Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da harshen Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis

external-link copy
39 : 7

وَقَالَتۡ أُولَىٰهُمۡ لِأُخۡرَىٰهُمۡ فَمَا كَانَ لَكُمۡ عَلَيۡنَا مِن فَضۡلٖ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡسِبُونَ

Hapo watasema wale waliofuatwa miongoni mwa viongozi na wengineo kuwaambia wafuasi wao, «Sisi na nyinyi tuko sawa katika uharibifu na upotevu na katika kufanya vitendo ambavyo ndio sababu ya kupata adhabu, kwa hivyo, nyinyi hamuna ubora juu yetu.» Mwenyezi Mungu Atawaambia wao wote, «Basi ionjeni adhabu,» yaani adhabu ya Jahanamu «kwa makosa mliyoyatenda.» info
التفاسير: