ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
16 : 15

وَلَقَدۡ جَعَلۡنَا فِي ٱلسَّمَآءِ بُرُوجٗا وَزَيَّنَّٰهَا لِلنَّٰظِرِينَ

Na miongoni mwa dalili za uweza wetu ni kwamba sisi tumeweka kwenye uwingu wa karibu vituo ya sayari kushukia, ambayo kwayo zinajulikana njia, nyakati, urutuba na ukavu, na tumeupamba uwingu huu kwa nyota ili wenye kuziangalia wataamali na wazingatie. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 15

وَحَفِظۡنَٰهَا مِن كُلِّ شَيۡطَٰنٖ رَّجِيمٍ

Na tumeuhifadhi uwingu huo na kila Shetani Aliyetolewa na aliyefukuzwa kutoka kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu ili asiufikie. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 15

إِلَّا مَنِ ٱسۡتَرَقَ ٱلسَّمۡعَ فَأَتۡبَعَهُۥ شِهَابٞ مُّبِينٞ

Isipokuwa aliyetega sikio kusikiliza maneno ya watu wa juu baadhi ya nyakati, akafikiwa na sayari inayotoa mwangaza na kumchoma.Na huenda Shetani akamddokeza rafiki yake baadhi ya habari alizozisikia kwa kutegea kabla hajateketezwa na kimondo. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 15

وَٱلۡأَرۡضَ مَدَدۡنَٰهَا وَأَلۡقَيۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ شَيۡءٖ مَّوۡزُونٖ

Na ardhi tumeinyosha ikawa kunjufu, tukaweka juu yake majabali yenye kuiimarisha , tuakaotesha kila aina ya mimea ambayo waja wanaihitajia kwa kipimo kinachojulikana. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 15

وَجَعَلۡنَا لَكُمۡ فِيهَا مَعَٰيِشَ وَمَن لَّسۡتُمۡ لَهُۥ بِرَٰزِقِينَ

Na tukawawekea nyinyi humo vitu mnavyovihitajia katika maisha yenu miongoni mwa makulima, wanyama, aina mbalimbali ya shughuli za kujipatia maisha na vinginevyo. Na tukawaumbia nyinyi watoto, watumishi na wanyama manaonufaika nao. Na riziki zao haziko juu yenu, bali ziko juu ya Mwenyezi Mungu Bwana wa viumbe vyote kwa wema utokao Kwake na ukarimu. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 15

وَإِن مِّن شَيۡءٍ إِلَّا عِندَنَا خَزَآئِنُهُۥ وَمَا نُنَزِّلُهُۥٓ إِلَّا بِقَدَرٖ مَّعۡلُومٖ

Na hakuna chochote cha manufaa ya waja isipokuwa ziko kwetu hazina zake za kila aina, na hatukiteremshi isipokuwa kwa kadiri iliyowekewa mpaka, kama vile tutakavyo. Hazina zote ziko mkononi mwa Mwenyezi Mungu, Anampa Anayemtaka na Anamzuilia Anayemtaka, kulingana na rehema Yake kunjufu na hekima Yake kubwa. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 15

وَأَرۡسَلۡنَا ٱلرِّيَٰحَ لَوَٰقِحَ فَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَسۡقَيۡنَٰكُمُوهُ وَمَآ أَنتُمۡ لَهُۥ بِخَٰزِنِينَ

Na tunatuma upepo na tunaufanya uwe mtiifu kwetu uyajaze mawingu yabubujishe maji na yanyeshe na yanywesheze miti, hapo majani yake yafunguke na mafumba yake yajitokeze. Na mvua inabeba heri na nafuu na tunayateremsha maji yake tuliyowatayarishia nyinyi kwa ajili ya kunywa kwenu, ardhi yenu na wanayama wenu. Na nyinyi si waweza wa kuyahifadhi na kuyaweka akiba, lakini sisi tunawahifadhia kwa kuwahurumia na kuwafanyia hisani. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 15

وَإِنَّا لَنَحۡنُ نُحۡيِۦ وَنُمِيتُ وَنَحۡنُ ٱلۡوَٰرِثُونَ

Ndio sisi tunaompa uhai aliyekufa kwa kumpatisha kutoka kwenye hali ya kutokuwako, na tunamfisha aliyekuwa hai baada ya ajali yake kukoma. Na sisi ndio wenye kuirithi ardhi na walioko juu yake. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 15

وَلَقَدۡ عَلِمۡنَا ٱلۡمُسۡتَقۡدِمِينَ مِنكُمۡ وَلَقَدۡ عَلِمۡنَا ٱلۡمُسۡتَـٔۡخِرِينَ

Kwa hakika tunawajua walioangamia miongoni mwenu tangu Ādam, walio hai na watakaokuja mpaka Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 15

وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحۡشُرُهُمۡۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٞ

Na hakika Mola wako Ndiye Atakayewakusanya wao wahesabiwe na walipwe. Hakika Yeye ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake mambo, ni Mwingi wa ujuzi, hakuna kinachofichika Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 15

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ

Kwa hakika tulimuumba Ādam kwa udongo mkavu, ukigongwa unasikiwa sauti. Na udongo huu mkavu ni miongoni mwa udongo mweusi uliogeuka rangi yake na harufu yake kwa kipindi kirefu cha kukaa kwake. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 15

وَٱلۡجَآنَّ خَلَقۡنَٰهُ مِن قَبۡلُ مِن نَّارِ ٱلسَّمُومِ

Na tulimuumba baba wa majini, naye ni Iblisi, kabla ya kuumbwa Ādam, kwa moto mkali sana, usio na moshi. info
التفاسير:

external-link copy
28 : 15

وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِنِّي خَٰلِقُۢ بَشَرٗا مِّن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ

Kumbuka, ewe Mtume, pindi Mola wako Aliposema kuwaambia Malaika, «Mimi nitamuumba mtu kutokana na udongo mkavu. Na udongo huu mkavu unatokana na udongo mweusi uliogeuka rangi. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 15

فَإِذَا سَوَّيۡتُهُۥ وَنَفَخۡتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُواْ لَهُۥ سَٰجِدِينَ

«Basi nitakapomtengeneza na kulikamilisha umbo lake na nikapuliza roho ndani yake, mwangukieni hali ya kusujudu,» sijida ya maamkizi na heshima na si sijida ya ibada. info
التفاسير:

external-link copy
30 : 15

فَسَجَدَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ كُلُّهُمۡ أَجۡمَعُونَ

Na Malaika wote walisujudu kwa umoja wao, kama Alivyowaamrisha Mola Wao.. Hakuna yoyote kati yao aliyekataa. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 15

إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰٓ أَن يَكُونَ مَعَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Lakini Iblisi alikataa kumsujudia Ādam pamoja na Malaika waliosujudu. info
التفاسير: