Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahilie - 'Alî Muhsin Al Barwânî

At-Tur

external-link copy
1 : 52

وَٱلطُّورِ

Naapa kwa mlima wa T'ur! info

Ninaapa kwa mlima wa T'ur ulioko katika Sinai. Kwenye mlima huo ndio Nabii Musa a.s. alisemezwa.

التفاسير:

external-link copy
2 : 52

وَكِتَٰبٖ مَّسۡطُورٖ

Na Kitabu kilicho andikwa . info

Ninaapa kwa mlima wa T'ur ulioko katika Sinai. Kwenye mlima huo ndio Nabii Musa a.s.

التفاسير:

external-link copy
3 : 52

فِي رَقّٖ مَّنشُورٖ

Katika ngozi iliyo kunjuliwa! info

Kilicho andikwa katika kurasa zilio nyepesi kuzisoma,

التفاسير:

external-link copy
4 : 52

وَٱلۡبَيۡتِ ٱلۡمَعۡمُورِ

Na kwa Nyumba iliyo jengwa! info

Na kwa Nyumba iliyo jengwa kwa sababu ya wenye kuizunguka kwa ibada na wenye kusimama na kurukuu na kusujudu kwa Swala,

التفاسير:

external-link copy
5 : 52

وَٱلسَّقۡفِ ٱلۡمَرۡفُوعِ

Na kwa dari iliyo nyanyuliwa! info

Na naapa kwa mbingu iliyo nyanyuliwa bila ya nguzo, na bahari iliyo jaa.

التفاسير:

external-link copy
6 : 52

وَٱلۡبَحۡرِ ٱلۡمَسۡجُورِ

Na kwa bahari iliyo jazwa! info

Na bahari iliyo jaa.

التفاسير:

external-link copy
7 : 52

إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَٰقِعٞ

Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea. info

Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi waliyo ahidiwa makafiri bila ya shaka itawateremkia hapana hivi wala hivi.

التفاسير:

external-link copy
8 : 52

مَّا لَهُۥ مِن دَافِعٖ

Hapana wa kuizuia. info

Hapana wa kuizuia isiwafikilie.

التفاسير:

external-link copy
9 : 52

يَوۡمَ تَمُورُ ٱلسَّمَآءُ مَوۡرٗا

Siku zitakapo tikisika mbingu kwa mtikiso! info

Siku mbingu itapo tikisika kwa mtikiso mkubwa.

التفاسير:

external-link copy
10 : 52

وَتَسِيرُ ٱلۡجِبَالُ سَيۡرٗا

Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa. info

Na milima itapo ng'oka kutoka hapo ilipo kwa kuonekana khasa.

التفاسير:

external-link copy
11 : 52

فَوَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Basi ole wao siku hiyo hao wanao kadhibisha, info

Maangamio makubwa yatawapata siku hiyo hao wanao kadhibisha Haki.

التفاسير:

external-link copy
12 : 52

ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي خَوۡضٖ يَلۡعَبُونَ

Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi. info

Ambao katika upotovu ndio mchezo wao wanapo chezea.

التفاسير:

external-link copy
13 : 52

يَوۡمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا

Siku watapo sukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu, info

Siku watakapo sukumwa kuingizwa Motoni kwa nguvu.

التفاسير:

external-link copy
14 : 52

هَٰذِهِ ٱلنَّارُ ٱلَّتِي كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ

(Waambiwe): Huu ndio ule Moto mlio kuwa mkiukanusha! info

Wataambiwa: Huu ndio Moto mlio kuwa mkiukanusha duniani.

التفاسير:

external-link copy
15 : 52

أَفَسِحۡرٌ هَٰذَآ أَمۡ أَنتُمۡ لَا تُبۡصِرُونَ

Je! Huu ni uchawi, au hamwoni tu? info

Je! Bado mnaendelea kuukanya. Huu Moto mnao uona ni uchawi, au hamwoni tu?

التفاسير:

external-link copy
16 : 52

ٱصۡلَوۡهَا فَٱصۡبِرُوٓاْ أَوۡ لَا تَصۡبِرُواْ سَوَآءٌ عَلَيۡكُمۡۖ إِنَّمَا تُجۡزَوۡنَ مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyo kuwa mkiyatenda. info

Uingieni, mpate kuonja vukuto lake. Mkivumilia shida zake, au mkitovumilia, kwenu ni mamoja. Hakika leo mtayakuta mliyo kuwa mkiyatenda duniani.

التفاسير:

external-link copy
17 : 52

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَنَعِيمٖ

Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na neema, info

Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani yenye wasaa, hapana awezae kuyaeleza yalivyo, na neema kubwa kadhaalika.

التفاسير:

external-link copy
18 : 52

فَٰكِهِينَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡ وَوَقَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ

Wakifurahi kwa yale aliyo wapa Mola wao Mlezi. Na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni. info

Wakistarehe na neema alizo wapa Mola wao Mlezi, na Mola wao Mlezi akawalinda na adhabu ya Moto.

التفاسير:

external-link copy
19 : 52

كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Kuleni na kunyweni kwa raha kabisa kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyatenda. info

Wataambiwa: Kuleni chakula mpendacho, na kunyweni kwa raha, kuwa ni malipo ya vitendo mlivyo vitenda duniani.

التفاسير:

external-link copy
20 : 52

مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ سُرُرٖ مَّصۡفُوفَةٖۖ وَزَوَّجۡنَٰهُم بِحُورٍ عِينٖ

Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza mahuru-l-aini. info

Wakikaa nao wameegema juu ya makochi yaliyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza wake weupe wenye macho ya vikombe wazuri.

التفاسير:

external-link copy
21 : 52

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱتَّبَعَتۡهُمۡ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَٰنٍ أَلۡحَقۡنَا بِهِمۡ ذُرِّيَّتَهُمۡ وَمَآ أَلَتۡنَٰهُم مِّنۡ عَمَلِهِم مِّن شَيۡءٖۚ كُلُّ ٱمۡرِيِٕۭ بِمَا كَسَبَ رَهِينٞ

Na walio amini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima atapata alicho kichuma. info

Na walio amini, na wakastahiki vyeo vya juu, na vizazi vyao wakawafuata katika Imani, na wao hawajafikia daraja zile za baba zao, tutawakutanisha nao hao dhuriya zao, wapate kutulia nyoyo zao. Na wala hatuwapunguzii chochote katika thawabu za vitendo vyao. Wala wazazi hawatobeba chembe katika makosa ya dhuriya zao. Kwa sababu kila mtu amefungamana kwa rahani na vitendo vyake visio bebwa na mwenginewe.

التفاسير:

external-link copy
22 : 52

وَأَمۡدَدۡنَٰهُم بِفَٰكِهَةٖ وَلَحۡمٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ

Na tutawapa matunda, na nyama kama watavyo penda. info

Na tutawazidishia matunda mengi, na nyama kama waipendayo.

التفاسير:

external-link copy
23 : 52

يَتَنَٰزَعُونَ فِيهَا كَأۡسٗا لَّا لَغۡوٞ فِيهَا وَلَا تَأۡثِيمٞ

Watapeana humo bilauri zisio na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi. info

Huko Peponi watakuwa wakipeana kwa mapenzi bilauri zilio jaa vinywaji visio leta maneno yasiyo na maana wala vitendo vya dhambi, yaani havilevi na kuondoa akili.

التفاسير:

external-link copy
24 : 52

۞ وَيَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ غِلۡمَانٞ لَّهُمۡ كَأَنَّهُمۡ لُؤۡلُؤٞ مَّكۡنُونٞ

Iwe wanawapitia watumishi wao kama kwamba ni lulu zilizomo katika chaza. info

Na watakuwa wakiwapitia vijana walio wekwa kwa kuwatumikia, kwa weupe wao na usafi wao kama lulu iliomo ndani ya chaza.

التفاسير:

external-link copy
25 : 52

وَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَسَآءَلُونَ

Wataelekeana wakiulizana. info

Na watu wa Peponi watakabiliana wakiulizana wao kwa wao khabari za hayo mambo makuu wanayo yapata na sababu zake.

التفاسير:

external-link copy
26 : 52

قَالُوٓاْ إِنَّا كُنَّا قَبۡلُ فِيٓ أَهۡلِنَا مُشۡفِقِينَ

Waseme: Tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa; info

Kabla ya neema hizi sisi tulikuwa pamoja na ahali zetu tukiiogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
27 : 52

فَمَنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡنَا وَوَقَىٰنَا عَذَابَ ٱلسَّمُومِ

Basi Mwenyezi Mungu akatufanyia hisani na akatulinda na adhabu ya upepo wa Moto. info

Mwenyezi Mungu akatufadhili kwa rehema yake, na akatukinga na adhabu ya Moto.

التفاسير:

external-link copy
28 : 52

إِنَّا كُنَّا مِن قَبۡلُ نَدۡعُوهُۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡبَرُّ ٱلرَّحِيمُ

Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwenye kurehemu. info

Hakika sisi kabla ya haya tulikuwa duniani tukimuabudu Yeye tu. Yeye peke yake ndiye Mhisani Mkunjufu wa rehema.

التفاسير:

external-link copy
29 : 52

فَذَكِّرۡ فَمَآ أَنتَ بِنِعۡمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٖ وَلَا مَجۡنُونٍ

Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu. info

Wewe endelea na kukumbusha kama unavyo fanya. Kwani wewe, kwa neema ya Mwenyezi Mungu aliyo kuneemesha kukupa Unabii na akili iliyo timia, si kuhani anaye toa khabari za ghaibu bila ya ilimu, wala si mwendawazimu unaye sema usiyo yasadiki.

التفاسير:

external-link copy
30 : 52

أَمۡ يَقُولُونَ شَاعِرٞ نَّتَرَبَّصُ بِهِۦ رَيۡبَ ٱلۡمَنُونِ

Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari. info

Bali ati wanasema huyu ni mtunga mashairi, tunaye mngojea afikiwe na mauti!

التفاسير:

external-link copy
31 : 52

قُلۡ تَرَبَّصُواْ فَإِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُتَرَبِّصِينَ

Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia. info

Waambie kwa kuwatisha: Ngojeeni, na mimi nami ni katika wanao ngojea mwisho wa hali yangu na hali yenu!

التفاسير:

external-link copy
32 : 52

أَمۡ تَأۡمُرُهُمۡ أَحۡلَٰمُهُم بِهَٰذَآۚ أَمۡ هُمۡ قَوۡمٞ طَاغُونَ

Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu? info

Bali ndio akili zao zinawaamrisha waseme maneno hayo yanayo gongana. Kwani kohani na mtunga mashairi ni watu wenye fahamu na akili; na mwendawazimu hana akili. Lakini hawa ni watu walio pita mipaka katika inadi zao.

التفاسير:

external-link copy
33 : 52

أَمۡ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُۥۚ بَل لَّا يُؤۡمِنُونَ

Au ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini! info

Bali ati wanasema: Muhammad ameizua hii Qur'ani! Bali hawa kwa ukaidi wao hawaamini tu.

التفاسير:

external-link copy
34 : 52

فَلۡيَأۡتُواْ بِحَدِيثٖ مِّثۡلِهِۦٓ إِن كَانُواْ صَٰدِقِينَ

Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli. info

Basi nawalete masimulizi kama haya ya Qur'ani, ikiwa wao ni wasema kweli kuwa Muhammad kaizua.

التفاسير:

external-link copy
35 : 52

أَمۡ خُلِقُواْ مِنۡ غَيۡرِ شَيۡءٍ أَمۡ هُمُ ٱلۡخَٰلِقُونَ

Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? info

Kwani wao wameumbwa bila ya kuweko Muumbaji, au wao wamejiumba wenyewe, basi kwa hivyo ati ndio hawamtambui Muumbaji wa kumuabudu?

التفاسير:

external-link copy
36 : 52

أَمۡ خَلَقُواْ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ

Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini. info

Kwani wao ndio walio ziumba mbingu na ardhi kwa uumbaji mzuri wa pekee wa namna hii? Bali wao hawana na yakini na lolote lilio mwajibikia Muumbaji. Na kwa hivyo ndio wanamshirikisha.

التفاسير:

external-link copy
37 : 52

أَمۡ عِندَهُمۡ خَزَآئِنُ رَبِّكَ أَمۡ هُمُ ٱلۡمُصَۜيۡطِرُونَ

Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka? info

Kwani wao wanazo khazina za Mola wako Mlezi wanazo zisarifu watakavyo? Au wana nguvu za kutenda watakavyo, na kupanga mambo kama wapendavyo?

التفاسير:

external-link copy
38 : 52

أَمۡ لَهُمۡ سُلَّمٞ يَسۡتَمِعُونَ فِيهِۖ فَلۡيَأۡتِ مُسۡتَمِعُهُم بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٍ

Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi! info

Bali wanacho kipandio cha kupandia mpaka mbinguni wakasikiliza anayo yahukumia Mwenyezi Mungu? Kama hivyo, basi nawamlete huyo mtu wao anaye sikiliza atoe hoja iliyo wazi kuthibitisha madai yake.

التفاسير:

external-link copy
39 : 52

أَمۡ لَهُ ٱلۡبَنَٰتُ وَلَكُمُ ٱلۡبَنُونَ

Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana? info

Ati Mwenyezi Mungu ndiye mwenye mabinti, kama mnavyo zua, na nyinyi ndio mna watoto wa kiume kama ndio mnavyo penda?

التفاسير:

external-link copy
40 : 52

أَمۡ تَسۡـَٔلُهُمۡ أَجۡرٗا فَهُم مِّن مَّغۡرَمٖ مُّثۡقَلُونَ

Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama? info

Kwani wewe unawaomba chochote kuwa ni ujira wa kuwafikishia Ujumbe wako, ndio wamethakilika na hizo gharama wakalalimika?

التفاسير:

external-link copy
41 : 52

أَمۡ عِندَهُمُ ٱلۡغَيۡبُ فَهُمۡ يَكۡتُبُونَ

Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wameandika? info

Bali kwani wao wanao ujuzi kujua mambo ya ghaibu, yaliyo fichikana, na hivyo wanaandika kutoka hayo wayatakayo?

التفاسير:

external-link copy
42 : 52

أَمۡ يُرِيدُونَ كَيۡدٗاۖ فَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ هُمُ ٱلۡمَكِيدُونَ

Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao walio kufuru ndio watakao tegeka. info

Au wanataka kukufanyia vitimbi tu na kuuharibu Ujumbe wako? Basi hao walio kufuru ndio wanao stahiki kutumbukia katika vitimbi vyao.

التفاسير:

external-link copy
43 : 52

أَمۡ لَهُمۡ إِلَٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِۚ سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Au wanae mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Subhanallah! Ametaksika Mwenyezi Mungu na hao wanao washirikisha naye. info

Au wao wanae mungu wa kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu atakae walinda na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wanayo mshirikisha naye!

التفاسير:

external-link copy
44 : 52

وَإِن يَرَوۡاْ كِسۡفٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ سَاقِطٗا يَقُولُواْ سَحَابٞ مَّرۡكُومٞ

Na hata wange ona pande linatoka mbinguni linaanguka wange sema: Ni mawingu yaliyo bebana. info

Na wakiona kipande cha mbingu kinwaangukia kuwaadhibu wao husema, kwa inda tu: Ni mawingu yaliyo bebana!

التفاسير:

external-link copy
45 : 52

فَذَرۡهُمۡ حَتَّىٰ يُلَٰقُواْ يَوۡمَهُمُ ٱلَّذِي فِيهِ يُصۡعَقُونَ

Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapo hilikishwa. info

Waache bila ya kuwajali mpaka watakapo ikuta siku yao watapo angamizwa.

التفاسير:

external-link copy
46 : 52

يَوۡمَ لَا يُغۡنِي عَنۡهُمۡ كَيۡدُهُمۡ شَيۡـٔٗا وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa. info

Siku ambayo hila zao hazitawakinga hata na chembe ya adhabu, wala hawatapata wa kuwanusuru.

التفاسير:

external-link copy
47 : 52

وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ عَذَابٗا دُونَ ذَٰلِكَ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Na hakika walio dhulumu watapata adhabu nyengine isiyo kuwa hii, lakini wengi wao hawajui. info

Na hakika hao walio dhulumu watapata adhabu mbali na hii waliyo teseka nayo hapa duniani, lakini wengi wao hawajui hayo.

التفاسير:

external-link copy
48 : 52

وَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعۡيُنِنَاۖ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ

Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo simama, info

Wewe isubirie hukumu ya Mola wako Mlezi ya kuwapa muhula hao, na wewe kupata maudhi yao. Kwani hakika wewe umo katika hifadhi yetu na ulinzi wetu. Basi vitimbi vyao havitokudhuru wewe. Na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo amka.

التفاسير:

external-link copy
49 : 52

وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَسَبِّحۡهُ وَإِدۡبَٰرَ ٱلنُّجُومِ

Na usiku pia mtakase, na zinapo kuchwa nyota. info

Na tafuta usiku usiku nafasi ya kumsabihi, yaani kumtakasa, Mwenyezi Mungu, na mtakase pia wakati zinapo kuchwa nyota, yaani alfajiri.

التفاسير: