Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Abdullah Mohammed e Nasser Khamis

Numero di pagina:close

external-link copy
39 : 19

وَأَنذِرۡهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡحَسۡرَةِ إِذۡ قُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ وَهُمۡ فِي غَفۡلَةٖ وَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Na uwaonye watu, ewe Mtume, Siku ya Majuto, wakati wa hukumu kutolewa, na mauti yaletwe kama kwamba ni kondoo mzuri, achinjwe hapo na na uamuzi utolewe baina ya viumbe, na hapo watu wa Imani waende Peponi na watu wa ukafiri waende Motoni, na hali wao leo katika dunia hii wameghafilika na yale ambayo walionywa nayo, hivyo basi hawaamini wala hawafanyi matendo mema. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 19

إِنَّا نَحۡنُ نَرِثُ ٱلۡأَرۡضَ وَمَنۡ عَلَيۡهَا وَإِلَيۡنَا يُرۡجَعُونَ

Sisi ndio tutakaoirithi ardhi na walio juu yake kwa kutoeka kwao na kusalia kwetu baada yao, na uamuzi wetu kupitishwa kwao. Na kwetu sisi ndio mwisho wao na kuhesabiwa kwao, na hapo tuwalipe kwa matendo yao. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 19

وَٱذۡكُرۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ إِبۡرَٰهِيمَۚ إِنَّهُۥ كَانَ صِدِّيقٗا نَّبِيًّا

Na uwatajie, ewe Mtume, watu wako katika hii Qur’ani kisa cha Ibrahīm, amani imshukiye; kwa hakika yeye alikuwa ni mkweli mkubwa na ni miongoni mwa Manabii wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, wenye daraja za juu. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 19

إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ يَٰٓأَبَتِ لِمَ تَعۡبُدُ مَا لَا يَسۡمَعُ وَلَا يُبۡصِرُ وَلَا يُغۡنِي عَنكَ شَيۡـٔٗا

Aliposema kumwambia babake, Āzar, «Ewe baba yangu! Ni kwa jambo gani unaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, masanamu wasiosikia, wasioona na wasioweza kuzuia chochote kisikufike? info
التفاسير:

external-link copy
43 : 19

يَٰٓأَبَتِ إِنِّي قَدۡ جَآءَنِي مِنَ ٱلۡعِلۡمِ مَا لَمۡ يَأۡتِكَ فَٱتَّبِعۡنِيٓ أَهۡدِكَ صِرَٰطٗا سَوِيّٗا

«Ewe baba yangu! Hakika Mwenyezi Mungu Amenipa ujuzi ambao hakukupa, basi nikubalie na unifuate kwa yale ninayokuitia kwayo, nikuongoze kwenye njia ya sawa ambayo hutapotea ukiifuata. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 19

يَٰٓأَبَتِ لَا تَعۡبُدِ ٱلشَّيۡطَٰنَۖ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ كَانَ لِلرَّحۡمَٰنِ عَصِيّٗا

«Ewe baba yangu! Usimtii Shetani ukawaabudu hawa masanamu, kwani Shetani anaenda kinyume na Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, anakuwa na kiburi kumtii Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 19

يَٰٓأَبَتِ إِنِّيٓ أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٞ مِّنَ ٱلرَّحۡمَٰنِ فَتَكُونَ لِلشَّيۡطَٰنِ وَلِيّٗا

«Ewe baba yangu! Mimi ninaogopa usije ukafa kwenye ukafiri wako, ikakupata adhabu ya Mwingi wa rehema na ukawa ni rafiki wa Shetani ndani ya Moto.» info
التفاسير:

external-link copy
46 : 19

قَالَ أَرَاغِبٌ أَنتَ عَنۡ ءَالِهَتِي يَٰٓإِبۡرَٰهِيمُۖ لَئِن لَّمۡ تَنتَهِ لَأَرۡجُمَنَّكَۖ وَٱهۡجُرۡنِي مَلِيّٗا

Baba yake Ibrāhīm akasema kumwambia mwanawe,»Kwani wewe umegeuka na kukataa kuabudu waungu wangu, ewe Ibrāhīm» Basi usipokomeka kuwatukana, nitakuua kwa kukupiga mawe. Na niondokee, usikutane na mimi wala usiseme na mimi kwa kipindi cha muda mrefu.» info
التفاسير:

external-link copy
47 : 19

قَالَ سَلَٰمٌ عَلَيۡكَۖ سَأَسۡتَغۡفِرُ لَكَ رَبِّيٓۖ إِنَّهُۥ كَانَ بِي حَفِيّٗا

Ibrāhīm alisema kumwambia baba yake, «Amani juu yako kutoka kwangu, halitakufikia kutoka kwangu jambo unalolichukia, na nitakuombea Mwenyezi Mungu uongofu na msamaha. Hakika Mola wangu ni Mwingi wa huruma ni Mpole kwangu kulingana na hali yangu, nikimuomba Ataniitikia. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 19

وَأَعۡتَزِلُكُمۡ وَمَا تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَأَدۡعُواْ رَبِّي عَسَىٰٓ أَلَّآ أَكُونَ بِدُعَآءِ رَبِّي شَقِيّٗا

«Na nitawaepuka nyinyi na waungu wenu mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na nitamuomba Mola wangu kwa kumtakasia, nikiwa na matumaini kuwa sitapita patupu kwa kumuomba Mola wangu Asinipe ninachomuomba.» info
التفاسير:

external-link copy
49 : 19

فَلَمَّا ٱعۡتَزَلَهُمۡ وَمَا يَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَهَبۡنَا لَهُۥٓ إِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَۖ وَكُلّٗا جَعَلۡنَا نَبِيّٗا

Na alipowaepuka wao na waungu wao wanaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tulimruzuku, miongoni mwa watoto tuliomruzuku, Ish,āq na Ya'ūb mwana wa Ish,āq na tukawafanya wawaili hao kuwa Manabii. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 19

وَوَهَبۡنَا لَهُم مِّن رَّحۡمَتِنَا وَجَعَلۡنَا لَهُمۡ لِسَانَ صِدۡقٍ عَلِيّٗا

Na tukawatunukia wao wote rehema zetu zikiwa ni nyongeza zisizohesabika, na tukawajaalia watajike vizuri na wasifiwe kwa sifa njema zenye kubaki kwa watu. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 19

وَٱذۡكُرۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ مُوسَىٰٓۚ إِنَّهُۥ كَانَ مُخۡلَصٗا وَكَانَ رَسُولٗا نَّبِيّٗا

Na utaje katika Qur’ani, ewe Mtume, kisa cha Mūsā, amani imshukiye. Kwa hakika, yeye alikuwa ni mteule aliyesafishwa, na alikuwa ni Mtume na ni Nabii miongoni mwa Mitume waliokuwa na uthabiti. info
التفاسير: