Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassarar Sawahil - Ali Muhsin al-Barwani

external-link copy
10 : 85

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ

Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua. info

Hakika walio watia matatani Waumini wanaume na Waumini wanawake kwa maudhi na kuwaadhibu kwa moto, kisha wasitubu na kurejea nyuma watapata Akhera adhabu ya Jahannamu kwa ukafiri wao, na watapata adhabu ya kuunguzwa kwa kule kuwaunguza moto Waumini.

التفاسير: