ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
34 : 10

قُلۡ هَلۡ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۚ قُلِ ٱللَّهُ يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ

Sema: Je, yupo katika washirika wenu mwenye kuanzisha kuumba viumbe, kisha akavirejesha? Sema: Mwenyezi Mungu anaazisha kuumba viumbe, kisha anavirejesha. Basi ni vipi mnadanganywa? info
التفاسير:

external-link copy
35 : 10

قُلۡ هَلۡ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلۡحَقِّۚ قُلِ ٱللَّهُ يَهۡدِي لِلۡحَقِّۗ أَفَمَن يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلۡحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّيٓ إِلَّآ أَن يُهۡدَىٰۖ فَمَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ

Sema, "Je, yupo yeyote katika washirika wenu mwenye kuongoa kwenye haki?" Sema, "Mwenyezi Mungu anaongoa kwenya haki." Basi, je, yule anayeongoa kwenye haki anastahiki zaidi kufuatwa au yule asiyeongoka isipokuwa akiongozwa? Basi nyinyi mna nini, mnahukumu namna gani? info
التفاسير:

external-link copy
36 : 10

وَمَا يَتَّبِعُ أَكۡثَرُهُمۡ إِلَّا ظَنًّاۚ إِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا يَفۡعَلُونَ

Na wengi wao hawafuati isipokuwa dhana tu. Na hakika, dhana haifai kitu mbele ya haki. Hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi yote wanayoyatenda. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 10

وَمَا كَانَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانُ أَن يُفۡتَرَىٰ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا رَيۡبَ فِيهِ مِن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na haikuwa Qur-ani hii ni ya kuzuliwa kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini ni usadikisho wa yale yaliyoitangulia, na ni maelezo ya kina ya Kitabu kisicho na shaka yoyote ndani yake, kutoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 10

أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ فَأۡتُواْ بِسُورَةٖ مِّثۡلِهِۦ وَٱدۡعُواْ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Ama ndiyo wanasema ameizua? Sema, "Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite muwawezao, kando na Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli." info
التفاسير:

external-link copy
39 : 10

بَلۡ كَذَّبُواْ بِمَا لَمۡ يُحِيطُواْ بِعِلۡمِهِۦ وَلَمَّا يَأۡتِهِمۡ تَأۡوِيلُهُۥۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلظَّٰلِمِينَ

Bali waliyakadhibisha yale wasiyoyaelewa elimu yake vyema kabla hayajawajia maelezo yake. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Basi angalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa madhalimu hao. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 10

وَمِنۡهُم مَّن يُؤۡمِنُ بِهِۦ وَمِنۡهُم مَّن لَّا يُؤۡمِنُ بِهِۦۚ وَرَبُّكَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُفۡسِدِينَ

Na miongoni mwao kuna anayeiamini, na miongoni mwao kuna asiyeiamini. Na Mola wako Mlezi ndiye anawajua vyema waharibifu. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 10

وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمۡ عَمَلُكُمۡۖ أَنتُم بَرِيٓـُٔونَ مِمَّآ أَعۡمَلُ وَأَنَا۠ بَرِيٓءٞ مِّمَّا تَعۡمَلُونَ

Na wakikukadhibisha, basi sema, "Mimi nina matendo yangu, na nyinyi mna matendo yenu. Nyinyi mko mbali sana na yale ninayoyatenda, nami niko mbali sana na mnayoyatenda." info
التفاسير:

external-link copy
42 : 10

وَمِنۡهُم مَّن يَسۡتَمِعُونَ إِلَيۡكَۚ أَفَأَنتَ تُسۡمِعُ ٱلصُّمَّ وَلَوۡ كَانُواْ لَا يَعۡقِلُونَ

Na miongoni mwao kuna wale wanaokusikiliza. Je, wewe unaweza wasikizisha viziwi hata kama hawatumii akili? info
التفاسير: