, tukanzisha kizazi kingine. info

Tena baada ya kaumu ya Nuhu tukaumba namna ya watu wengine, na wao ni A'adi.

التفاسير:

external-link copy
32 : 23

فَأَرۡسَلۡنَا فِيهِمۡ رَسُولٗا مِّنۡهُمۡ أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ

Tukawapelekea Mtume miongoni mwao, kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu asiye kuwa Yeye. Jee, hamwogopi? info

Tukawapelekea Huud. Naye ni katika wao. Tukawaambia kwa ulimi wake: Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake. Kwani nyinyi hamna Mungu anaye stahiki kuabudiwa asiye kuwa Yeye. Ni Yeye peke yake anaye faa mumwogope. Basi, jee mmeikhofu adhabu yake mkimuasi?

التفاسير:

external-link copy
33 : 23

وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِلِقَآءِ ٱلۡأٓخِرَةِ وَأَتۡرَفۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا مَا هَٰذَآ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُكُمۡ يَأۡكُلُ مِمَّا تَأۡكُلُونَ مِنۡهُ وَيَشۡرَبُ مِمَّا تَشۡرَبُونَ

Na wakubwa katika watu wake walioukufuru, na wakakanusha mkutano wa Akhera, na tukawadekeza kwa starehe, katika maisha ya dunia, walisem: Huyu si chochote ila ni mwanadamu kama nyinyi, anakula mlacho, na anakunywa mnywacho. info

Na wakubwa katika kaumu yake walio kufuru na kukadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu na mambo ya Akheria ya hisabu na malipo, na tukawapa sehemu kubwa ya starehe na neema, wakasema kwa kukanusha wito wake, na kuwazuia watu wasimfuate: Hapana khitilafu yo yote baina ya Huud na nyinyi. Anakula chakula hicho hicho mnacho kila nyinyi. Na anakunywa vinywaji hivyo hivyo mnavyo vinywa nyinyi. Mfano wa huyu hawezi kuwa Mtume, kwa sababu hana sifa msizo kuwa nazo nyinyi.

التفاسير:

external-link copy
34 : 23

وَلَئِنۡ أَطَعۡتُم بَشَرٗا مِّثۡلَكُمۡ إِنَّكُمۡ إِذٗا لَّخَٰسِرُونَ

Na nyinyi mkimt'ii mtu kama nyinyi basi hakika mtakuwa khasarani. info

Na wakawahadharisha kwa nguvu na mkazo, wakiwaambia: Mkimt'ii mtu aliye kama nyinyi kwa utu wake, basi nyinyi hakika mtakuwa mmekhasiri kwa kuwa hamtapata manufaa yo yote mkimfuata.

التفاسير:

external-link copy
35 : 23

أَيَعِدُكُمۡ أَنَّكُمۡ إِذَا مِتُّمۡ وَكُنتُمۡ تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَنَّكُم مُّخۡرَجُونَ

Hivyo anakuahidini ati ya kwamba mtakapo kufa na mkawa udongo na mifupa kuwa mtatolewa? info

Wakawaambia pia katika kukanya kufufuliwa: Hivyo Huud anakuahidini kuwa mtafufuliwa kutoka makaburini kwenu baada ya kwisha kufa kwenu, na mkawa udongo na mafupa yasiyo kuwa na nyama na mishipa?

التفاسير:

external-link copy
36 : 23

۞ هَيۡهَاتَ هَيۡهَاتَ لِمَا تُوعَدُونَ

Hayawi! Hayawi hayo mnayo ahidiwa. info

Hayo anayo kuahidini ni ya mbali mno, wala hayatakuwa abadan.

التفاسير:

external-link copy
37 : 23

إِنۡ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا ٱلدُّنۡيَا نَمُوتُ وَنَحۡيَا وَمَا نَحۡنُ بِمَبۡعُوثِينَ

Hapana ila uhai wetu wa duniani tu, tunakufa na kuishi basi. Wala sisi hatutafufuliwa. info

Hapana uhai ila mmoja tu. Nao ndio huu uhai wa duniani, ambao tunauona una mauti na uhai unao tupitia. Kinacho zaliwa kinazaliwa, na kilicho hai kinakufa. Wala hatutofufuliwa baada ya kwisha kufa kabisa.

التفاسير:

external-link copy
38 : 23

إِنۡ هُوَ إِلَّا رَجُلٌ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبٗا وَمَا نَحۡنُ لَهُۥ بِمُؤۡمِنِينَ

Huyu si lolote ila ni mtu anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, wala sisi sio wa kumuamini. info

Huyu si chochote ila ni mtu aliye mzulia Mwenyezi Mungu, na akadai kwamba Mwenyezi Mungu kamtuma yeye. Na amesema uwongo katika hayo anayo tuitia. Wala hatutomsadiki abadan. *

التفاسير:

external-link copy
39 : 23

قَالَ رَبِّ ٱنصُرۡنِي بِمَا كَذَّبُونِ

Akasema: Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa sababu wananikanusha. info

Huud akasema baada ya kwisha kata tamaa kuamini kwao: Ewe Mola wangu Mlezi! Ninusuru na uwatie adabu, kwa sababu ya kuukadhibisha wito wangu.

التفاسير:

external-link copy
40 : 23

قَالَ عَمَّا قَلِيلٖ لَّيُصۡبِحُنَّ نَٰدِمِينَ

(Mwenyezi Mungu) akasema: Baada ya muda mchache watakuwa wenye kujuta. info

Mwenyezi Mungu akamwambia Huud kuzidi kutilia nguvu ahadi yake: Baada ya muda mchache watakuja juta, kwa waliyo yafanya, itapo wateremkia adhabu.

التفاسير:

external-link copy
41 : 23

فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ بِٱلۡحَقِّ فَجَعَلۡنَٰهُمۡ غُثَآءٗۚ فَبُعۡدٗا لِّلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

Basi ukawanyakua ukelele kwa haki, na tukawafanya kama takataka zinazo elea juu ya maji. Ikapotelea mbali kaumu ya madhaalimu! info

Ukawachukua ukelele mkali ulio wahilikisha kama walivyo stahiki. Tukawafanya kwa udhalili na udhaifu kama vijiti na majani ya miti yanayo chukuliwa na maji ya mvua. Na huko ni kuteketea na kupotelea mbali na rehema kwa madhaalimu kwa ukafiri wao na uasi wao.

التفاسير:

external-link copy
42 : 23

ثُمَّ أَنشَأۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِمۡ قُرُونًا ءَاخَرِينَ

Kisha tukaleta baada yao vizazi vingine. info

Kisha baada yao tukawaumba kaumu nyengine wasio kuwa wao, kama kaumu ya Swaleh na ya Luut'i na ya Shuaib.

التفاسير: