Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da harshen Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis

external-link copy
8 : 5

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُونُواْ قَوَّٰمِينَ لِلَّهِ شُهَدَآءَ بِٱلۡقِسۡطِۖ وَلَا يَجۡرِمَنَّكُمۡ شَنَـَٔانُ قَوۡمٍ عَلَىٰٓ أَلَّا تَعۡدِلُواْۚ ٱعۡدِلُواْ هُوَ أَقۡرَبُ لِلتَّقۡوَىٰۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie,, kuweni wasimamizi wa haki kwa ajili ya kuzitafuta radhi za Mwenyezi Mungu, muwe mashahidi kwa uadilifu. Wala kusiwapelekee nyinyi kuwachukia watu kuacha kufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu baina ya maadui na vipenzi kwa daraja moja sawasawa. Kufanya uadilifu huko kuko karibu zaidi na kumuogopa Mwenyezi Mungu. Na jihadharini na kufanya udhalimu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi wa mnayoyafanya na Atawalipa kwa hayo. info
التفاسير: