ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
52 : 15

إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗا قَالَ إِنَّا مِنكُمۡ وَجِلُونَ

Pindi walipoingia kwake na wakamwamkia kwa kusema, «Amani.» Hapo naye akawarudishia maamkizi ya amani. Kisha akwaletea chakula na wao wasikile, na hapo akasema, «Sisi ni wenye kicho na nyinyi.» info
التفاسير:

external-link copy
53 : 15

قَالُواْ لَا تَوۡجَلۡ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ

Malaika wakamwambia, «Usiwe na kicho. Sisi tumekuja kukupa habari njema kwamba utapata mwana atakayekuwa na ujuzi mwingi wa Dini, naye ni Is’ḥāq.» info
التفاسير:

external-link copy
54 : 15

قَالَ أَبَشَّرۡتُمُونِي عَلَىٰٓ أَن مَّسَّنِيَ ٱلۡكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ

Ibrāhīm akasema, huku yuwaona ajabu, «Mnanipa habari njema za kupata mwana na mimi nishakuwa mtu mzima, na mke wangu pia, ni kwa njia gani mnanipa habari njema hizo za kushangaza?» info
التفاسير:

external-link copy
55 : 15

قَالُواْ بَشَّرۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡقَٰنِطِينَ

Wakasema, «Tunakupa habari njema kwa kweli ambayo Mwenyezi Mungu Ametujulisha nayo. Basi usiwe miongoni mwa waliokata tamaa ya wewe kupata mwana.» info
التفاسير:

external-link copy
56 : 15

قَالَ وَمَن يَقۡنَطُ مِن رَّحۡمَةِ رَبِّهِۦٓ إِلَّا ٱلضَّآلُّونَ

Ibrāhīm akasema, «Hakika hawakati tamaa na rehema za Mola wao isipokuwa walio na makosa waliojitenga na njia ya haki.» info
التفاسير:

external-link copy
57 : 15

قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ

Na akasema, «Ni jambo gani kubwa mlilolijia, enyi mliotumwa, kutoka kwa Mwenyezi Mungu?» info
التفاسير:

external-link copy
58 : 15

قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٖ مُّجۡرِمِينَ

Wakasema, «Hakika Mwenyezi Mungu Ametutuma kuwaangamiza watu wa Lūṭ walio washirikina wapotofu, info
التفاسير:

external-link copy
59 : 15

إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمۡ أَجۡمَعِينَ

isipokuwa Lūṭ na watu wake waliomuamini, hao hatutawaangamiza na tutawaokoa wote. info
التفاسير:

external-link copy
60 : 15

إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ قَدَّرۡنَآ إِنَّهَا لَمِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ

Ama yule mke wake aliye kafiri, tumepitisha kwa amri ya Mwenyezi Mungu kumwangamiza pamoja na watakaosalia kwenye adhabu.» info
التفاسير:

external-link copy
61 : 15

فَلَمَّا جَآءَ ءَالَ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلُونَ

Basi walipofika kwa Lūṭ Malaika waliotumwa, info
التفاسير:

external-link copy
62 : 15

قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ

Aliwaambia, «Kwa kweli, nyinyi ni watu msiojulikana na mimi.» info
التفاسير:

external-link copy
63 : 15

قَالُواْ بَلۡ جِئۡنَٰكَ بِمَا كَانُواْ فِيهِ يَمۡتَرُونَ

Wakasema, «Usiogope. Kwani hakika yetu sisi tumekujilia na adhabu ambayo jamaa zako walikuwa na shaka nayo na hawakuwa wakiikubali kuwa ni kweli. info
التفاسير:

external-link copy
64 : 15

وَأَتَيۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ

Na tumekujia na haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kwa hakika sisi ni wasema kweli. info
التفاسير:

external-link copy
65 : 15

فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعٖ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَٱتَّبِعۡ أَدۡبَٰرَهُمۡ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدٞ وَٱمۡضُواْ حَيۡثُ تُؤۡمَرُونَ

Kwa hivyo, toka miongoni mwao , wakiwa pamoja na wewe watu wako waumini, baada ya kupita sehemu ya usiku. Na wewe nenda nyuma yao isije mmoja wao akasalia nyuma ikampata adhabu. Na jichungeni asije mmoja wenu akageuka na akatazama nyuma yake asije akaona adhabu na pia naye ikampata. Na kimbilieni kule ambako Amewaamrisha Mwenyezi Mungu, ili mpate kuwa mahali salama penye amani. info
التفاسير:

external-link copy
66 : 15

وَقَضَيۡنَآ إِلَيۡهِ ذَٰلِكَ ٱلۡأَمۡرَ أَنَّ دَابِرَ هَٰٓؤُلَآءِ مَقۡطُوعٞ مُّصۡبِحِينَ

Na tukampelekea wahyi Lūṭ kwamba watu wako(waliokukanusha) wataangamizwa wote, hakuna atakayesalia, pindi kutakapoanza kupambazuka. info
التفاسير:

external-link copy
67 : 15

وَجَآءَ أَهۡلُ ٱلۡمَدِينَةِ يَسۡتَبۡشِرُونَ

Na wakaja wakazi wa mji wa Lūṭ mpaka kwa Lūṭ pindi walipojua kwamba kwake kuna wageni, huku wana furaha na nderemo kwa wageni wake, ili wawachukue wafanye nao machafu. info
التفاسير:

external-link copy
68 : 15

قَالَ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ ضَيۡفِي فَلَا تَفۡضَحُونِ

Lūṭ akawaambia, «Hawa ni wageni wangu, na wako kwenye himaya yangu, basi msiniaziri, info
التفاسير:

external-link copy
69 : 15

وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ

na yaogopeni mateso ya Mwenyezi Mungu, wala msiwasumbue mkaniingiza kwenye unyonge na madharau kwa kuwaudhi wageni wangu.» info
التفاسير:

external-link copy
70 : 15

قَالُوٓاْ أَوَلَمۡ نَنۡهَكَ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Watu wake wakasema, «Kwani sisi si tulikukataza kumkaribisha mgeni yoyote miongoni mwa walimwengu - na walikuwa wakiwakatia njia wasafiri - kwa kuwa sisi tunataka kufanya machafu na wao?» info
التفاسير: