ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
94 : 9

يَعۡتَذِرُونَ إِلَيۡكُمۡ إِذَا رَجَعۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡۚ قُل لَّا تَعۡتَذِرُواْ لَن نُّؤۡمِنَ لَكُمۡ قَدۡ نَبَّأَنَا ٱللَّهُ مِنۡ أَخۡبَارِكُمۡۚ وَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمۡ وَرَسُولُهُۥ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Watataka udhuru kwenu, enyi Wumini, hawa waliojikalisha nyuma na kuacha kupigana jihadi na washirikina, kwa kutumia maneno ya urongo, mtakaporudi kutoka kwenye jihadi ya vita vya Tabūk. Waambie, ewe Mtume, «Msitoe udhuru, hatutawaamini katika yale mnayoyasema. Mwenyezi Mungu Ashatupa habari, kuhusu mambo yenu, ambazo zimetupa uthibitisho wa urongo wenu. Mwenyezi Mungu Atayaona matendo yenu na Mtume Wake, iwapo mtatubia unafiki wenu au mtaendelea nao. Na Mwenyezi Mungu Atawaonesha watu matendo yenu waziwazi hapa duniani kisha mtarudishwa, baada ya kufa kwenu, kwa Yule Ambaye hayafichiki Kwake mambo yenu ya ndani na ya nje, ili Awape habari ya matendo yenu yote na Awape malipo yake. info
التفاسير:

external-link copy
95 : 9

سَيَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمۡ إِذَا ٱنقَلَبۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡ لِتُعۡرِضُواْ عَنۡهُمۡۖ فَأَعۡرِضُواْ عَنۡهُمۡۖ إِنَّهُمۡ رِجۡسٞۖ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُ جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Mtakaporejea kwao kutoka vitani, wanafiki watawaapia nyinyi kwa Mwenyezi Mungu, wakitoa udhuru hali ya kuwa ni warongo, ili muwaache bila kuwauliza. Basi jiepusheni nao na muwape mgongo kwa kuwadharau, kwani wao ni wachafu wa ndani. Na mahali pao pa kushukia kesho Akhera ni Moto wa Jahanamu, ukiwa ni malipo ya yale waliokuwa wa kiyatenda ya madhambi na makosa. info
التفاسير:

external-link copy
96 : 9

يَحۡلِفُونَ لَكُمۡ لِتَرۡضَوۡاْ عَنۡهُمۡۖ فَإِن تَرۡضَوۡاْ عَنۡهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَرۡضَىٰ عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Wanawaapia nyinyi, enyi Waumini, wanafiki hawa kwa urongo ili mridhike nao. Basi mkiridhika nao, kwa kuwa hamjui urongo wao, hakika Mwenyezi Mungu Haridhiki na hawa wala wengineo kati ya wale walioendelea na uasi na kutoka nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 9

ٱلۡأَعۡرَابُ أَشَدُّ كُفۡرٗا وَنِفَاقٗا وَأَجۡدَرُ أَلَّا يَعۡلَمُواْ حُدُودَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Mabedui, wakazi wa jangwani, ni washupavu zaidi wa ukafiri na unafiki kuliko wakazi wa mjini. Hivyo ni kwa sababu ya ugumu wa tabia za, ususuavu wa nyoyo zao na kuwa mbali kwao na elimu, wanavyuoni, vikao vya mawaidha na dhikr (kumtaja Mwenyezi Mungu). Kwa hivyo wao wanastahilii zaidi wasijue mipaka ya Dini na zile sheria na hukumu ambazo Mwenyezi Mungu Ameziteremsha. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa hali za hawa wote, ni Mwenye hekima Katika uendeshaji Wake mambo ya waja Wake. info
التفاسير:

external-link copy
98 : 9

وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغۡرَمٗا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ ٱلدَّوَآئِرَۚ عَلَيۡهِمۡ دَآئِرَةُ ٱلسَّوۡءِۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Na miogoni mwa Mabedui kuna wanaohesabu wanachokitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni kodi na ni hasara, hawatazamii, kwa kile wakitoacho, thawabu wala kujikinga na adhabu, na wana hamu mupatwe na misiba na maafa. Lakini mabaya yatawazunguka wao, sio Waislamu. Na Mwenyezi Mungu ni Msikizi wa wanayoyasema, ni Mjuzi wa nia zao mbaya. info
التفاسير:

external-link copy
99 : 9

وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَٰتٍ عِندَ ٱللَّهِ وَصَلَوَٰتِ ٱلرَّسُولِۚ أَلَآ إِنَّهَا قُرۡبَةٞ لَّهُمۡۚ سَيُدۡخِلُهُمُ ٱللَّهُ فِي رَحۡمَتِهِۦٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na miongoni mwa Mabedui kuna wanaomuamini Mwenyezi Mungu na kukubali upweke Wake, kufufuliwa baada ya kufa na kuwa kuna thawabu na adhabu, na wanatarajia malipo mema kwa kile chochote wanachokitoa cha matumizi katika kupigana jihadi na washirikina, kwa kusudia radhi za Mwenyezi Mungu na mapenzi Yake, na kukifanya ni njia ya kumfanya apate maombi ya Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye. Jua utanabahi kwamba matendo haya yatawaweka wao karibu na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Mwenyezi Mungu Atawatia kwenye Pepo Yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha wa maovu waliyoyafanya, ni Mwenye kuwarehemu. info
التفاسير: