ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
21 : 10

وَإِذَآ أَذَقۡنَا ٱلنَّاسَ رَحۡمَةٗ مِّنۢ بَعۡدِ ضَرَّآءَ مَسَّتۡهُمۡ إِذَا لَهُم مَّكۡرٞ فِيٓ ءَايَاتِنَاۚ قُلِ ٱللَّهُ أَسۡرَعُ مَكۡرًاۚ إِنَّ رُسُلَنَا يَكۡتُبُونَ مَا تَمۡكُرُونَ

Na tunapowaonjesha watu rehema baada ya shida iliyowagusa, tazama, wanafanya njama katika Ishara zetu. Sema, “Mwenyezi Mungu ni Mwepesi zaidi wa kupanga njama. Hakika wajumbe wetu wanayaandika hayo mnayoyapangia njama.” info
التفاسير:

external-link copy
22 : 10

هُوَ ٱلَّذِي يُسَيِّرُكُمۡ فِي ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا كُنتُمۡ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَجَرَيۡنَ بِهِم بِرِيحٖ طَيِّبَةٖ وَفَرِحُواْ بِهَا جَآءَتۡهَا رِيحٌ عَاصِفٞ وَجَآءَهُمُ ٱلۡمَوۡجُ مِن كُلِّ مَكَانٖ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُمۡ أُحِيطَ بِهِمۡ دَعَوُاْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ لَئِنۡ أَنجَيۡتَنَا مِنۡ هَٰذِهِۦ لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّٰكِرِينَ

Yeye ndiye anayewaendesha katika nchi kavu na baharini. Mpaka mnapokuwa katika majahazi na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri na wakaufurahia, upepo mkali ukayajia, na yakawajia mawimbi kutoka kila mahali, na wakaona kwamba wameshazungukwa, basi hapo wanamwomba Mwenyezi Mungu kwa kumpwekeshea yeye tu dini, “Ukituokoa na haya, bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.” info
التفاسير:

external-link copy
23 : 10

فَلَمَّآ أَنجَىٰهُمۡ إِذَا هُمۡ يَبۡغُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّۗ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّمَا بَغۡيُكُمۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمۖ مَّتَٰعَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ ثُمَّ إِلَيۡنَا مَرۡجِعُكُمۡ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Lakini anapowaokoa, tazama, wanafanya jeuri tena katika ardhi bila ya haki. Enyi watu! Hakika jeuri zenu zitawadhuru nyinyi wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 10

إِنَّمَا مَثَلُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا كَمَآءٍ أَنزَلۡنَٰهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ فَٱخۡتَلَطَ بِهِۦ نَبَاتُ ٱلۡأَرۡضِ مِمَّا يَأۡكُلُ ٱلنَّاسُ وَٱلۡأَنۡعَٰمُ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَخَذَتِ ٱلۡأَرۡضُ زُخۡرُفَهَا وَٱزَّيَّنَتۡ وَظَنَّ أَهۡلُهَآ أَنَّهُمۡ قَٰدِرُونَ عَلَيۡهَآ أَتَىٰهَآ أَمۡرُنَا لَيۡلًا أَوۡ نَهَارٗا فَجَعَلۡنَٰهَا حَصِيدٗا كَأَن لَّمۡ تَغۡنَ بِٱلۡأَمۡسِۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ

Hakika mfano wa uhai wa dunia hii ni kama maji tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha mimea ya ardhi ikachanganyika nayo miongoni mwa vile wanayvovila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipokamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani kwamba wameshaiweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, kwa hivyo tukaifanya kama iliyofyekwa, kama kwamba haikuwapo jana. Hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara zetu kwa kaumu wanaotafakari. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 10

وَٱللَّهُ يَدۡعُوٓاْ إِلَىٰ دَارِ ٱلسَّلَٰمِ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Na Mwenyezi Mungu anaita kwenye Nyumba ya amani, na anamwongoa amtakaye kwenye Njia iliyonyooka. info
التفاسير: