クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Abdullah Muhammad and Nasir Khamis

ページ番号:close

external-link copy
56 : 25

وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا مُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا

Na hatukukutumiliza wewe, ewe Mtume, isipokuwa uwe ni mwenye kuwabashiria Waumini Pepo na mwenye kuwaonya makafiri na Moto. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 25

قُلۡ مَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍ إِلَّا مَن شَآءَ أَن يَتَّخِذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلٗا

Waambie, «Sitaki kutoka kwenu, kwa kufikisha ujumbe, malipo yoyote. Lakini mwenye kutaka kuongoka na kufuata njia ya haki inayompeleka kwa Mola wake na kutumia katika mambo Anayoyaridhia, mimi sitawalazimisha hilo, isipokuwa hilo, kwa kweli, ni bora kwa maslahi ya nafsi zenu.» info
التفاسير:

external-link copy
58 : 25

وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱلۡحَيِّ ٱلَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِهِۦۚ وَكَفَىٰ بِهِۦ بِذُنُوبِ عِبَادِهِۦ خَبِيرًا

Na jitegemeze kwa Mwenyezi Mungu Ambaye Ana uhai uliokamilika kwa namna zote, kama inavyonasibiana na utukufu Wake, Ambaye hafi, na umtakase na sifa za upungufu. Na inatosha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi wa madhambi ya viumbe Vyake. Hakuna chochote kinachofichika Kwake katika hayo. Na Atawahesabia na Atawalipa kwa hayo. info
التفاسير:

external-link copy
59 : 25

ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ ٱلرَّحۡمَٰنُ فَسۡـَٔلۡ بِهِۦ خَبِيرٗا

Aliyeumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina yake kwa Siku sita, kisha akalingana juu ya '“Arsh - yaani Akawa juu na Akaangatika- kulingana kunakonasibiana na utisho Wake, Yeye Ndiye Mwingi wa rehema. Basi muulize, ewe Mtume, Mtambuzi kuhusu Yeye. Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Anajikusudia Mwenyewe Aliyetukuka, kwani Yeye Ndiye Anayejua sifa Zake, ukuu Wake na utukufu Wake. Na hakuna yoyote, katika binadamu, anayemjua zaidi Mwenyezi Mungu wala anayetambua habari Zake zaidi kuliko mja Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye. info
التفاسير:

external-link copy
60 : 25

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱسۡجُدُواْۤ لِلرَّحۡمَٰنِ قَالُواْ وَمَا ٱلرَّحۡمَٰنُ أَنَسۡجُدُ لِمَا تَأۡمُرُنَا وَزَادَهُمۡ نُفُورٗا۩

Na wakiambiwa makafiri, «Msujudieni Al-Raḥmān (Mwingi wa rehema) na muabuduni,» wanasema, «Hatumjui Al-Raḥmān (Mwingi wa rehema). Je, tukisujudie kila unachotuamrisha kukisujudia kwa kutii amri yako?» Basi hilo la kuwaita wao kumsujudia Al-Raḥmān (Mwingi wa rehema) linawaongezea wao kuikimbia imani na kuwa mbali nayo. info
التفاسير:

external-link copy
61 : 25

تَبَارَكَ ٱلَّذِي جَعَلَ فِي ٱلسَّمَآءِ بُرُوجٗا وَجَعَلَ فِيهَا سِرَٰجٗا وَقَمَرٗا مُّنِيرٗا

Ni kubwa baraka za Mwingi wa rehema na ni nyingi kheri Zake Aliyeziweka mbinguni nyota kubwa pamoja njia zake, na akaliweka, katika hizo mbingu, jua linalotoa mwangaza na mwezi unaong’ara. info
التفاسير:

external-link copy
62 : 25

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ خِلۡفَةٗ لِّمَنۡ أَرَادَ أَن يَذَّكَّرَ أَوۡ أَرَادَ شُكُورٗا

Na Yeye Ndiye Aliyefanya usiku na mchana vipishane, kimoja baada ya kingine, kwa anayetaka kuzingatia hilo kwa kumuamini Mwenyezi Mungu, Mpelekeshaji mambo na Muumbaji au anayetaka kumshukuru Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa neema Zake na mema Yake. info
التفاسير:

external-link copy
63 : 25

وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلَّذِينَ يَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنٗا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَٰهِلُونَ قَالُواْ سَلَٰمٗا

Na waja wa Mwingi wa rehema walio wema ni wale ambao wanatembea juu ya ardhi kwa utulivu wakiwa wanyenyekevu; na wajinga mafidhuli wanaposema nao maneno ya kuwaudhi wanawapa majibu mazuri na wanasema nao maneno ya kuwafanya wasalimike na dhambi na (pia wasalimike na) kukabiliana na mjinga kwa ujinga wake. info
التفاسير:

external-link copy
64 : 25

وَٱلَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمۡ سُجَّدٗا وَقِيَٰمٗا

Na ambao wanaswali usiku kwa wingi wakimtakasia Mola wao wakiwa ndani ya Swala na wakijidhalilisha Kwake kwa kusujudu na kusimama. info
التفاسير:

external-link copy
65 : 25

وَٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا ٱصۡرِفۡ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَۖ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا

Na ambao, pamoja na kujibidiisha kufanya ibada, wanamuogopa Mola wao na kwa hivyo wanamuomba Awaokoe na adhabu ya Jahanamu, kwani adhabu yake inalazimiana na muadhibiwa. info
التفاسير:

external-link copy
66 : 25

إِنَّهَا سَآءَتۡ مُسۡتَقَرّٗا وَمُقَامٗا

Kwa hakika moto wa Jahanamu ni mahali pabaya pa kutulia na kukaa. info
التفاسير:

external-link copy
67 : 25

وَٱلَّذِينَ إِذَآ أَنفَقُواْ لَمۡ يُسۡرِفُواْ وَلَمۡ يَقۡتُرُواْ وَكَانَ بَيۡنَ ذَٰلِكَ قَوَامٗا

Na ambao wakitumia mali zao hawapitishi kipimo katika kutoa wala hawabani katika matumizi, na kutumia kwao huwa kuko kati na kati baina ya kupitisha kipimo na kubana. info
التفاسير: