ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
71 : 10

۞ وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ نُوحٍ إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيۡكُم مَّقَامِي وَتَذۡكِيرِي بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَعَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡتُ فَأَجۡمِعُوٓاْ أَمۡرَكُمۡ وَشُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ لَا يَكُنۡ أَمۡرُكُمۡ عَلَيۡكُمۡ غُمَّةٗ ثُمَّ ٱقۡضُوٓاْ إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ

Na wasomee habari za Nuhu alipowaambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Ikiwa ni kukubwa kwenu kukaa kwangu nanyi na kuwakumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, nyinyi likusanyeni jambo lenu pamoja na washirika wenu, kisha jambo lenu hilo lisiwe la kufichikana kwenu, kisha nihukumuni, wala msinipe muhula. info
التفاسير:

external-link copy
72 : 10

فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَمَا سَأَلۡتُكُم مِّنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِۖ وَأُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ

Na mkigeuka, basi mimi sikuwaomba ujira wowote. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waislamu. info
التفاسير:

external-link copy
73 : 10

فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَجَعَلۡنَٰهُمۡ خَلَٰٓئِفَ وَأَغۡرَقۡنَا ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُنذَرِينَ

Lakini wakamkadhibisha. Kwa hivyo tukamwokoa, pamoja na wale waliokuwa naye, katika jahazi. Na tukawafanya wao ndio waliobakia, na tukawazamisha wale waliozikadhibisha Ishara zetu. Basi angalia vipi ulikuwa mwisho wa walioonywa. info
التفاسير:

external-link copy
74 : 10

ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِۦ رُسُلًا إِلَىٰ قَوۡمِهِمۡ فَجَآءُوهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْ بِمَا كَذَّبُواْ بِهِۦ مِن قَبۡلُۚ كَذَٰلِكَ نَطۡبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلۡمُعۡتَدِينَ

Kisha baada yake tukawatuma Mitume kwa kaumu zao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizo wazi. Lakini hawakuwa wenye kuyaamini wale waliyoyakanusha kabla yake. Hivyo ndivyo tunavyoziziba nyoyo za wavukao mipaka. info
التفاسير:

external-link copy
75 : 10

ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ وَهَٰرُونَ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ بِـَٔايَٰتِنَا فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمٗا مُّجۡرِمِينَ

Kisha baada yao tukamtuma Musa na Haruni kwa Firauni na waheshimiwa wake, kwa Ishara zetu. Wakatakabari, na wakawa kaumu wahalifu. info
التفاسير:

external-link copy
76 : 10

فَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلۡحَقُّ مِنۡ عِندِنَا قَالُوٓاْ إِنَّ هَٰذَا لَسِحۡرٞ مُّبِينٞ

Basi ilipowajia haki kutoka kwetu, walisema: Hakika huu ni uchawi ulio dhahiri. info
التفاسير:

external-link copy
77 : 10

قَالَ مُوسَىٰٓ أَتَقُولُونَ لِلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَكُمۡۖ أَسِحۡرٌ هَٰذَا وَلَا يُفۡلِحُ ٱلسَّٰحِرُونَ

Akasema Musa, "Je, mnasema hivi juu ya haki ilipowajia? Je, huu ni uchawi? Na wachawi hawafanikiwi!" info
التفاسير:

external-link copy
78 : 10

قَالُوٓاْ أَجِئۡتَنَا لِتَلۡفِتَنَا عَمَّا وَجَدۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا ٱلۡكِبۡرِيَآءُ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا نَحۡنُ لَكُمَا بِمُؤۡمِنِينَ

Wakasema: Je, umetujia ili utuachishe tuliyowakuta nayo baba zetu, na mpate nyinyi wawili ukubwa katika ardhi? Wala sisi hatuwaamini nyinyi. info
التفاسير: