Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da harshen Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis

Lambar shafi:close

external-link copy
44 : 24

يُقَلِّبُ ٱللَّهُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّأُوْلِي ٱلۡأَبۡصَٰرِ

Na miongoni mwa ushahidi wa kutolea dalili uweza wa Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, kwamba Yeye Anaugeuza usiku na mchana kwa kuja mmoja wapo baada ya mwingine na kutafautiana kwao kwa urefu na ufupi. Katika hilo pana ushahidi kwa mtu mwenye busara na kuizingatia. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 24

وَٱللَّهُ خَلَقَ كُلَّ دَآبَّةٖ مِّن مَّآءٖۖ فَمِنۡهُم مَّن يَمۡشِي عَلَىٰ بَطۡنِهِۦ وَمِنۡهُم مَّن يَمۡشِي عَلَىٰ رِجۡلَيۡنِ وَمِنۡهُم مَّن يَمۡشِي عَلَىٰٓ أَرۡبَعٖۚ يَخۡلُقُ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amekiumba kila kitambaacho ardhini kutokana na maji, kwani maji ndio asili ya kuumbwa kwake. Na miongoni mwa vitambaavyo kuna anayetembea kwa matumbo yake kama vile nyoka na mfano wake, na katika hao kuna anayetembea kwa miguu miwli kama binadamu, na miongoni mwao kuna anayetembea kwa miguu minne kama wanyama na mfano wake. Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Anaumba anachotaka, na Yeye ni Muweza wa kila kitu. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 24

لَّقَدۡ أَنزَلۡنَآ ءَايَٰتٖ مُّبَيِّنَٰتٖۚ وَٱللَّهُ يَهۡدِي مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Na kwa hakika tumeteremsha katika Qur’ani vitambulisho vilivyo waziwazi venye kuongoza kwenye haki. Na Mwenyezi Mungu Anamuongoza na kumuelekeza Anayemtaka katika waja wake kwenye njia iliyolingana sawa, nayo ni Uislamu. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 24

وَيَقُولُونَ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلرَّسُولِ وَأَطَعۡنَا ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٞ مِّنۡهُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَۚ وَمَآ أُوْلَٰٓئِكَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na wanafiki wanasema, «Tumemuamuni Mwenyezi Mungu na yale ambayo amekuja nayo Mtume na tumezitii amri zao.» Kisha vinatoka vikundi kati yao, baada ya hapo, vikayapa mgongo hayo, visiukubali uamuzi wa Mtume. Basi hao hawakuwa ni Waumini. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 24

وَإِذَا دُعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ لِيَحۡكُمَ بَيۡنَهُمۡ إِذَا فَرِيقٞ مِّنۡهُم مُّعۡرِضُونَ

Na wanapoitwa, wanapokuwa kwenye ugomvi baina yao, kwenye hukumu iliyo ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na waje kwa Mtume ili afanye uamuzi kati yao, ghafula hujitokeza kikundi kati yao kikajiepusha na kikawa hakikubali hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, pamoja na kuwa hiyo ndiyo haki isiyo na shaka. info
التفاسير:

external-link copy
49 : 24

وَإِن يَكُن لَّهُمُ ٱلۡحَقُّ يَأۡتُوٓاْ إِلَيۡهِ مُذۡعِنِينَ

Na iwapo haki iko upande wao, basi wao wanakuja kwa Nabii, rehema na amani zimshukie, wakiwa watiifu na kuwa tayari kuiandama hukumu yake, kwa kutambua kwao kwamba yeye atatoa uamuzi wa haki. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 24

أَفِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَمِ ٱرۡتَابُوٓاْ أَمۡ يَخَافُونَ أَن يَحِيفَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ وَرَسُولُهُۥۚ بَلۡ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Je, sababu ya kupa mgongo kwao ni ule ugonjwa wa unafiki ulio ndani ya nyoyo zao au wanaushuku unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie? Au sababu ni kuchelea kwao isije ikawa hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni ya maonevu? Ukweli ni kwamba wao hawaogopei maonevu, isipokuwa kiini hasa ni kwamba wao wenyewe ndio madhalimu walio waovu. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 24

إِنَّمَا كَانَ قَوۡلَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ إِذَا دُعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ لِيَحۡكُمَ بَيۡنَهُمۡ أَن يَقُولُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Ama Waumini wa kweli, msimamo wao ni kwamba wanapoitwa kwenda kuhukumiwa, katika ugomvi ulio kati yao, na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na hukumu ya Mtume Wake, wanakubali uamuzi unaotolewa na wanasem, «Tumesikia tulioambiwa na tumemtii aliyetuita kwenye hilo.» Na hao ndio waliofaulu wenye kufuzu kupata matakwa yao kwenye mabustani ya Pepo yenye neema. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 24

وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَخۡشَ ٱللَّهَ وَيَتَّقۡهِ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَآئِزُونَ

Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika kufuata maamrisho na kujiepusha na makatazo na akaogopa mwisho mbaya wa uasi na akajihadhari na adhabu ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio wenye kufuzu kupata neema Peponi.. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 24

۞ وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَئِنۡ أَمَرۡتَهُمۡ لَيَخۡرُجُنَّۖ قُل لَّا تُقۡسِمُواْۖ طَاعَةٞ مَّعۡرُوفَةٌۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Na wanafiki waliapa kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, kwa upeo wa juhudi yao, viapo vizito, «Ukituamrisha, ewe Mtume, kutoka kwenda kwenye jihadi pamoja na wewe, tutatoka tena tutatoka» Sema uwaambie, «Msiape viapo vya urongo, kwani utiifu wenu unajulikana kuwa ni wa ulimini tu. Kwa kweli Mwenyezi Mungu Anayatambua mnayoyafanya, na Atawapa malipo yake. info
التفاسير: