ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
37 : 9

إِنَّمَا ٱلنَّسِيٓءُ زِيَادَةٞ فِي ٱلۡكُفۡرِۖ يُضَلُّ بِهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُحِلُّونَهُۥ عَامٗا وَيُحَرِّمُونَهُۥ عَامٗا لِّيُوَاطِـُٔواْ عِدَّةَ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُ فَيُحِلُّواْ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُۚ زُيِّنَ لَهُمۡ سُوٓءُ أَعۡمَٰلِهِمۡۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Hakika yale Waarabu walikuwa wakiyafanya katika kipindi cha ujinga kwa kuiharamisha miezi minne kila mwaka, kwa idadi na sio kwa kuyataja majina ya miezi iliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu, wakawa waichelewesha baadhi yake au waitanguliza, na wakaiweka badala yake miezi ya uhalali kama wanavyotaka, kulingana na mahitaji yao ya kupigana. Hakika hayo ni katika kuzidisha ukafiri. Shetani anawapoteza kwa hayo wale waliokufuru : wanauhalalisha ule waliouchelewesha kuuharamisha kati ya miezi minne mwaka huu, na wanauhalalisha mwaka mwingine, ili walinganishe kiwango cha miezi minne, wapate kuihalalisha Aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu kati ya hiyo. Shetani amewapambia vitendo viovu. Na Mwenyezi Mungu Hawaafikii watu Makafiri kufuata haki na usawa. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 9

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَا لَكُمۡ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ٱنفِرُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱثَّاقَلۡتُمۡ إِلَى ٱلۡأَرۡضِۚ أَرَضِيتُم بِٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا مِنَ ٱلۡأٓخِرَةِۚ فَمَا مَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا فِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Mkafuata sheria Zake kivitendo, mna nini nyinyi pindi mkiambiwa, «Tokeni mwnde jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ili mkapigane na maadui wenu,» mnafanya uvivu na mnajikalia majumbani mwenu? Je mnapendelea mafungu yenu ya starehe za kilimwengu kuliko neema za kesho Akhera? Basi kile mnachostarehe nacho ulimwenguni ni kichache chenye kuondoka. Ama neema za Akhera ambazo Mwenyezi Mungu Ameziandalia Waumini ni nyingi zenye kudumu. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 9

إِلَّا تَنفِرُواْ يُعَذِّبۡكُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا وَيَسۡتَبۡدِلۡ قَوۡمًا غَيۡرَكُمۡ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيۡـٔٗاۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Iwapo hamtatoka, enyi Waumini, kwenda kupigana na adui yenu , Mwenyezi Mungu Atawateremshia mateso Yake na atawaleta watu wengine ambao watatoka kwenda vitani waambiwapo watoke, watamtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Na nyinyi hamtamdhuru Mwenyezi Mungu chochote kwa kuikimbia kwenu jihadi, kwani Yeye ni mwenye kujitosheleza na nyinyi, na nyinyi ndio wahitaji Wake. Na Analolitaka Mwenyezi Mungu litakuwa hapana budi. Na Mwenyezi Mungu, juu ya kila kitu, ni Muweza, miongoni mwa kutetea dini Yake na Mtume Wake pasi na nyinyi. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 9

إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدۡ نَصَرَهُ ٱللَّهُ إِذۡ أَخۡرَجَهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ثَانِيَ ٱثۡنَيۡنِ إِذۡ هُمَا فِي ٱلۡغَارِ إِذۡ يَقُولُ لِصَٰحِبِهِۦ لَا تَحۡزَنۡ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَنَاۖ فَأَنزَلَ ٱللَّهُ سَكِينَتَهُۥ عَلَيۡهِ وَأَيَّدَهُۥ بِجُنُودٖ لَّمۡ تَرَوۡهَا وَجَعَلَ كَلِمَةَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلسُّفۡلَىٰۗ وَكَلِمَةُ ٱللَّهِ هِيَ ٱلۡعُلۡيَاۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Enyi mkusanyiko wa Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, msipotoka pamoja na yeye anapowataka mtoke, na msipomtetea, basi Mwenyezi Mungu Alimsaidia na kumtetea siku ile Makafiri wa Kikureshi walipomtoa kwenye mji wake wa Maka, na yeye ni wapili kati ya wawili( yeye na Abu Bakr al-Siddiq, radhi ya Mwenyezi Mungu imshukiye) wakawafanya ibidi waingie pangoni katika jabali la Thawr, wakakaa humo siku tatu, pindi alipomwambia rafiki Yake Abu Bakr, alipomuona ameingiwa na kicho juu yake, «Usihuzunike, Mungu Yupo pamoja na sisi» kwa kutunusuru na kutupa nguvu. Hapo Mwenyezi Mungu Aliteremsha utulivu kwenye moyo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye, na akamsaidia kwa askari ambao hakuna aliowaona kati ya wanadamu, nao ni Malaika. Hapo Mwenyezi Mungu Alimuokoa na adui yake, Akawafanya wanyonge maadui wake, Akalifanya neno la waliokanusha ndilo la chini na neno la Mwenyezi Mungu ndilo la juu. Na hilo ni kwa kuliinua juu jambo la Uislamu. Na Mwenyezi Mungu ni Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwingi wa hekima katika kuyaendesha mambo ya waja Wake. Katika aya hii pana kitambulisho cha cheo cha Abu Bakr, radhi ya Mwenyezi Mungu zimshukie. info
التفاسير: