Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da harshen Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis

external-link copy
40 : 7

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَٱسۡتَكۡبَرُواْ عَنۡهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمۡ أَبۡوَٰبُ ٱلسَّمَآءِ وَلَا يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ ٱلۡجَمَلُ فِي سَمِّ ٱلۡخِيَاطِۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Hakika wale makafiri ambao hawakuzikubali hoja zetu na aya zetu zinazojulisha upweke wetu na ambao hawakuzitumia sheria zetu kwa kiburi na majivuno, vitendo vyao maishani, na pia roho zao wakati wa kufa, havitafunguliwa milango ya mbingu. Na haiwezekani kwa makafiri hawa kuingia Peponi isipokuwa iwapo ngamia ataingia kwenye tundu ya sindano; na hilo ni muhali. Na mfano wa malipo haya tutawalipa wale ambao uovu wao umezidi na kukiuka kwao mipaka kumepindukia. info
التفاسير: