ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
43 : 10

وَمِنۡهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيۡكَۚ أَفَأَنتَ تَهۡدِي ٱلۡعُمۡيَ وَلَوۡ كَانُواْ لَا يُبۡصِرُونَ

Na wapo miongoni mwao wanao kutazama. Je, wewe utawaongoa vipofu ingawa hawaoni? info

Na wengine wapo wanao kutazama na wanalifikiria jambo lako, na wanaona dalili zilizo wazi za Unabii wako. Lakini bado hawaongoki wakafuata. Mfano wa hayo ni mfano wa kipofu, nawe huwezi kuwaongoa hao vipofu. Upofu wa macho ni kama upofu wa moyo. Wote hawana uwongofu! Kipofu haioni njia kwa kuhisi, na mpotovu haongoki kwa maana.

التفاسير:

external-link copy
44 : 10

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَظۡلِمُ ٱلنَّاسَ شَيۡـٔٗا وَلَٰكِنَّ ٱلنَّاسَ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ

Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote; lakini watu wenyewe wanajidhulumu nafsi zao. info

Hakika Mwenyezi Mungu Subhanahu atawalipa watu kwa vitendo vyao kwa uadilifu na haki, wala hatamdhulumu hata mmoja wapo kwa kitu chochote. Lakini watu wanajidhulumu nafsi zao kwa kukhiari kwao ukafiri kuliko Imani.

التفاسير:

external-link copy
45 : 10

وَيَوۡمَ يَحۡشُرُهُمۡ كَأَن لَّمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا سَاعَةٗ مِّنَ ٱلنَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيۡنَهُمۡۚ قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِلِقَآءِ ٱللَّهِ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ

Na Siku atakapo wakusanya, itakuwa kama kwamba hawakukaa ila saa moja tu ya mchana! Watatambuana. Hakika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuwa wenye kuongoka. info

Ewe Mtume! Wahadharishe na Siku tutayo wakusanya kwa ajili ya Hisabu, wawe na hakika kuwa Siku ya Akhera itakuja, baada ya kuwa walikuwa wakiikanusha na wakikumbuka maisha yao ya duniani tu. Waone ni kama saa moja tu ya mchana, hapana wasaa wa kufanya kitendo chochote cha kheri, na wajuane wao kwa wao wakilaumiana kwa kufuru na upotovu walio kuwa nao! Wamekhasiri wakanushao Siku ya Akhera na wasitangulize vitendo vyema katika dunia yao, na wakakosa neema za Akhera kwa kufuru zao.

التفاسير:

external-link copy
46 : 10

وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعۡضَ ٱلَّذِي نَعِدُهُمۡ أَوۡ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيۡنَا مَرۡجِعُهُمۡ ثُمَّ ٱللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ

Na vyovyote vile, tukikuonyesha baadhi ya tunayo waahidi, au tukakufisha kabla yake, marejeo yao ni kwetu. Kisha Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa wanayo yafanya. info

Ewe Mtume! Tukikuonyesha baadhi ya tunayo waahidi, nayo kuwa utawashinda na wao watapata adhabu, au tukakufisha kabla ya kuyaona yote hayo, vyovyote vile hawawezi kuepuka kurejea kwetu tuwahisabie na kuwalipa. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Mwenye kuwachungua na Mwenye kujua kila walitendalo, naye atawalipa.

التفاسير:

external-link copy
47 : 10

وَلِكُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولٞۖ فَإِذَا جَآءَ رَسُولُهُمۡ قُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa. info

Na kila umma ulijiwa na Mtume akafikisha wito wa Mwenyezi Mungu, akaamini aliye amini, na akakanusha aliye kanusha. Ikifika Siku ya kufufuliwa, Mtume wao atakuja na kuwatolea ushahidi wale walio mkadhibisha kuwa hao ni makafiri, na walio amini kuwa ni Waumini. Basi Mwenyezi Mungu atawahukumu kwa uadilifu ulio timia. Hatomdhulumu yeyote katika malipo anayo stahiki.

التفاسير:

external-link copy
48 : 10

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡوَعۡدُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

. Na wanasema: Lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli? info

Na makafiri wanakusudia kuikanusha Siku ya Akhera, basi wanaihimiza kwa kejeli na kusema: Itakuwa lini hiyo adhabu unayo tuahidi, kama wewe, ewe Mtume, na hao walio pamoja nawe, ni wakweli katika hayo mnayo yaamini na mnatuitia sisi tuyakubali?

التفاسير:

external-link copy
49 : 10

قُل لَّآ أَمۡلِكُ لِنَفۡسِي ضَرّٗا وَلَا نَفۡعًا إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۗ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌۚ إِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ فَلَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ

Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Kila umma una muda wao walio wekewa. Ukifika muda wao hawakawii hata saa moja wala hawatangulii. info

Ewe Mtume! Waambie: Mimi sina uwezo wa kujitendea mwenyewe kheri wala shari, ila kwa aliyo niwezesha Mwenyezi Mungu. Basi vipi niweze kuihimiza ije upesi hiyo adhabu? Hakika kila umma una ukomo wake aliyo uwekea Mwenyezi Mungu tangu na tangu. Ukiwadia ukomo huo basi hawatoweza kuuchelewesha hata kidogo, kama wasivyo weza kuutanguliza!

التفاسير:

external-link copy
50 : 10

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُهُۥ بَيَٰتًا أَوۡ نَهَارٗا مَّاذَا يَسۡتَعۡجِلُ مِنۡهُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ

Sema: Mwaonaje ikikufikieni hiyo adhabu yake usiku au mchana, sehemu gani ya adhabu wanaihimiza wakosefu? info

Waambie wanao himiza ifike adhabu: Hebu niambieni, ikikufikieni adhabu ya Mwenyezi Mungu usiku au mchana, pana faida gani watayo ipata wakosefu wenye madhambi kutaka ije kwa haraka? Na hali adhabu yote ni mbaya!

التفاسير:

external-link copy
51 : 10

أَثُمَّ إِذَا مَا وَقَعَ ءَامَنتُم بِهِۦٓۚ ءَآلۡـَٰٔنَ وَقَدۡ كُنتُم بِهِۦ تَسۡتَعۡجِلُونَ

Tena je! Ikisha tokea mtaiamini? Je! Ndio sasa tena? Na nyinyi mlikuwa mkiihimiza. info

Sasa mnaikanusha adhabu? Tena itapo kufikieni mtaambiwa kwa kubeuliwa: Je! Sasa mnaamini kwa kuwa mnaiona, na nyinyi huko duniani mlikuwa mkiihimiza kwa dharau na kukanusha!

التفاسير:

external-link copy
52 : 10

ثُمَّ قِيلَ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ ذُوقُواْ عَذَابَ ٱلۡخُلۡدِ هَلۡ تُجۡزَوۡنَ إِلَّا بِمَا كُنتُمۡ تَكۡسِبُونَ

Kisha walio dhulumu wataambiwa: Onjeni adhabu ya kudumu. Kwani mtalipwa isipo kuwa yale mliyo kuwa mkiyachuma? info

Tena Siku ya Kiama wataambiwa walio jidhulumu nafsi zao kwa kukufuru na kukanusha: Onjeni adhabu ya milele..sasa hamlipwi ila kwa a'mali zenu mlizo zitenda duniani.

التفاسير:

external-link copy
53 : 10

۞ وَيَسۡتَنۢبِـُٔونَكَ أَحَقٌّ هُوَۖ قُلۡ إِي وَرَبِّيٓ إِنَّهُۥ لَحَقّٞۖ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ

Na wanakuuliza: Je! Ni kweli hayo? Sema: Ehe! Naapa kwa Mola wangu Mlezi! Hakika hayo ni kweli, na wala nyinyi hamshindi! info

Na makafiri, kwa njia ya kejeli na kukataa, wanakutaka wewe, Mtume, uwaambie hivyo ni kweli hayo uliyo yaleta katika Qur'ani na khabari za kufufuliwa, na adhabu? Waambie: Naam! Kwa haki ya Muumba wangu aliye niumba, hakika hayo yatakuwa bila ya shaka yoyote. Wala nyinyi hamtoshinda wala hamwezi kuzuia adhabu aitakayo Mwenyezi Mungu kukuleteeni.

التفاسير: