ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
71 : 15

قَالَ هَٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِيٓ إِن كُنتُمۡ فَٰعِلِينَ

Lūṭ akasema kuwaambia, «Hawa wanawake wenu ni mabinti zangu, waoeni iwapo mnataka kumaliza hamu zenu, wala msiyafanye mliyokatazwa na Mwenyezi Mungu ya kuwajia wanaume.» Amewaita hao wanawake kuwa ni mabinti zake, kwa kuwa Nabii wa ummah ana cheo cha baba kwao. info
التفاسير:

external-link copy
72 : 15

لَعَمۡرُكَ إِنَّهُمۡ لَفِي سَكۡرَتِهِمۡ يَعۡمَهُونَ

Muumba Anaapa kwa Anayemtaka na kwa Anachokitaka. Ama muumbwa haifai kwake kuapa isipokuwa kwa jina la Mwenyezi mungu. Na Ameapa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa uhai wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, kwa kumtukuza kwa watu, kwamba watu wa Lūṭ wako kwenye sahau kali, wana shaka na wako kwenye ushindani. info
التفاسير:

external-link copy
73 : 15

فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُشۡرِقِينَ

Walikuwa hivyo mpaka kilipowashukia kimondo cha adhabu katika kipindi cha kutoka jua. info
التفاسير:

external-link copy
74 : 15

فَجَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةٗ مِّن سِجِّيلٍ

Hapo tulivipindua vijiji vyao tukavifanya juu yake kuwa chini yake, na tukawanyeshea mawe ya udongo uliokauka ulio mgumu. info
التفاسير:

external-link copy
75 : 15

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّلۡمُتَوَسِّمِينَ

Kwa hakika, katika yale yaliyopwapata pana mawaidha kwa wenye kuangalia na kuzingatia. info
التفاسير:

external-link copy
76 : 15

وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٖ مُّقِيمٍ

Na kwa hakika, vijiji vyao viko kwenye njia ya kudumu ambayo wasafiri wanaopitia huko wanaviona. info
التفاسير:

external-link copy
77 : 15

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ

Kwa hakika, katika kule kuwaangamiza kwetu pana ushahidi waziwazi kwa wenye kuamini na wenye kutenda matendo yanayoambatana na sheria za Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
78 : 15

وَإِن كَانَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأَيۡكَةِ لَظَٰلِمِينَ

Na kwa hakika, wakazi wa mji uliozingirwa na miti, nao ni watu wa Shu'ayb, walikuwa ni wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa kumkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume wao mtukufu. info
التفاسير:

external-link copy
79 : 15

فَٱنتَقَمۡنَا مِنۡهُمۡ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٖ مُّبِينٖ

Hivyo basi tuliwaadhibu kwa mtetemeko na adhabu ya siku ya uvuli. Na kwa hakika, makazi ya watu wa Lūṭ na watu wa Shu'ayb yako katika njia iliyo wazi, watu wanayapitia katika safari zao na wanapata mazingatio. info
التفاسير:

external-link copy
80 : 15

وَلَقَدۡ كَذَّبَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡحِجۡرِ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Na kwa hakika, walimkanusha Mtume Ṣāliḥ, amani imshukiye, watu wa bonde la Hijr, nao ni kina Thamūd, wakawa kwahilo ni wenye kuwakanusha Mitume wote. Kwani mwenye kumkanusha Mtume mmoja huwa amewakanusha Mitume wote, kwani wao wako kwenye Dini moja. info
التفاسير:

external-link copy
81 : 15

وَءَاتَيۡنَٰهُمۡ ءَايَٰتِنَا فَكَانُواْ عَنۡهَا مُعۡرِضِينَ

Na tuliwapa watu wa Ṣāliḥ aya zetu zinazojulisha usahihi wa mambo ya haki ambayo amekuja nayo kwao Mtume Ṣāliḥ, na miongoni mwayo ni ngamia, waszingatie kwa aya hizo na wakawa ni wenye kujiweka mbali nazo na kuzipa mgongo. info
التفاسير:

external-link copy
82 : 15

وَكَانُواْ يَنۡحِتُونَ مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتًا ءَامِنِينَ

Na walikuwa wakiyachonga majabali na wakifanya humo majumba, na huku wao wanajiaminisha kwamba hayatawaangukia na hayataharibika. info
التفاسير:

external-link copy
83 : 15

فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُصۡبِحِينَ

Kikawachukua wao kimondo cha adhabu kipindi cha kucha mapema. info
التفاسير:

external-link copy
84 : 15

فَمَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Na hazikuwatetea wao mali zao wala zile ngome kwenye mlilima ya mawe wala zile nguvu na heshima walizopewa. info
التفاسير:

external-link copy
85 : 15

وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۗ وَإِنَّ ٱلسَّاعَةَ لَأٓتِيَةٞۖ فَٱصۡفَحِ ٱلصَّفۡحَ ٱلۡجَمِيلَ

Na hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina yake isipokuwa kwa haki, zikiwa ni zenye kujulisha ukamilifu wa muumba wake na uweza Wake, na kwamba Yeye Ndiye Ambaye ibada yoyote haifai kufanyiwa isipokuwa Yeye, Peke Yake, Asiyekuwa na mshirika. Na ule wakati ambao Kiyama kitasimama hauna budi ni wenye kuja, ili kila mtu apate kulipwa kwa yale aliyoyatenda. Basi wasamehe, ewe Mtume, hao washirikina, usiwachukulie na uyaachilie mbali wanayoyatenda. info
التفاسير:

external-link copy
86 : 15

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡخَلَّٰقُ ٱلۡعَلِيمُ

Hakika Mola wako Ndiye Muumba wa kila kitu, Ndiye Anayekijua, kwa hivyo hakuna kitu chochote kinachomshinda wala kufichika Kwake katika ardhi wala mbinguni. info
التفاسير:

external-link copy
87 : 15

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَٰكَ سَبۡعٗا مِّنَ ٱلۡمَثَانِي وَٱلۡقُرۡءَانَ ٱلۡعَظِيمَ

Na kwa kweli tumekupa, ewe Mtume, ufunguo wa Qur,ani, nao ni hizo aya saba (za sura ya Fatiha) zinazokaririwa katika kila Swala, na tumekupa Qur,ani tukufu. info
التفاسير:

external-link copy
88 : 15

لَا تَمُدَّنَّ عَيۡنَيۡكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجٗا مِّنۡهُمۡ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَٱخۡفِضۡ جَنَاحَكَ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

Usiziangalie kwa macho yako mawili zile starehe za duniani ambazo tuliwastarehesha nazo makafiri aina mbalimbali, na usisikitike juu ya ukafiri wao, na uwanyenyekee wenye kumuamini MwenyeziMungu na Mtume wake. info
التفاسير:

external-link copy
89 : 15

وَقُلۡ إِنِّيٓ أَنَا ٱلنَّذِيرُ ٱلۡمُبِينُ

Na sema, «Mimi ndiye muonyaji mwenye kuyafunua wazi yale ambayo watu wanaongokea kwayo kwenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu. info
التفاسير:

external-link copy
90 : 15

كَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَى ٱلۡمُقۡتَسِمِينَ

Na ni mwenye kuwaonya nyinyi isije ikawapata adhabu kama ile Aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu kwa wale walioigawanya Qur,ani, wakaiamini baadhi yake na wakaikanusha baadhi nyingine miongoni mwa Mayahudi, Wanaswara na makafiri wa Kikureshi. info
التفاسير: