Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Abdullah Mohammed e Nasser Khamis

Numero di pagina:close

external-link copy
77 : 19

أَفَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي كَفَرَ بِـَٔايَٰتِنَا وَقَالَ لَأُوتَيَنَّ مَالٗا وَوَلَدًا

Je ushajua, ewe Mtume, na ukaona ajabu kuhusu huyu kafiri, Al-'Ās bin Wail na walio mfano wake? Kwani yeye alizikufuru aya za Mwenyezi Mungu, akazikanusha na akasema, «Nitapatiwa-nitapatiwa huko Akhera mali na watoto.» info
التفاسير:

external-link copy
78 : 19

أَطَّلَعَ ٱلۡغَيۡبَ أَمِ ٱتَّخَذَ عِندَ ٱلرَّحۡمَٰنِ عَهۡدٗا

Je, amechungulia ghaibu akaona kuwa yeye atakuwa na mali na watoto, au ana ahadi juu ya hilo kutoka kwa Mwenyezi Mungu? info
التفاسير:

external-link copy
79 : 19

كَلَّاۚ سَنَكۡتُبُ مَا يَقُولُ وَنَمُدُّ لَهُۥ مِنَ ٱلۡعَذَابِ مَدّٗا

Mambo siyo kama vile alivyodai yule kafiri, kwani yeye hana ujuzi wala hakupewa ahadi. Tutatayaandika anayoyasema ya urongo na uzushi juu ya Mwenyezi Mungu, na huko Akhera tutamuongezea aina mbali mbali za mateso, kama alivyojiongezea upotovu na upotevu. info
التفاسير:

external-link copy
80 : 19

وَنَرِثُهُۥ مَا يَقُولُ وَيَأۡتِينَا فَرۡدٗا

Na tutamrithi mali yake na watoto wake, na atatujia Siku ya Kiyama akiwa peke yake, hana mali wala watoto. info
التفاسير:

external-link copy
81 : 19

وَٱتَّخَذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ ءَالِهَةٗ لِّيَكُونُواْ لَهُمۡ عِزّٗا

Na washirikina wamewachukua waungu wanaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ili wawatetee na wajipatie nguvu kwao. info
التفاسير:

external-link copy
82 : 19

كَلَّاۚ سَيَكۡفُرُونَ بِعِبَادَتِهِمۡ وَيَكُونُونَ عَلَيۡهِمۡ ضِدًّا

Mambo sivyo kama wanavyodai. Hawa waungu hawatakuwa ni nguvu kwao, lakini waungu hawa watawaruka huko Akhera kuwa waliwaabudu wao na watakuwa ni wenye kusaidia katika kuteta na wao na kuwakanusha , kinyume na vile walivyodhania juu yao. info
التفاسير:

external-link copy
83 : 19

أَلَمۡ تَرَ أَنَّآ أَرۡسَلۡنَا ٱلشَّيَٰطِينَ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ تَؤُزُّهُمۡ أَزّٗا

Je, huoni, ewe Mtume, kwamba sisi tumewasaliti Mashetani juu ya wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu na Mitume Wake, ili wawapoteze na wawaondoe kutoka kwenye utiifu kuwapeleka kwenye uasi? info
التفاسير:

external-link copy
84 : 19

فَلَا تَعۡجَلۡ عَلَيۡهِمۡۖ إِنَّمَا نَعُدُّ لَهُمۡ عَدّٗا

Basi usiwafanyie haraka, ewe Mtume, kwa kutaka adhabu iwashukie hawa makafiri, kwa kweli sisi tunahesabu umri wao na matendo yao hesabu isiyo na kasoro wala ukawiaji. info
التفاسير:

external-link copy
85 : 19

يَوۡمَ نَحۡشُرُ ٱلۡمُتَّقِينَ إِلَى ٱلرَّحۡمَٰنِ وَفۡدٗا

Siku ambayo tutawakusanya wachamungu kwa Mola wao Mwenye huruma na wao, wakiwa makundi ya watu wenye kukirimiwa, info
التفاسير:

external-link copy
86 : 19

وَنَسُوقُ ٱلۡمُجۡرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرۡدٗا

na tutawaongoza wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu kwa kuwasuta kwa nguvu kuwapeleka Motoni, wakitembea kwa miguu, wakiwa na kiu. info
التفاسير:

external-link copy
87 : 19

لَّا يَمۡلِكُونَ ٱلشَّفَٰعَةَ إِلَّا مَنِ ٱتَّخَذَ عِندَ ٱلرَّحۡمَٰنِ عَهۡدٗا

Makafiri hawa hawatakuwa na uwezo wa kumuombea yoyote. Watakaokuwa na uwezo huo ni wale waliochukua ahadi ya hilo mbele ya Mwingi wa rehema, nao ni wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake. info
التفاسير:

external-link copy
88 : 19

وَقَالُواْ ٱتَّخَذَ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَلَدٗا

Na hawa makafiri walisema, «Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto.» info
التفاسير:

external-link copy
89 : 19

لَّقَدۡ جِئۡتُمۡ شَيۡـًٔا إِدّٗا

Kwa hakika mumeleta, enyi hao wenye kusema, kwa kusema neno hili, jambo kubwa lililo baya. info
التفاسير:

external-link copy
90 : 19

تَكَادُ ٱلسَّمَٰوَٰتُ يَتَفَطَّرۡنَ مِنۡهُ وَتَنشَقُّ ٱلۡأَرۡضُ وَتَخِرُّ ٱلۡجِبَالُ هَدًّا

Zakaribia mbingu kupasuka kwa ubaya mkubwa wa neno hilo, ardhi kuvunjika vipande-vipande ma majabali kuanguka kwa nguvu kwa kukasirika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu info
التفاسير:

external-link copy
91 : 19

أَن دَعَوۡاْ لِلرَّحۡمَٰنِ وَلَدٗا

kwa kumnasibishia mtoto, Mwenyezi Mungu Ametukuka na jambo hilo kutukuka kukubwa sana. info
التفاسير:

external-link copy
92 : 19

وَمَا يَنۢبَغِي لِلرَّحۡمَٰنِ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا

Haifai kwa Mwenyezi Mungu na hainasibiani na Yeye Awe na mtoto, kwani kuwa na mtoto ni dalili ya upungufu na mahitajio, na Mwenyezi Mungu Ndiye Mkwasi Mwenye kuhimidiwa Aliyeepushwa na sifa zote za upungufu. info
التفاسير:

external-link copy
93 : 19

إِن كُلُّ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ إِلَّآ ءَاتِي ٱلرَّحۡمَٰنِ عَبۡدٗا

Hakuna aliye mbinguni, miongoni mwa Malaika, wala aliye ardhini, miongoni mwa binadamu na majini, isipokuwa atamjia Mola wake Siku ya Kiyama akiwa ni mja mdhalilifu mnyenyekevu mwenye kukubali uja wake Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
94 : 19

لَّقَدۡ أَحۡصَىٰهُمۡ وَعَدَّهُمۡ عَدّٗا

Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Amewadhibiti viumbe Wake wote na Ameijua idadi yao, hakuna yoyote miongono mawao mwenye kufichika na Yeye. info
التفاسير:

external-link copy
95 : 19

وَكُلُّهُمۡ ءَاتِيهِ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فَرۡدًا

Na kila mtu, miongoni mwa viumbe, atamjia Mola wake, Siku ya Kiyama, hali ya kuwa hana mali wala watoto pamoja na yeye. info
التفاسير: