Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassarar Sawahil - Ali Muhsin al-Barwani

Lambar shafi:close

external-link copy
25 : 2

وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ أَنَّ لَهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ كُلَّمَا رُزِقُواْ مِنۡهَا مِن ثَمَرَةٖ رِّزۡقٗا قَالُواْ هَٰذَا ٱلَّذِي رُزِقۡنَا مِن قَبۡلُۖ وَأُتُواْ بِهِۦ مُتَشَٰبِهٗاۖ وَلَهُمۡ فِيهَآ أَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞۖ وَهُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Na wabashirie walio amini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake; kila watapo pewa matunda humo, watasema: Haya ndiyo kama tuliyo pewa mbele. Na wataletewa matunda yaliyo fanana; na humo watakuwa na wake walio takasika; na wao humo watadumu. info

Ikiwa hizi ni adhabu za waovu wapinzani, basi Pepo ndio makao ya Waumini. Waambie wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Kitabu chake, na wakaikubali haki bila ya kutia shaka au wasiwasi, na wakatenda vitendo vyema - waambie khabari ya kuwafurahisha na kukunjua vifua vyao; nayo ni kuwa Mwenyezi Mungu amewaandalia mabustani yenye mazao, yapitayo mito chini ya miti yake na majumba yake. Kila Mwenyezi Mungu akiwaruzuku matunda ya hizo bustani wao husema: "Haya yamefanana na yale tuliyo pewa kabla." Kwani matunda haya yanashabihiana kwa sura, lakini yanakhitalifiana kwa utamu na ladha. Na watakuwa nao humo pia wake walio kamilika walio safi, wasio kuwa na ila yoyote. Na katika Pepo hii wataishi maisha ya milele wala hawatotoka humo.

التفاسير:

external-link copy
26 : 2

۞ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسۡتَحۡيِۦٓ أَن يَضۡرِبَ مَثَلٗا مَّا بَعُوضَةٗ فَمَا فَوۡقَهَاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَيَعۡلَمُونَ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡۖ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَيَقُولُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلٗاۘ يُضِلُّ بِهِۦ كَثِيرٗا وَيَهۡدِي بِهِۦ كَثِيرٗاۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِۦٓ إِلَّا ٱلۡفَٰسِقِينَ

Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano hata wa mbu na ulio wa zaidi yake. Ama wale walio amini hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi, lakini wale walio kufuru husema: Ni nini analo kusudia Mwenyezi Mungu kwa mfano huu? Kwa mfano huu huwapoteza wengi na huwaongoa wengi; lakini hawapotezi ila wale wapotovu, info

Mwenyezi Mungu huwaletea mifano watu kueleza hakika ya mambo yalivyo juu, kwa kufananisha na vidudu vidogo na pia vitu vikubwa. Wasio amini waliikejeli hiyo mifano ya vijidudu vidogo kama nzi na buibui. Basi Mwenyezi Mungu aliye takasika haoni aibu kama wanavyo aibika watu kwa kuona haya. Hana la kumzuia asiwape waja wake mfano wowote autakao hata ukiwa mdogo vipi. Kwa hivyo ni sawa kabisa kupiga mfano wa mbu na kilio zaidi kuliko hivyo. Na walio amini wanajua kuwa hii ni mifano, na kuwa huu ni ukweli utokao kwa Mwenyezi Mungu. Ama walio kufuru hawapendi hayo, na husema: "Mwenyezi Mungu anataka nini kwa mfano huu?" Na mfano kama huu huwa ni sababu ya kupotea wale wasio tafuta haki wala hawaitaki, na huwa ni sababu ya kuwaongoa wenye kuamini na kuitaka haki. Basi hawapotei ila waasi walio kwisha potea.

التفاسير:

external-link copy
27 : 2

ٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهۡدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مِيثَٰقِهِۦ وَيَقۡطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara. info

Na hao walio kwisha potea ni wale ambao wanaivunja ahadi ya Mwenyezi Mungu, na wao ndio wasio ishika vilivyo ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyo iweka katika nafsi zao tangu kuumbwa, kuwa ni fungamano la akili yenye kutambua na yenye kuunga mkono Utume, na wakayakata yale aliyo yaamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, kama vile kuwaangalia jamaa, na kupendana na kutendeana mema, na kuoneana hurumu watu kwa watu; na wakafanya fisadi katika nchi kwa mambo maovu na kuzua fitna na kuchochea vita na kuharibu majenzi. Hao ndio wenye kuleta khasara kwa kufisidi khulka yao walio umbwa nayo, na wakawagawa watu mapande mapande, badala ya kuleta mapenzi na kuoneana huruma kama inavyo stahiki. Kwa vitendo vyao hivyo watapata hizaya duniani na adhabu huko Akhera.

التفاسير:

external-link copy
28 : 2

كَيۡفَ تَكۡفُرُونَ بِٱللَّهِ وَكُنتُمۡ أَمۡوَٰتٗا فَأَحۡيَٰكُمۡۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمۡ ثُمَّ يُحۡيِيكُمۡ ثُمَّ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu akakufufueni! Kisha atakufisheni, tena atakufufueni, kisha kwake mtarejeshwa?. info

Hakika hali yenu instaajabisha! Vipi mnakufuru na wala hapana sababu yoyote ya kutegemewa katika kukufuru kwenu? Ukiangalia hali yenu utaona inakataa ukafiri huu wala hamna udhuru wowote. Kwani nyinyi mlikuwa maiti, hamna uhai, akakuumbeni Mwenyezi Mungu na akakupeni uhai na umbo zuri. Kisha ni Yeye atakaye kurejezeni muwe maiti baada ya kutimia wakati wenu. Kisha atakufufueni muwe hai mara nyingine kwa ajili ya hisabu na malipo. Kisha mtarejea kwake, wala hamwendi kwa mwenginewe, mtarejea, kwa ajili ya hisabu na malipwa kwa vitendo vyenu.

التفاسير:

external-link copy
29 : 2

هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰٓ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَسَوَّىٰهُنَّ سَبۡعَ سَمَٰوَٰتٖۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ

Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi. Tena akazielekea mbingu, na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu. info

Mwenyezi Mungu anaye pasa kuabudiwa na kut'iiwa ndiye aliye kufadhilini. Akaumba kwa ajili ya manufaa na faida yenu kila neema inayo patikana duniani, kisha baadae akazielekea mbingu akaziumba mbingu saba kwa mpango. Katika hayo yapo mnayo yaona na msiyo yaona. Na Mwenyezi Mungu amevizunguka vitu vyote, na anavijua vyote.

التفاسير: