Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassarar Sawahil - Ali Muhsin al-Barwani

Al-Qari'ah

external-link copy
1 : 101

ٱلۡقَارِعَةُ

Inayo gonga! info

AL-QAARIA'H, Inayo gonga, ni Kiyama, ambacho kinaanza kwa mpulizo wa mwanzo wa barugumu, na kinaishia itapo katwa hukumu baina ya watu.

التفاسير:

external-link copy
2 : 101

مَا ٱلۡقَارِعَةُ

Nini Inayo gonga? info

Kitu gani kilicho cha ajabu zaidi katika ukuu wake, na khatari zake na kitisho chake!

التفاسير:

external-link copy
3 : 101

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡقَارِعَةُ

Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga? info

Na kitu gani kitacho kujuulisha hali ya AL-QAARIA'H katika kitisho chake juu ya nafsi za watu?

التفاسير:

external-link copy
4 : 101

يَوۡمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلۡفَرَاشِ ٱلۡمَبۡثُوثِ

Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika; info

Siku hiyo watu watakuwa kama vipepeo kwa wingi na kuhangaika kulia na kushoto, madhaifu na wanyonge!

التفاسير:

external-link copy
5 : 101

وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ ٱلۡمَنفُوشِ

Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa! info

Na milima itakuwa kama sufi iliyo tiwa rangi na kuchambuliwa kwa kutapanyika vipande mbali mbali na kupeperuka katika anga huku na huku.

التفاسير:

external-link copy
6 : 101

فَأَمَّا مَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ

Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, info

Ama yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, mema yake yakapindukia kuliko maovu yake,

التفاسير:

external-link copy
7 : 101

فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ

Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza. info

Basi huyo atakuwa na maisha yatayo mridhisha mwenyewe, na nafsi yake itue.

التفاسير:

external-link copy
8 : 101

وَأَمَّا مَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ

Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, info

Na ama ambaye mizani yake itakuwa nyepesi, na maovu yake yakazidi kuliko mema yake,

التفاسير:

external-link copy
9 : 101

فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةٞ

Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! info

Basi makaazi yake yatakuwa Jahannamu.

التفاسير:

external-link copy
10 : 101

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا هِيَهۡ

Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo? info

Na nini cha kukujuulisha ni nini Hawiya?

التفاسير:

external-link copy
11 : 101

نَارٌ حَامِيَةُۢ

Ni Moto mkali! info

Moto ulio mkali, hapana moto unao fikilia ukali wake, hata ukichochewa vipi na kutiwa kuni gani!

التفاسير: